Rais Kikwete asaini Muswada wa Katiba

CCM wamesha piga bao mkuu hiyo proposal yako inaamanisha suala la kurekebisha katiba litahama kutoka CCM kuja CDM watu wapo busy wanatafuta credibility za 2015 tumefanya hivi na vile sasa CCM wao watasema tumerekebisha sheria wanachelewa hii hoja isipokwe na watu wengine. Sasa kama CDM wamedhamiria kidhati washiriki kikamilifu kupeleka maoni yao kwenye tume na pengine kuna na some sort of evidence ili kama haikufanyiwa kazi wananchi waamue hiyo siku ya siku (2015).

Kwa ufupi muswada umeshasainiwa na sasa umeshakuwa sheria.
#

Mkuu hoja si kuanzisha bali ni kupata katiba bora. Kama hatutopata katiba bora mchakato huu utarudiwa sooner or later. Sidhani kama katiba mpya itapunguza makali ya maisha kwa wananchi kuelekea 2015.
 
Du!. Nilijua alishausani ile Jumapili asubuhi kabla ya kukutana na Chedema!.

Kitendo cha kuusaini leo, ni uthibitisho kuwa JK ni rais msikivu na tena amewageshimu sana Chadema hadi kuwasikiliza kwanza kama wana hoja za msingi ndipo akausaini!.

Maadam umeshasainiwa, kazi sasa ni moja tuu, tuipe tume ushirikiano stahiki tupate katiba bora na sio bora katiba!.

Kaka huwa ninaheshimu sana hoja zako lakini kwa hapa nahisi umekuwa over jubilant,My apology kama niko wrong!

Hivi unaweza kuthibitisha kazi ya marekebisho itakuwa rahiosi baada ya kusaini ukilinganisha na kabla ya hapo?Ni nini political implications za kusaini na kisha marekebisho yakafanyika baadaye?Hebu tuwe realistic Pasco !
 
Guys this is politics. Hivi kuna mtu yeyote mwenye akili yake alidhani kuwa JK hatasaini muswada ule?. Asinge saini angewasha moto mkubwa sana na wabunge wake wa CCM waliokuwa wakitoa povu ili kuwakomoa CDM...
Na wka upande mwingine asingeusaini, ingekwua vigumu sana kwa maoni ya Chadema kuingizwa kwenye shweria. Hivi sasa ameusaini, ni trahisi sana kuurudisha tena Bungeni ili ufanyiwe mabadiliko (amendments). kama angeurudisha kabla ya kuusaini, ni kweli ingezusha tafrani miongoni mwa wabunge wa CCM na wale waliouunga mkono muswada. hapa amewapiga bao la kisigino wabunge wake mwenyewe
 
....# hakunaga Rais mwingine kama wewe, hakunaga!
....# hakunaga daktari mwingine kama wewe, hakunaga!


....# oya oyaa, kaa ukijua starehe ni gharama!!

.....# unibebe, unibebe, unibembeleze.....
Yani kama si haya madudu ya ufisadi,huyu jamaa hata mimi ningemfagilia mbaya sanaa...!

Huyu mtu anazifahamu siasa vilivyo...No wonder pamoja na mwalimu kutokumpenda bado alikuwa propagandist na kada maarufu tu wa chama!
 
Hivi kuna mtu alifikiri JK asingesaini ule muswada,hivi mlisoma vizuri yale makubaliano na CDM?

