Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Wakuu sAlaam.
Hayo hapo juu ni baadhi ya matunda mabovu ya uongozi katika taifa , kama inavyoelezwa Richmond ni mali ya nani basi tuelezwe na hizo ni mali ya nani na ni nani aliyesababisha ubadhirifu mkubwa kiasi hicho tena wa aibu kwa vizazi vya leo na vinavyokuja.
 
wameziba masikio halafu wanasema hapa kazi tu. kura yangu ni UKAWA TU.
 
Tuelezwe na hayo ili tuchague vizuri mwaka huu, sio tuzidiwe maendeleo na Burundi wasio na utalii wala rasilimali bado tucheke
 
Mnapokuwa na viongozi wakuu halafu Yale mambo mazito yaliyoyumbisha misimamo ya nchi halafu wanatoa majibu kama wakina Aunt Ezekiel au Wema inaleta mashaka sana. Na mashaka yanaongezeka pale sisi wananchi tunapopokea majibu hayo kwa bashasha ya ushabiki kama mazuzu.
Mile nadhani mkuu anatudharau sana Watanzania hasa kwa vile tulimchagua wakati yeye mwenyewe alikuwa anajua hawezi hiyo kazi.
Serikali inaendeshwa kama bongo movie na ndio maana wanaukaribu sana
 
Jamani izo ndo kauli za Rais wetu JK tumpendae!
 
Natamani sana kutawaliwa na Rais Fisadi, mgonjwa na asiyejua kuongea vitendo A, nimechoka kuoingozwa na Wasafi, wenye afya njema na waongeaji wazuri vitendo F.
 
Uko sawa kabisa. Ni kweli CCM wangekuwa wameshaanika kila kitu hadharani. Wanajua mhusika mkuu ni nani ndio maana wanapata kigugumizi.
Mkuu hilo liko wazi kabisa nawashangaa wanaccm wanaoendelea kubwata kuhusu uhusika wa ENL kwenye richmond wanashindwa kujiuliza viswali vidogo kama hivi!
 
Mie sijui...hebu nielezee kwa ushahidi ili na mie nielewe kama wewe!...kama huwezi basi huna tofauti na wambeya wengine km wale walosema simbachawene kafumaniwa na mke wa mtu kumbe uzushi tu!...rais wako anamtaka Lissu ndo aseme wakati Lissu kashasema muhusika JK anataka aseme nini tena?
sasa zamu ya JK kusema toa ushahidi. UONE MOTO WAKE. Lisu atamkii hiv hiv kesha kamata nondo za kiwakili.
Nakuambia mchezo hapo nukta JK kimyaaa... kama atatamka hiyo kitu utaniambia
 
kikwete ameshawahi kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa hajui mmiliki wa dowans na richmond leo kamaliza muda wake anasema anamjua
Ndio mana wanakimbia midahalo. mana pale maswali ni ya papo kwa papo.
Halafu kuna umuhiku wa UKAWA kuunda kitengo wawe wanafuatilia nyeti hizi tuletewe ni gazeti toleo lipi na taarifa ianikwe.
 
Kiwete aliomba Li's amtaje mhusika was Richmond. Jamaa akamtaja Jana Morogoro. Mjadala umeisha.

Jk kumpa kazi Lisu ya kumtaja mtuhumiwa ina maana kwamba Jk anajua kwamba Lisu anamjua.kwa hiyo Lisu atakapomtaja naamini jk atakubali na asilete ubishi.
 
Jk kumpa kazi Lisu ya kumtaja mtuhumiwa ina maana kwamba Jk anajua kwamba Lisu anamjua. Kwa hiyo Lisu atakapomtaja naamini jk atakubali na asilete ubishi.
Mbona Lissu keshamtaja na Kikwete keshakubali na hana ubishi tena.
 
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” Eeehh ? Sasa wasubiri nini..!?
 
kikwete sijuwi anafikiri kwa kutumia kiungo gani sasa kama lowasa muhalifu basi wewe ndie amiri jeshi mkamate basi
 
time will tell,
mtaelewa tuu sasa tingatinga limeshaanza kupiga jaramba

Yaani mnavyomuita Magufuli Tingatinga mnamdhalilisha kwani Tingatinga ni li mtambo ambalo ili liweze kufanya kazi ipasavyo ni lazima liwekewe mafuta na kuongozwa na muendesha mitambo bila kufanya hivyo haliwezi kufanya chochote kwa hiyo kwa kumuita hivyo ni dhahiri Magufuli atakuwa ni Mtambo ambao ili ufanye kazi lazima uongozwe na Kikwete na Mkapa.
 
Anko jei hueleweki eleweki hv. We uko upande gani

USEMALO NI KWELI KURA YANGU NI 1 NA HAIWEZI GAWANYIKA INGAWA MPAKA SASA NIPO KATI NA LAZIMA NIPIGE KURA, NASUBIRIA MAMBO MAWILI (1) MDAHALO WA WAGOMBEA (2) UAMUZI WA AZIZI WA IGUNGA KUTANGAZA HADHARANI ANASAPOTI MAMVI NA UKAWA. IKIWA UKAWA WATAKWEPA MDAHALO KURA INAENDA ACT, IKIWA AZIZI ATAENDA CDM KURA INAENDA SSM. sijui hapo umenielewa??
 
Back
Top Bottom