Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

CHADEMA sasa wanawajibika kuonyesha usikivu na wao, maana ukisikilizwa na wewe wapasa kusikiliza.
Wameshasikilizwa sasa ni zamu yao kusikiliza.
 
Guys this is politics. Hivi kuna mtu yeyote mwenye akili yake alidhani kuwa JK hatasaini muswada ule?. Asinge saini angewasha moto mkubwa sana na wabunge wake wa CCM waliokuwa wakitoa povu ili kuwakomoa CDM. The movie is simple, saini muswada iwe sheria halafu peleka bungeni marekebisho ili ku-accomodate hoja za watu wengine. Ingekuwa ni provocation kama angesaini muswada kabla ya kukutana na CDM.

Kitu pekee ambacho anaweza kukichelewesha ni kuanza utekelezaji wa sheria kama kuteua wajumbe wa kusikiliza maoni. Kama atateua tume hiyo basi ni dhahiri kuwa hakuna la maana litakalofanyika. Kama mna kumbukumbu nzuri hata sheria ya uchaguzi aliitia saini kama huu muswada alioutia leo kabla ya kufanya marekebisho.

JK angeonekana ni msaliti mkuu kwa wabunge wa CCM kama asingeutia saini muswada huu, kitu ambacho kingemuweka pabaya kwenye kupitisha sheria zingine huko mbeleni.

Tusihofu wala ku-spin this out of control, issue si kuzuia muswada kutiwa saini issue ni kuzuia sheria mbaya kuanza kutumika. Haiingii akilini hata kidogo serikali hiyohiyo ipeleke muswada bungeni na wabunge wake waipishe halafu iwasaliti wabunge hao kwa kutousaini muswada huo. Ingekuwa sheria hii imeanzia bungeni JK alikuwa na sababu ya ku-VETO.

Kidogo kwa mbali umenitia moyo lakini yakiingia na kuletwa mambo ya kisiasa na sanaa,du naona itakuwa imekula nguvu ya Watanzania wanaoililia Tanzania.

Hofu yangu ni kuwa akitangaza tume basi ndio hivyo tena kwaheri Mwalimu Kwaheri tutaonana kesho!!!!!!!!!!!.
 
Hivi kulikuwa na haja gani ya makubaliano kati yake na chadema. Hivi ni kwanini kikwete hawezi kamwe kuwasikiliza wananchi? Hivi ni kwa nini kikwete anatuchukulia hivi watanzania? Hakika siamini kama duniani kote kuna kiongozi wa nchi mpenda mzaha ktk mambo ya msingi kama kikwete. Kwa kweli hii hali imenisikitisha sana.
 
Hili la ku-sign lilikuwa wazi kabisa. Rais Kikwete asingeweza kusaliti wabunge wa ccm maana kwa kufanya hivyo angekuwa amejimaliza. Ndani ya chama chake hali si shwari lakini Waziri mkuu kafanya kazi ya kusomesha wabunge wa ccm ili waukubali na wamefanya hivyo. Kama rais angekataa au hata ku-delay ku-sign angekuwa amepoteza karata yake ya mwisho - wabunge wa ccm. Kwa upande mwingine kama angekataa kukutana na CHADEMA nayo ingemletea shida!

Hata hivyo kwa ku-sign huu muswada Kikwete na CCM wanakuwa wamiliki (100%) including ubovu uliomo ndani yake! This is potentially dangerous kwa ccm na wasipokuwa makini (I dont know how) huu muswada - sasa sheria utawaletea shida, utawamaliza 2015. Makosa yalifanyika tangu bungeni.

Kwa upande wa CHADEMA, sasa wanakuwa na even more moral authority kukosoa mchakato mzima - kila hatua wanaweza kukosoa na most likely wananchi wengi watawasikiliza. Na watasema (CHADEMA) 'tuliukataa kuanzia bungeni, speech ya Lissu kwenye hansard za bunge ipo ikionesha mambo yote ya msingi yaliyoachwa na CCM" , pia CHADEMA watasema hata baada ya kutoka bungeni walifanya jitahada za kukutana na rais (kwa siku mbili) na kumueleza matatizo yaliyopo kwenye muswada pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuuboresha na kuufanya uwe wa kitaifa. Tukumbuke CHADEMA ndio waliomba kukutana na rais and not the other way round.

Hivyo basi, Kikwete amechora mstari, CHADEMA wanakuwa upande mmoja -wakitizama ni wapi CCM watakosea ili wapaze sauti -we said so...! Upande wa pili ni CCM wamebeba mzigo uliojaa utata, je mbeleko ya ccm itaweza kumudu uzito?
 
