Rais Kikwete amtimua Mwenyekiti wa Bodi Bandari

Mkuu, Precision ni ya watu binafsi ingekuwa ATCL ndio inaruka kwenda Mbeya, ungekuwa na haki ya kumpongeza. Why tuue ndege ya Umma na tupongeze mabepari wanaoingiza pesa binafsi??

Kwa taarifa yako. Mwakyembe ameingia katika wizara hiyo ATCL ikiwa angani. Kwa sasa ATCL iko mahututi kama sio kaburini na sababu kubwa no makosa aliyoyafanya mwakyembe kumfukuza Chizi.

Usafiri wa treni ni mpango ulioanzishwa zamani sana mkuu fuatilia vema, isipokuwa ni kwamba umeanza kipindi ambacho Mwakyembe yuko madarakani. Unakumbuka yale mabehewa ya Uda yalibadilishwa ili kubeba abiria Dar kwa njia ya Treni? Mwakyembe wakati huo alikuwa bado Mbunge wa Afrika Mshariki,So amekuta mpango uko mwishoni na ndio sifa anayopata ingawa walistahili hawapo madarakani now

TRL wanafanya hiyo kazi tangu enzi za TRC na kitengo cha maintanence kinafanya kazi frequently

BTW

Mambo mengi yanatofanywa sasa ni utekelezwaji wa mipango ambayo ilianza zamani sana na ikawa katika pipeline. tatizo tumezoea kusifia end product badala ya initiator wa mpango mzima.

Tatizo tulilonalo Tanzania ni utekelezaji anyway; kwenye Mipango tupo fit. Nae katekeleza

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wana JFRais Kikwete amemtimua mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari TPA Rahael Mollel kuanzia tarehe 16 Januari.Badala yake Amemteua Profesa Msambichaka kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo

Huyu nae anajijitutumuaga kweli. Ni kama vile analala then akishtuka anafanya maamuzi
 
Mwenye Mbwa kamtimua mwenye Mbwa? mmmh hii ni senema tu
 
wakati mwingine mimi najiuliza kama ni wewe yule songoro wa kibaha sec school enzi za 1980's yule aliyekuwa mwenyekiti wa ccm kwenye kikundi cha maigizo cha shule!!! kama ni wewe naona ulikuwa uigizi kumbe ccm ilikuwa kwenye damu

Acha Imani za kishirikina kujifanya unaweza kuwajua watu kwa njia za Giza rudi kwenye Mjadala naona unamwaga CV yako kimtindo uonekane ulisoma Kibaha Seco!
 
Kwani wale Mawaziri Nyerere alokuwa anawafukuza wakikosea walikuwa wameteuliwa na nani? ina maana asisifiwe kwa kuwa yeye ndie aliemteua? Huna Record ya Kumsifia Jk kwa lolote japokuwa dhamira ya nafsi yako inakiri yapo alojiotahidi na kufanikiwa Badilika wenzio kina Mbowe (kwenye uzinduzi wa Barabara Hai)i,Slaa kwenye ( kukabidhiwa hati ya kujenga Hospital kubwa ya CCBRT) Zitto ( kwenye uzinduzi wa Barabara kigoma) wameshaanza kubadilika, ukimsifia kwa hili hutoitwa masalia wala hutotengwa kwenye Nyumba ya Ibada wala hutopoteza mashabiki wako humu! """ETI ASISIFIWE KWA KUWA YEYE NDIE ALIEMTEUA"""". Mbona aliemteua Kafulila a.k.a SISIMIZI kwenye uenezi chadema ndie aliemfukuza na bado alisifiwa!

Personal attack?!........
 
Wana JFRais Kikwete amemtimua mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari TPA Rahael Mollel kuanzia tarehe 16 Januari.Badala yake Amemteua Profesa Msambichaka kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo

Prof wa Chuo cha Mbeya yule Engineer?
 
hao ndio wanaotucheleweshea maendeleo, wanapewa majukumu makubwa kuisaidia nchi wanaenda kuneemesha matumbo yao,. kikwete hapo unapaswa kumulika hadi chini madudu ni mengi sana.bravo jk
 
Amini usiamini mkuu

Wengi hapa wamezolewa na ule mkumbo wa kumuona Mwakyembe kama MTUME aliyetumwa kuiokoa Bandari na hasa baada ya kuwatimua viongozi wa juu wa Bandari na kisha kuwatimua wajumbe wa bodi ya Bandari.

Lakini nakwambia serikali haipaswi kuweka siasa katika uendeshaji wa Bandari. Mwakyembe is fighting for popularity na hakuna zaidi. Mfano: Unakumbuka wale makarani aliodai wa TPA aliwakamata kwa rushwa eti wakitaka kuachia watu watoe mizigo na kukwepa ushuru??? Kesi imeishia wapi????

Kwa taarifa ile ilikuwa ni issue ya TRA na sio TPA sababu kilichofanyika ni kuwa kamishna wa forodha ndie aliyetoa msamaha kwa jamaa wenye mzigo na TPA haihusiki kwa namna yoyote na Mwakyembe akajikuta ameingizwa mkenge.

