Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Tiote

Senior Member
Mar 6, 2011
139
36
Naupongeza uteuzi wa Mabalozi wapya uliofanywa na Rais Kikwete na kira gazes TBC1 hivi punde.

--------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-

i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.

2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.


========================
jk-mabalozi-1.jpg

jk-mabalozi.jpg
 
....Taarifa za muda mfupi ulipita ni kuwa Jk kateua mabalozi wa kutuwakilisha na wakimwemo B.Buriani aliyepigwa chini na Lema na Philip Marmo.....
 
Mabalozi wapya wameteuliwa na Rais kikwete na wanaanza kazi 12 Oct 2011. Walioteuliwa ni:

1. Batilda Burian....Kenya
2. Ali Salehe........Falme za Kiarabu
3. Ladislaus Komba.....
4. Philpo Marmo......China
5. Dr Kamala..........Belgium
Wengine majina yao sijayapata vizuri...


Source: TBC1
 
Wekeni list yote kama ipo badala ya kuweka nusu nusu. Jairo vipi hajatumbukizwa kwenye hiyo list?
 
Ikiwa ni kweli nchi itakuwa ni ya kulindana lindana. Sura zile zile, hivi hakuna vijana wanaofaa kuwa mabalozi?
 
Nimesikia kwamba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Jakaya
kikwete ameteuwa mabalozi wapya watakaowakilisha Tanzania katika Nchi
kadhaa majina ninayo machache

Philip Marmo ambaye ameenda Uchina

Batilda Burhani Ambaye ameenda Kenya

Mwenye orodha kamili atupe lakini inaonyesha wale walioshindwa ubunge
ndio wengi wamepewa nafasi za Ubalozi nchi za Nje na naomba kuuliza
kama teuzi hizi zinabaraka za Bunge au la .

Mabalozi hao wataapishwa Tarehe 19 mwezi huu
 
Rais amefanya uteuzi wa Mabolozi wapya miongoni mwao ni:
1)Dr.Deodoros Kamala- UBELGIJI
2) Dr Batilda burian-Kenya
3) Filip Marmo-Uchina
4)Ali Saleh-Oman
Na wengineo
Source TBC Habari
 
Iv na mi ningepigwa chini ubunge kumbe ningekula shavu ka Marmo. Daaah ushwaiba nchi hiii balaaa. Sawa baba Ridhi kwa kendeleleza ushwaiba. Hongera kilaza Marmo. Wasalimie China cjui au Ubelgiji cjui!
 
Wanaenda kumwakilisha jk siyo wananchi. Wananchi waliwatupa kwenye dust bin, Jk kaenda kuwaokota kwenye dampo.
 
*
*********** Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-
*
(i)*************** Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
*
(ii)************ Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
*
(iii)********** Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
*
(iv)********** Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
*
(v)************ Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
*
*
*
*
*
*
*
*
*
(vi)********** Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(vii)******* Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
*
(viii)***** Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.
*
2.******** Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011.* Wataapishwa tarehe***** 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.
*
………………………………********
 
Back
Top Bottom