Ni hatua nzuri kwa maslahi ya katiba mpya,matakwa ya wananchi na utaifa wetu. Tunasubiri tuone matendo! Maneno yasimeze matendo baali matendo yameze maneno.! Tunahita katiba safi kwa ajili ya wananchi. Katiba itakayozaa serikali wanayoichagua wa Tanzania na itakayofanya kazi kwa ajili ya wa Tanzania. Mzee Mwinyi aliwahi kusema.."Tupingane" bila " Kupigana" na hatimaye tujali maslahi ya taifa letu.
 
Na wka upande mwingine asingeusaini, ingekwua vigumu sana kwa maoni ya Chadema kuingizwa kwenye shweria. Hivi sasa ameusaini, ni trahisi sana kuurudisha tena Bungeni ili ufanyiwe mabadiliko (amendments). kama angeurudisha kabla ya kuusaini, ni kweli ingezusha tafrani miongoni mwa wabunge wa CCM na wale waliouunga mkono muswada. hapa amewapiga bao la kisigino wabunge wake mwenyewe

Hapo kwenye red; absolutely true. Miaka ile tulifundishwa kwenye Somo la Siasa (siku hizi nadhani Uraia) kwamba mswaada ukipitishwa na Bunge (in fact Bunge makini), kuna mambo kama matatu yanaweza kutokea:-

(i) Rais aweza kuusaini kama ulivyo
(ii) Rais aweza kuurudisha Bungeni kwa marekebisho
(iii) Kukiwa na mvutano katika hayo mawili (i) na (ii) Rais anapaswa kulivunja Bunge na kuitisha Uchaguzi Mkuu.

Sasa kwa jinsi wabunge wa CCM na CUF walivyouchangia kwa ushabiki unaweza kuona mwenyewe katika hayo matatu ni lipi lilikuwa rahisi zaidi kwa Rais kulifanya.
 
Hili la ku-sign lilikuwa wazi kabisa. Rais Kikwete asingeweza kusaliti wabunge wa ccm maana kwa kufanya hivyo angekuwa amejimaliza. Ndani ya chama chake hali si shwari lakini Waziri mkuu kafanya kazi ya kusomesha wabunge wa ccm ili waukubali na wamefanya hivyo. Kama rais angekataa au hata ku-delay ku-sign angekuwa amepoteza karata yake ya mwisho - wabunge wa ccm. Kwa upande mwingine kama angekataa kukutana na CHADEMA nayo ingemletea shida!

Hata hivyo kwa ku-sign huu muswa Kikwete na CCM wanakuwa wamiliki (100%) including ubovu uliomo ndani yake! This is potentially dangerous kwa ccm na wasipokuwa makini (I dont know how) huu muswasa - sasa sheria utawaletea utawamaliza 2015. Makosa yalifanyika tangu bungeni.

Kwa upande wa CHADEMA, sasa wanakuwa na even more moral authority kukosoa mchakato mzima - kila hatua wanaweza kukosoa na most likely wananchi wengi watawasikiliza. Na watasema (CHADEMA) 'tuliukataa kuanzia bungeni, speech ya Lissu kwenye hansard za bunge ipo ikionesha mambo yote ya msingi yaliyoachwa na CCM" , pia CHADEMA watasema hata baada ya kutoka bungeni walifanya jitahada za kukutana na rais (kwa siku mbili) na kumueleza matatizo yaliyopo kwenye muswada pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuuboresha na kuufanya uwe wa kitaifa. Tukumbuke CHADEMA ndio waliomba kukutana na rais and not the other way round.

Hivyo basi, Kikwete amechora mstari, CHADEMA wanakuwa upande mmoja -wakitizama ni wapi CCM watakosea ili wapaze sauti -we said so...! Upande wa pili ni CCM wamebeba mzigo uliojaa utata, je mbeleko ya ccm itaweza kumudu uzito?
Kwa hiyo swala zima la Katiba Mpya ni la KISIASA! - Ndio mguu tuloanza nao na ajabu watu wameshindwa pia kutazama hapa.
 
I smell something here.......hiyo iliyopitishwa ni sheria ya kuunda tume kwa ajili ya kushughulikia katiba mpya na sio sheria/katiba mpya!