JK amekubali kufanyia marekebisho hiyo sheria na hilo hata CDM ndilo walilolitaka sasa tusubiri bunge la February kuona hayo marekebisho kinyume ya hapo tutaingia mtaani
 
Katika thread ya jana iliyosema"Re: Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa! ", niliandika ifuatavyo:
"Ukisoma katikati ya mistari utagundua kuwa kuna mambo hawakutaka kuyaweka wazi; lakini mimi naona rais amekubali kurudi hatua fulani nyuma.
Ukisoma kifungu cha kwanza; ina maana kwamba bunge kupitisha siyo mwisho, bado kuna nafasi ya kuboresha, baada ya rais kusaini ali mradi utumikaji wa sheria uwe haujaanza.
Maboresho hayo yatakuwaje ndipo tunakuja kifungu cha pili kwamba mawasiliano na mashauriano kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo yafanyike. Hapa wadau si ndio sisi - wananchi, jukwaa la katiba, dini mablimbali, NGOs wasomi nk. Hii ni diplomatic language kwamba rais amekubali maoni ya wadau mbalimbali yaendelee kupokelewa!
Mnajua kwa vyovyote vile isingewezekana kuandika wazi kuwa muswada unarudishwa kwa wananchi, hii ingemcontradict rais straight ukifikiria yale aliyozungumza na wazee wa dsm. Lakufanya sasa sisi wadau kwa makundi yetu mbalimbali tuwasilishe hoja za kuboresha sheria hiyo.Kumbuka hapa inaongelewa sheria, maana yake rais atakuwa ameshaisaini na kitakachofanyika ni serikali kuwasilisha bungeni muhtasari wa marekebisho kutegemea na hoja tutakazotoa sisi wadau - na hili ndilo Lisu aliliongelea isipokuwa sasa badala ya wadau kurudishiwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza, tunarudishiwa sheria ili mawazo yetu yatumike kuiboresha kabla haijaanza kutumika.

Kama kweli rais atakuwa tayari (kama siyo usanii) kuiambia seriakali yake kuwa mawazo yetu yaingizwe kwenye marakebisho then tutakuwa tumefaulu."

Ilikuwa wazi basi kuwa muswada utasainiwa then marekebisho yafanywe kwenye sheria kabla haijaanza kutumika.
 
Na wka upande mwingine asingeusaini, ingekwua vigumu sana kwa maoni ya Chadema kuingizwa kwenye shweria. Hivi sasa ameusaini, ni trahisi sana kuurudisha tena Bungeni ili ufanyiwe mabadiliko (amendments). kama angeurudisha kabla ya kuusaini, ni kweli ingezusha tafrani miongoni mwa wabunge wa CCM na wale waliouunga mkono muswada. hapa amewapiga bao la kisigino wabunge wake mwenyewe
Ikisha kuwa sheria ndio imetoka mkuu wangu, muda wenyewe uko wapi na huko Bungeni nambie hata kipengele kimoja cha sheria wabunge wa CCM hawakubaliani nacho maana kura ndio zitaweza badilisha lolote.
 
Hakuna mbwembwe Mkuu
Hivi Simba akikamata mawindo yake anataka mbwembwe? Fisi mwenyewe anauwawa kwenye process ili kuweza kuleta utulivu!(Sijawaita CDM Mafisi)

Kwenye hili ni JK 1 vs. CDM 0,hilo ni taka wasitake,naona walibweteka na ukweli kwamba wananchi wamechoshwa na CCM na kwamba wanataka mabadilko.

Wamejiingiza kwenye shimo baya sana,only time will tell...
 