Unakumhuka issue ya wizi wa mafuta na makontena bandarini??? Nani amewahi kulalamika kuibiwa mafuta ama kontena lake?? Ukweli ni kwamba makampuni yote yanayoingiza mafuta Tanzania na nje yamekanusha kuwahi kuibiwa hapo Bandarini. Mwakyembe amekuwa kimya baada ya kuona ameingizwa mkenge pia.

Jana Mkurugenzi wake mpya wa TPA aliyemteua ametimuliwa na wabunge kutokana na porojo zake na kaambiwa akajiandae upya hadi jtano aende kuwasilisha ripoti. Yule mkurugenzi ni mjomba wa JK (take it from me) na hana utaalamu wowote wa kusimamia Bandari.

Mollel alikuwa ni mtu straight katika maamuzi na alikuwa akipingana na Waziri waziwazi pale waziri alipokuwa akipindisha sheria, Mfano alimpinga waziri kuwatimua wakurugenzi sababu ni kinyume cha sheria mtu kutimuliwa bila kupewa tuhuma na kuzijibu kisha kupewa onyo kama kuna makosa ama taratibu nyingine kufuata.

Ngoja tuone hii sinema inakokwenda lakini am telling you, Bandari inaelekea kuzimu under Mwakyembe!!
Mkuu mbona wanapoteuliwa hudai watoe vigezo vya kuteuliwa? Cheo ni dhamana na sio haki!
 
Mollel alikuwa ni mtu straight katika maamuzi na alikuwa akipingana na Waziri waziwazi pale waziri alipokuwa akipindisha sheria, Mfano alimpinga waziri kuwatimua wakurugenzi sababu ni kinyume cha sheria mtu kutimuliwa bila kupewa tuhuma na kuzijibu kisha kupewa onyo kama kuna makosa ama taratibu nyingine kufuata.

Ngoja tuone hii sinema inakokwenda lakini am telling you, Bandari inaelekea kuzimu under Mwakyembe!!

dah Mwana Mpotevu haya sikua nayajua kama ni ya kweli bado tuna kazi kubwa
 
Ndiyo haya tunayosema madaraka makubwa aliyonayo Rais wetu .....,............. hivyo inachukua muda mrefu kufanya maamuzi. Kama mamlaka kwenye ngazi kama hii angepewa waziri then Mwakyembe angesha shughulikia zamani.

kwa mtizamo wangu nafikiri tatizo lililopo ni kuwekwa madarakani na watu wenye fedha waliojipenyesha kwenye chama cha kijamaa..kwa maneno ya kawaida ubepari ulioingia kwenye ujamaa..
inakuwa ngumu sana kuwashughulikia..maana unafkiria bila wao usingekuwepo hapo.maamuzi yanazidi kuwa magumu..halafu wenye chama chao wanaishia kupiga makofi tu na kupata kiduchuuu..kulipiwa gesti, fedha za nauli na kaposho kidogo..FIKRA ZA MWENYEKITI ZIHESHIMIWE
 
Mollel alikuwa ni mtu straight katika maamuzi na alikuwa akipingana na Waziri waziwazi pale waziri alipokuwa akipindisha sheria, Mfano alimpinga waziri kuwatimua wakurugenzi sababu ni kinyume cha sheria mtu kutimuliwa bila kupewa tuhuma na kuzijibu kisha kupewa onyo kama kuna makosa ama taratibu nyingine kufuata.

Ngoja tuone hii sinema inakokwenda lakini am telling you, Bandari inaelekea kuzimu under Mwakyembe!!
Wewe kwa namna moja au nyingine lazima utakuwa mwathirika wa maamuzi ya Dr. Mwakyembe. Si bure!
 
Mshazoa ule msemo kua kufukuzwa kazi serikalini ni vigumu mpaka vikao,sijui upewe onyo ,safari hii hakuna ,kama baba zenu au wajomba zenu wezi watatimuliwa tu tushachoka sisi..mnapelekwa shule marekani na kodi za wakulima,mnaendesha ma lexus na kodi zetu mtatutambua mwaka huu.Viva mwakyembe..Mjomba hongera zako hapo umechelewa but tutafanyaje
 
Mollel alikuwa ni mtu straight katika maamuzi na alikuwa akipingana na Waziri waziwazi pale waziri alipokuwa akipindisha sheria, Mfano alimpinga waziri kuwatimua wakurugenzi sababu ni kinyume cha sheria mtu kutimuliwa bila kupewa tuhuma na kuzijibu kisha kupewa onyo kama kuna makosa ama taratibu nyingine kufuata.

Ngoja tuone hii sinema inakokwenda lakini am telling you, Bandari inaelekea kuzimu under Mwakyembe!!

Acha kutuaminisha siasa zako! Hatuhitaji ushahidi wala kuipa bodi ya bandari tuhuma zozote ili wazijibu, bandari inanuka kwa rushwa na ufanisi wake ni mdogo, nenda hata kawaulize watu rwanda, burundi, congo mpaka zambia wanalijua hilo. Hata wew unayajua haya sasa unataka tuwabebe mgongoni. Piga chini wameshindwa kufanya kazi bora kwa watanzania
 
Back
Top Bottom