Wengi wetu huwa hatuelewi tunaishia kuconclude mambo bila ya uelewa kwa ufupi kuna kundi walitaka na wao wawepo kwenye hilo jopo/tume ili watafune na posho ila nadhani JK atawateuwa watu wa kada mbalimbali ili kusitokee manung'uniko. Narudia kusema tena kwa kinywa kipana mnachotakiwa ni kumwamini JK sidhani kama atapoteza fursa hii adhimu kuingia kwenye historia ya Tanzania ya miaka 200 ijayo! JK hana cha kupoteza kwenye hiyo katiba mpya nina imani kuwa atafanya vizuri kuliko wengi wetu tunavyodhani.

@Mohammed Shossi, soma kwa makini hii sheria aliyo-sign. Rais ataunda tume itakayokusanya maoni pamoja na kuandaa 'draft' katiba. Kwa kifupi Rais anatuandikia katiba mpya!
 
Sasa wamewasiliana vipi na umma kuhusu kilichowapeleka Ikulu?
Nadhani ni kupitia ile taarifa ya pamoja iliyotolewa jana. Ingawa ni fupi, lakini imebeba ujumbe mzito. Pia Mbowe na Lissu walizungumza na baadhi ya vyombo vya habari jana
 
Chuo cha maraisi kinatakiwa kwa hali na mali hapa kwetu TZ.Sababu kumbe hawajui hata wajibu wao kwa wananchi.Aiseeee!!!!!!!.
 
CCM na CHADEMA ni wadau wawili kati ya wadau wengi wenye interest na katiba mpya. CCM ina wanachama milioni tano, CHADEMA ina wanachama laki tatu na nusu. Watanzania tuko milioni 40. Kwa hiyo ukitoa watanzania milioni tano na laki tatu na nusu ambao ni wanachama wa vyama hivyo viwili bado unabaki na watanzania zaidi ya milioni 30.
Hivi mnadhani ni sahihi jamba linalohusu watu milioni 40 liamuliwe kwa maslahi ya watu milioni 5.35 tu?
Tafakari...
 
Wanabodi,
Lazima tufike mahali tuwe tunakubali matokeo!. Mbona statement ni nzuri tuu. Milango iko wazi kwa marekebisho yoyote. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu!.

Mkuu pasco umekuwa ukıkumbatıa sana muswada huu ntangu sessıons za Bunge zınaendelea na mpaka sasa umesıgnıwa na Raıs, nashındwa kukutofautısha na Wabunge wa CCM na CUF walıounga mkono kupıtıshwa kwa Muswada!
Nakufananısha na Prof Majımarefu kwa umbumbu na kushabıkıa muswada ambao ulıtakıwa ukatalıwe hatua za awalı kabısa kama ambavyo CDM na NCCR walıpendekeza. Kulıko kufanyıa amendments ya sherıa ambayo nı changa kabsa na kıuharısıa nı ufujajı mwıngıne wa pesa pasıpo ulazıma coz ıtaınvolve parlıamentaly debates whıch means wambunge watalamba posho tena kama kawaıda!
 
Du!. Nilijua alishausani ile Jumapili asubuhi kabla ya kukutana na Chedema!.

Kitendo cha kuusaini leo, ni uthibitisho kuwa JK ni rais msikivu na tena amewageshimu sana Chadema hadi kuwasikiliza kwanza kama wana hoja za msingi ndipo akausaini!.

Maadam umeshasainiwa, kazi sasa ni moja tuu, tuipe tume ushirikiano stahiki tupate katiba bora na sio bora katiba!.
Pasc u r disgusting. Tunajua unajipendekeza wala hujali madhara ya katiba mbuvu kwa vijavo ila punguza kaka.
 
Kwa hiyo swala zima la Katiba Mpya ni la KISIASA! - Ndio mguu tuloanza nao na ajabu watu wameshindwa pia kutazama hapa.

Hapo kwenye red; kwa TZ, na hasa kwa CCM ndio hivyo Mkuu. Tena si wao (CCM) tu, bali pia vyombo vyetu vya kisheria vinatuaminisha hivyo. Rejea Hukumu ya Mahakama ya Rufaa juu ya suala la mgombea binafsi lilivyoamuliwa na jopo la Majaji 7 chini ya Uongozi wa Jaji Mkuu wakiwapo wazee na "marafiki" kadhaa wa mahakama akina Prof. Palamagamba Kabudi. Habari ndio hiyo!
 
jamani kutia saini kuwa sheria sio maanake kwamba tusitoe maoni ni kuanzisha mchakato wa maoni. tutumie fursa hiyo ili tusije lalamika huko mbele
 
Back
Top Bottom