Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Mi naamini hakuna tatizo kwenye uteuzi huu uliofanywa na rais, hata kwa wale walioshindwa ubunge wana haki hiyo pia kwani kushindwa kwenye ubunge sio kigezo kuwa wewe hufai kwa lolote, na ukiangalia hizi chaguzi zetu bado zinatawaliwa na rushwa kwa kiasi kikubwa. Pamoja na kushindwa kwao lakini mkuu wao anajua utendaji wao. KWA SISI AMBAO HATUNA ROHO ZA VIKOROSHO TUNATOA PONGEZI KWA UTEUZI HUO.
 
Mods haya si matusi kwa mkuu wa nchi?
Chinchilla, Kisheria neno Mpuuzi sio kosa la kisheria. Tafsiri yake ni mtu asiyejali, anaye puuza mambo. Sasa naomba usijipendekeze kwa kwa Kikwete kwa kuwa kuna watu wako pale ikulu idara ya usalama kitengo cha mawasiliano wanafanya hii kazi ya kufuatilia social websites zote nchini. Kwa hili hamna kosa.
 
Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kuchanja mbuga.... JK kweli wewe ni chiboko!!
 
Nimewafurahia Dr. Batilda Burian na Dr. Kamala.

Kamala kupelekwa Ubelgiji ni mwisho wa Tanzania .Pale mahali ni muhimu mno kumpeleka Kamala ni hatari zaidi na kama huamini ngojea utaona ukweli huu.Balozi wa Belgium ndiye pia Balozi wa EU na Holland, Luxemburg sasa huyu Kamala ataweza ? Haya wacha tuone but we have lost big time .
 
hongera mh, rais fanya kazi yako katiba inakuruhusu na wanaobeza wanyamazie kama huwaoni, ipo cku watakukumbuka maana rais ajaye hatatoa ruhusa hy tena.

jamani mnaoshabikia kuwa anyamazage hata vitu vya msingi mnamponza. Kuna wakati ukimya ni dawa lkn si wakati wote.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-

(i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniCHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

(ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

(iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniKENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

(iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniUGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

(v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniMSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamzaalikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchiniOMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo(Consul General) nchini Dubai.

2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.

……………………………… MWISHO …………………………………….



(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI

IKULU,
DAR ES SALAM.

16 Desemba, 2011
 
Lazima tumkumbuke kwa mengi tu
#KUIKANA DOWANS
#HAJUI Y T'NIA NI POOR
#ALIANGUKA JANGWANI
#ALILINDWA NA SHEKH YAHYA
#ALIZ0MEWA UDSM
#ATALETA KATIBA AITAKAYO
#AMEKIGAWA CHAMA
#MWANAE ANAHUSISHWA NA UKWAS WA KUTISHA
#ONGEZEA
Mpe rais wetu heshima yake bwana mambo ya kumuita rais wetu kilaza sio heshima. Big up JK watu watakukumbuka sana ukitoka madarakani. Go go JK gooo............
 
Kamala kupelekwa Ubelgiji ni mwisho wa Tanzania .Pale mahali ni muhimu mno kumpeleka Kamala ni hatari zaidi na kama huamini ngojea utaona ukweli huu.Balozi wa Belgium ndiye pia Balozi wa EU na Holland, Luxemburg sasa huyu Kamala ataweza ? Haya wacha tuone but we have lost big time .

mkuu watajaza wenyewe waliomshindisha kwa kishindo, ingekuwa dr ameteua hivyo ningeumiza kichwa kufikiria teuzi. Don't waste your time to think abt de facto pres
 
Du! hata ile chupi chafu iliyotupwa jalalani na wana Arusha JK kaiokota na kuipeleka Kenya!! kweli tz nchi inayoendeshwa kifedhuli....sasa kenya atafanyaje kazi!!maana wa tz wengi waliopo kenya ni wakutoka Arusha na Moshi.........she is heading for disaster and scandles in Kenya....wait and see......
On a bigger note though.....this whole thing shows how ignorantly and redundantly this country(Tanzania)is run......

mkuu ondoa post yako kabla mod hawajaikuta, ban lake hapo tutaonana next yr
 
Just a formality, a protocol thing..... most of them are retired top spies na kabla nchi yeyote haijakupa diplomatic immunity, lazima wajue wewe uko vipi. Hata ukitaka kusafiri nje mataifa mengine hukucheck out.

Siku hizi kuna PR companies ambazo zipo chini ya lobbyists wa US, EU, China, Japan.. etc na ukitaka connections za kuonana na Obama, sarkozy, Merkel, Hu Juntao etc, unawalipa half a million halafu unasukiwa connection.


Hawa mabalozi hawan sana maana siku hizi, wala msilikuze hili, ni fadhila tu.


I can see, you have a point.
 
Ubalozi una maana kwa nchi zenye makoloni na ubepari uliobobea, wanawatumia kulinda interests zao, na siyo sisi ambao ndo makoloni yenyewe...
 
Back
Top Bottom