Rais Kikwete akutana na uongozi wa NCCR Mageuzi - Ikulu

Kwa maisha anayoishi kama mwenyekiti wa chama, kina Kafulila hawawezi kuwa na nafasi ndani ya chama. Hata hivyo namsikitikia sana Machali. Nimekuwa mjini Kasulu kwa siku zaidi ya 5 kuanzia tarehe 13 mwezi huu. Hali ya kisiasa kwa Machali na chama chake mjini hapo ni ya mashaka sana.

Mkuu tuombe uhai kwani 2015 si mbali.Hiki chama hakitapata hata diwani mmoja.Nani atachagua vyama vya hovyo hovyo ambavyo vinanuka migogoro kila kukicha.Vyama ambavyo Mwenyekiti ni Mungu mtu na atakayemsema tu anafukuzwa uanachama? Shame on Mbatia and his gang!
 
Hawana lolote hao kazi kucheka cheka tu.
Washa nunuliwa kama CUF.Njaa mbaya.


​Duh hakika kuna ulazima wa katiba mpya na sio mpya katiba
 
Ikulu kuna ni? Kila chama wanapigania kwenda kumwona rahisi maana sasa siyo rais tena
 
Kwangu mie nisiye na chama NCCR,bado wananafasi ya kubadilika na kutanguliza UTAIFA KWANZA.Ni chama kwongwe kwenye siasa za mageuzi Tanzania lakini ni chama kilichopteza mvuto kwa umma,Na juio wa swala la kijana Kafulila ndio umechafua kabisa tasira ya chama hiki kwa umma.

Nimatumaini nao nafasi kama hii ya kuonana na Rais wataitumia vizuri kuwakilisha Watanzania katika hali ya kawaida huku wakiendelea kuasahihisha makosa yao.Ila kwangu nawaona NCCR_MAGEUZI ni kama chama kinachoitaji mageuzi makubwa kama jina leke lilivyo ili kiweze kukidhi matakwa ya Watanzania wa kileo yani kizazi kipya ambao wengi sasa maisha yao ni ya mchakamchaka.Hivyo kubadilika kwa safu ya uongozi wa juu,kutaleta picha nzuri ndani ya chama hicho ambacho miaka kumi iliyopita kilikuwa ni chama number moja.

Muonekano wake wa kuwa ni tawi la CCM,kwa viongozi wake wakuu kupishana na kauri na baadhi ya watu mashuhuri Tanzania katika kupigania maslahi ya Taifa,kumekifanya chama hiki kikose wananchama na wapenzi damu changa ambao ni muhimu sana kwa zama hzi za sasa.Hakika mabadiliko kwenye safu ya uongozi na aina ya siasa kinachotumia za Mwenyekiti kuonekana katika Radio na Televisheni kama Mtu Mlalamishi wa Maswala muhimu ya kitaifa dhidi ya wenzie kumechangia chama hicho kukumbwa na anguko licha ya kuwa bado kinasupport kwa baadhi ya wanachama ambao wengi ni watu wazima sana.

Ubora wa chama sio mfumo wake wa uongozi wake uko imara kiasi gani bali ubora wa chama ni jinsi kinavyokubalika kwa umma na kupata wanachama na wapenzi wapya wanaokisaupport chama husika.Tufike sehemu vyama vya kisiasa vitambue umuhimu wa kujiangalia na kujipima ni jinsi gani kinapokewa na wananchi wake na sio viongozi kuwa na jeuri na kiburi kwa kuwa wana ruzuku ya kuendesha chama [Wazungu wanasema as usual] kwa kiswahili tunasema kama kawa.

NCCR kazi nzuri kwa kupeleka mawazo yenu ikulu lakini you guys kwa nia njema ya TAIFA you need to change.Kwa kuwa kuoza na kuharibika kwa chama au vyama vya upinzani ni kukaribisha bomu baya la kukosa walinzi wa uwajibikaji ndani ya Serkali na chama tawala.Kwa kuwa Taifa la watu makini uzaa vyama vyenye itikadi makini.Sio siri uongozi wa juu ndani ya NCCR unaitajika kupigwa chini wote kisha kupanga safu mpya.Tena ninapata shida sana kuwa wanamtaalmu mzuri sana wa sheria Dk Mvungi inakuaje wanapoteza alama ya kukubalika kitaifa kama watu walio mbele kutetea maslahi ya Taifa kuliko kukubali Wananchi kuwaona kama ni tawi la CCM.

NCCR -MAGEUZI YOU NEED A BIG CHANGE SERIOUSLY.
 
Taratibu ndio mwendo. Tutamzoea tu hata kama baadhi tulimkataa> Na hao wengine si wanafuata?
 
watanzania inabidi tijiombee sana maana tumejaa upumbavu, ujinga, ushabiki, uchoyo na ulafi. Kwa sasa hatuna jipya maana Kikwete amekuwa kikwete, CUF imekuwa CUF na mengineyo. Kama inawezekana tuingie barabarani, au tuwafate mafisadi tukianzia na mkubwa maana wameuza nchi.
 
Usanii wa Kikwete ni muda mrefu, unapokuwa na Taisoni, ukajumlisha na waziri wa micharazo na utamadini....mh!

Sie macho kuuona mwisho wa mchezo huu wa katibu..mpya!

Regards
Josam
 
HUYU MACHALI HAJUI KAMA SUTI INAPELEKWAGA DRI CLEANER HEE,SASA HILO KOTI SIJUI ALIKUWA ANAPIGIA PASI YA MKAA IKAKAMATA KAZI KWELI KWELI ETI nccr NAO WAMO DU
 
Tunaomba na Chama cha waalimu, CWT waende kumuona rais kwa ajili ya manufaa ya nchi, wanahandisi nao kupitia ERB na IET tuende tukamuone mhe rais, vyovyote vile iwe lakini tunahitaji kutoa huu ushuzi wa kuwaachia wanasiasa kila kitu kutuamlia kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu. Sasa ni wakati wa kuanza harakati za kukataa porojo ni wakaati wa kufanya kazi kwa kila kundi kuheshimu mipaka ya kazi/taaluma zake bila kuingilia za wengine.
 
Back
Top Bottom