Rais Kikwete azindua Sera ya Elimu na Maabara

Rais Kikwete azindua Sera ya Elimu na Maabara

Mkuu, kwenye hii sera ya elimu iliyozinduliwa jana, ina mambo mengi mazuri zaidi ya elimu ya sekondari kuwa bure. Soma kwa makini ndipo utakapogundua kuwa hizi si kampeni za uchaguzi
 
Nakumbuka hata James Mbatia ameshiriki kikamilifu wakati wa kuandaa hii sera ijapokuwa sijamuona akishiriki kwenye uzinduzi
 
Ukimuona mtu anapinga kila kitu basi atakuwa na shida kubwa kwenye kichwa chake,

Hii sera ya elimu imebeba mambo makubwa na yenye manufaa kwa taifa letu,

Ni wapuuzi wachache ndiyo wanaweza kupinga au kubeza hatua hii ya serikali kuanzisha hii sera.
 
Serikali jana imetangaza elimu bure kuanzia primary hadi sekondary na kwa shule za private bei elekezi kutolewa! Pia baada ya maabara nguvu kuelekezwa nyumba za walimu! Elimu ya msingi miaka 10.

Hilo ni jambo jema kabisa nakubali, lakini je kwanini limekuja wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu? Je, ilisubiri uchaguzi tu? Kama si kampeni ya CCM ni nini?

Ukitaka kujua yaliyojiri jana soma magazeti ya leo : Majira, Mtanzania....n.k
Hiki unachouliza ni sawa na kusema kuwa kwanini wewe ulisubiri ulisubiri mama yako akakuzaa wewe kwanini wewe ulisubiri mpaka akakuzaa wewe badala ya wewe kumzaa kwanza!
 
Serikali jana imetangaza elimu bure kuanzia primary hadi sekondary na kwa shule za private bei elekezi kutolewa! Pia baada ya maabara nguvu kuelekezwa nyumba za walimu! Elimu ya msingi miaka 10.

Hilo ni jambo jema kabisa nakubali, lakini je kwanini limekuja wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu? Je, ilisubiri uchaguzi tu? Kama si kampeni ya CCM ni nini?

Ukitaka kujua yaliyojiri jana soma magazeti ya leo : Majira, Mtanzania....n.k

kkwanini ukawa hamjaungana miaka kumi iliyopita mnakuja kuungana juzi.
 
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ametimiza ahadi yake aliyoitoa Agosti mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, kwamba amekusudia kufuta ada ya shule za sekondari nchi nzima.

Akizindua Sera mpya ya Elimu na Mafunzo 2014 katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitangaza kufutwa kwa ada ya sekondari, kuanzia mwakani.

Kwa tangazo hilo, Bajeti ya mwisho ya uongozi wa Rais Kikwete itakayoanza kujadiliwa Mei mwaka huu, itatakiwa kuwa na fungu la kulipa gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitoa kwa watoto wao wanaosoma elimu ya sekondari katika shule za Serikali nchi nzima.

Kwa sasa wazazi wamekuwa wakilipa Sh 20,000 kwa shule za kutwa na Sh 70,000 kwa shule za bweni, ili watoto wao wapate elimu ya sekondari.

Ubora

Alisema sera hiyo imezingatia stadi za msingi ambazo ni kuandika, kusoma na kuhesabu, ili kuwezesha watoto kujengwa kwenye msingi mzuri na hata kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hilo limezingatiwa.

"Hata kwenye mpango wa BRN tumelizungumza ili kuhakikisha inatolewa elimu bora. Tusifanye mambo ya kuchekesha mtoto anafika madarasa ya juu hajui kuandika, kusoma na kuhesabu. "Kuanzia sasa kama mtoto anafika darasa la pili, hajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), ni bora asiende darasa la tatu…naamini watoto wakiimarishwa katika stadi za KKK itaondoa matatizo haya," alisema.

Tathimini ya Msingi ya Taifa kwa ajili ya uwezo wa wanafunzi katika KKK, kwa wanafunzi wa Darasa la Pili iliyofanyika mwaka jana, ilibaini kuwa asilimia 98 ya wanafunzi wa Darasa la Pili nchini, walikuwa hawaelewi wanachokisoma.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema, tathimini hiyo imefanywa kwa baraka za Wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), ili kupata taarifa kuhusu hali halisi ilivyo ya wanafunzi wa Tanzania kumudu stadi za KKK wanapofika Darasa la Pili.

Mafanikio

Mbali na mafanikio ya kufikia uwezo wa kuanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bure, huku msisitizo ukiwekwa katika utoaji wa elimu bora, Rais Kikwete pia ilitangaza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambayo yamefikiwa katika uongozi wake wa miaka kumi.

Rais Kikwete alisema sasa elimu imepewa kipaumbele katika sera na shughuli za serikali, ndio maana Bajeti ya Elimu, ndio kubwa kuliko bajeti zote.

Alifafanua kuwa mwaka 2005/06 bajeti hiyo ilikuwa Sh bilioni 6.7, wakati mwaka huu wa fedha imepanda na kufikia Sh trilioni 3.1.

Hatua hiyo ya kibajeti kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni ongezeko la mara tano ya Bajeti ya mwaka 2005 sawa na asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ambayo inatengwa kwa ajili ya elimu.

Katika suala la mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema imetoka Sh bilioni 56 kwa mwaka wa fedha 2005/06, hadi kufikia Sh bilioni 345 kwa mwaka huu wa fedha.

Aidha, kwa mwaka jana, wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliongezeka kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000.

Kwa upande wa shule za msingi, alisema zimeongezeka kutoka 14,000 kwa mwaka 2005 hadi kufikia shule 16,343 kwa mwaka 2014, huku shule za sekondari zikiongezeka kutoka 531 kwa mwaka 2005, hadi kufikia 4,576, mwaka 2014.

Idadi wanafunzi wanaojiunga na sekondari, Rais Kikwete alisema imeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi milioni 1.8.

Rais Kikwete alisema pia vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka vyuo 184 mwaka 2005 na kufikia vyuo 744 kwa mwaka 2014, huku vyuo vikuu vikiongezeka kutoka vyuo vikuu 26 mwaka 2005 na kufikia vyuo vikuu 50 kwa mwaka 2014.

Alikumbusha kuwa kama sio kuanzishwa kwa shule za kata, idadi ya wanafunzi pia isingeongezeka.

"Hali imebadilika, sasa wanafunzi wengi wanakwenda shule na vyuoni na suala la watoto na vijana kupata fursa ya kusoma, sio tatizo katika sekta ya elimu, sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha inapatikana elimu bora kwa kuboresha mazingira ya elimu," alisema Rais Kikwete.

Chanzo: Habari Leo
 
Ukimuona mtu anapinga kila kitu basi atakuwa na shida kubwa kwenye kichwa chake,

Hii sera ya elimu imebeba mambo makubwa na yenye manufaa kwa taifa letu,

Ni wapuuzi wachache ndiyo wanaweza kupinga au kubeza hatua hii ya serikali kuanzisha hii sera.

Lakini wehu hawakoekani watu kama yericko waliosafiri gari moja na mbuzi kazi kweli.
 
Nakumbuka hata James Mbatia ameshiriki kikamilifu wakati wa kuandaa hii sera ijapokuwa sijamuona akishiriki kwenye uzinduzi

mmefanya utafiti mkaona kuna serikali dunian zinatoa elimu bure.....?
Tatizo la ccm nikuiba sera nzuri za upinzan nani jambo njema lakini kwenye utekelezaji ndio kasheshe kama mlivyofanya kwenye katiba mpya.
Tujitahidi kutekeleza hii sera ili adui wa kwanza tumtupe mbali
 
uzuri wa jk akiahidi anatimiza sasa kathubutu kaweza na jambo la kushukuru anazidi kusonga mbele safi sana jk.
 
Yetu macho kama mpango huu utaendelea baada ya uchaguzi 2015
 
Hii michango atalipa nani,,?
1. Caution money
2. Ulinzi
3. Afya
4. Ujenzi.
5. Thamani
6. Vifaa vya usafi
7. Mahafali.
6. Tour
7. Ukarabati
8. Mitihani ya MOCK, INTER SCHOOL
9. ETC.
 
Tunaomba magufuli naye akiingia aendeleze haya mazuri ambayo jk ameyaanzisha ili kuzidi kulipa taifa letu maendeleo ya hadhi zaidi.
 
mmefanya utafiti mkaona kuna serikali dunian zinatoa elimu bure.....?
Tatizo la ccm nikuiba sera nzuri za upinzan nani jambo njema lakini kwenye utekelezaji ndio kasheshe kama mlivyofanya kwenye katiba mpya.
Tujitahidi kutekeleza hii sera ili adui wa kwanza tumtupe mbali
Serikali ya ccm ni sikivu. Inajali wananchi wake
 
Na watu huko mtaani wanasherekea , eti elim bure!!

Huuuhhhh!!!
 
Hongera rais wetu kwa kuliona hilo kwa 7bu watoto wa maskini wengi walikuwa wanakosa haki yao ya kupata elimu angalizo nashauri serikali idhibiti michango ktk shule zote za msingi na sekondari ni kikwazo kikubwa kwa wazazi.
 
Kwa nini hakufanya hayo wakati akiwa kiongozi????
Ameondoka kazini anashinikiza bajeti ijayo kwa wenzake anastahili ...........!!!!!!! Huyu
 
Mkuu, kwenye hii sera ya elimu iliyozinduliwa jana, ina mambo mengi mazuri zaidi ya elimu ya sekondari kuwa bure. Soma kwa makini ndipo utakapogundua kuwa hizi si kampeni za uchaguzi

Ukimuona mtu anapinga kila kitu basi atakuwa na shida kubwa kwenye kichwa chake,

Hii sera ya elimu imebeba mambo makubwa na yenye manufaa kwa taifa letu,

Ni wapuuzi wachache ndiyo wanaweza kupinga au kubeza hatua hii ya serikali kuanzisha hii sera.

Katika uzi wangu ukisoma kwa makini kabisa hakuna sehemu nilipopinga sera ya elimu bure, nimekubali kuwa ni jambo jema!
 
Back
Top Bottom