Katika thread ya jana iliyosema"Re: Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa! ", niliandika ifuatavyo:"Ukisoma katikati ya mistari utagundua kuwa kuna mambo hawakutaka kuyaweka wazi; lakini mimi naona rais amekubali kurudi hatua fulani nyuma. Ukisoma kifungu cha kwanza; ina maana kwamba bunge kupitisha siyo mwisho, bado kuna nafasi ya kuboresha, baada ya rais kusaini ali mradi utumikaji wa sheria uwe haujaanza. Maboresho hayo yatakuwaje ndipo tunakuja kifungu cha pili kwamba mawasiliano na mashauriano kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo yafanyike. Hapa wadau si ndio sisi - wananchi, jukwaa la katiba, dini mablimbali, NGOs wasomi nk. Hii ni diplomatic language kwamba rais amekubali maoni ya wadau mbalimbali yaendelee kupokelewa! Mnajua kwa vyovyote vile isingewezekana kuandika wazi kuwa muswada unarudishwa kwa wananchi, hii ingemcontradict rais straight ukifikiria yale aliyozungumza na wazee wa dsm. Lakufanya sasa sisi wadau kwa makundi yetu mbalimbali tuwasilishe hoja za kuboresha sheria hiyo.Kumbuka hapa inaongelewa sheria, maana yake rais atakuwa ameshaisaini na kitakachofanyika ni serikali kuwasilisha bungeni muhtasari wa marekebisho kutegemea na hoja tutakazotoa sisi wadau - na hili ndilo Lisu aliliongelea isipokuwa sasa badala ya wadau kurudishiwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza, tunarudishiwa sheria ili mawazo yetu yatumike kuiboresha kabla haijaanza kutumika. Kama kweli rais atakuwa tayari (kama siyo usanii) kuiambia seriakali yake kuwa mawazo yetu yaingizwe kwenye marakebisho then tutakuwa tumefaulu. "Ilikuwa wazi basi kuwa muswada utasainiwa then marekebisho yafanywe kwenye sheria kabla haijaanza kutumika.
Well elaborated. Wengi hajaliangalia suala hili kwa sura hii
 
#

Mkuu hoja si kuanzisha bali ni kupata katiba bora. Kama hatutopata katiba bora mchakato huu utarudiwa sooner or later. Sidhani kama katiba mpya itapunguza makali ya maisha kwa wananchi kuelekea 2015.

Liangalie hili swala kwa jicho la tatu utasadiki niyasemayo. JK anao uwezo wa kuiacha katiba bora nani aliejua kuwa Amani Karume angeridhia makubaliano ya kumaliza uhasama na kuifanya Zanzibar iwe kitu kimoja (unguja na pemba)? aliwapuuza kina shamhuna na ali ameir na wahafidhina wengineo akasaini muswada ulioifanya zanzibar kutawalika vizuri.

JK ni msikivu na kwa kuwa kuna mambo mengi sana yametokea katika serikali yake nina amini atatuachia jambo ambalo kamwe hatutaweza kumsahau na litakalotufanya tusahau yote ya nyuma.

JK ni msikivu na nina imani kuwa atayafanyia kazi makabrasha ya cdm ili tuwe na katiba bora kabisa ambayo itamjengea sifa na pengine kuja kujishindia tuzo ya Mo Ibrahim.
 
Du!. Nilijua alishausani ile Jumapili asubuhi kabla ya kukutana na Chedema!.

Kitendo cha kuusaini leo, ni uthibitisho kuwa JK ni rais msikivu na tena amewageshimu sana Chadema hadi kuwasikiliza kwanza kama wana hoja za msingi ndipo akausaini!.

Maadam umeshasainiwa, kazi sasa ni moja tuu, tuipe tume ushirikiano stahiki tupate katiba bora na sio bora katiba!.

mzee wa kifungu cha 87...
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Novemba, 2011
So funny!!!!!!!!!!!!!
 
Oh,hii cngle itabamba hasa kwenye anti-vairasi
....# hakunaga Rais mwingine kama wewe, hakunaga!
....# hakunaga daktari mwingine kama wewe, hakunaga!


....# oya oyaa, kaa ukijua starehe ni gharama!!

.....# unibebe, unibebe, unibembeleze.....
 
Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Pamoja na mapungufu yote, makubaliano kati ya Chadema na Serikali yalikua ni kwamba Rais asaini kwanza muswada ili maoni ya chadema na wadau wengine yawasilishwe bunge lijalo kama schedule of amendments. Hapa JK ametimiza ahadi yake kwa Chadema. Tatizo ambalo tunaweza kujadili ni kama je, maoni yaliyowasilishwa na Chadema yana uzito? Na kama yana uzito kwa maslahi ya umma, je, yatazingatiwa yote? Hapo sasa!!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom