Rais Kikwete akutana na uongozi wa NCCR Mageuzi - Ikulu

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Ujumbe toka Ikulu:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi) kimempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusimamia suala la Katiba vizuri na kwa umakini mkubwa.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bwana James Mbatia ametoa pongezi hizo leo jioni alipofika Ikulu, akiongoza ujumbe wa viongozi wenzake sita(6), kuja kujadili suala la Katiba Mpya ya Tanzania.

"Tunakupongeza kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala zito ambalo litatupa uhai vizazi na vizazi vijavyo". Amesema kama utangulizi wa ujio wao Ikulu.

"Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya Katiba kwa amani na hoja bila kuvuruga amani yetu” Bwana Mbatia amesema na kuongeza kuwa “suala la Katiba linahitaji ushirikiano wa pamoja kwa nia njema, kwani taifa hili ni letu sote" ameeleza.

Akiwakilisha hoja ya NCCR-Mageuzi kwa Rais Kikwete, Mkuu wa Idara ya Sheria wa NCCR-Mageuzi Dkt. Senkondo Mvungi amesema, NCCR - Mageuzi inatambua ukubwa wa jambo hili la wa Tanzania kupata Katiba.

"Ni jambo kubwa sana, wewe ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata katiba mpya na kuanzisha Mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Kikao cha leo cha Rais na viongozi wa NCCR-Mageuzi ni mwendelezo wa jitihada za Rais Kikwete, kusikiliza, kuchukua maoni na mawazo ya wadau mbalimbali kutoka vyama vya siasa, asasi za kijamii na makundi mbalimbali katika kuelekea mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania.

Rais amesema kuwa nchi hii inayo Katiba ambayo imelilea vizuri na kulifikisha Taifa la Tanzania hapa lilipo, lakini pia Taifa linahitaji Katiba inayoendana na wakati na itakayoweza kulilea Taifa hili kwa miaka mingi ijayo.

Mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa NCCR-Mageuzi, Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo yao yalioanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2011, kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania.

Katika mazungumzo haya na Vyama vya Siasa Rais amesisitiza kuwa lengo la mazungumzo haya yote ni kuhakikisha kuwa hatimaye Watanzania wote watakiri kuwa Katiba Mpya ni yao wote na hatimaye ifikapo mwaka 2015 nchi iweze kufanya uchaguzi wake na Katiba Mpya.


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,
Ikulu.
Dar es salaam.
21 Januari, 2012

PICHA:
magari-nccr-ikulu.jpg

nccr-wakisubiri.jpg

mbatia-kikwete.jpg

NCCR-Kikwete.jpg

mvungi-kikwete.jpg

machali-kikwete.jpg

kikwete-na-nccr.jpg

mapendekezo-nccr.jpg

mvungi-akiwasilisha.jpg

kikwete-akiwasikiliza.jpg

team-nccr-ikulu.jpg

jk-akiwakosoa.jpg

juice-ikanyweka.jpg

nccr-wakiondoka.jpg

picha-ya-pamoja-nccr.jpg

nccr-wakiagwa.jpg

nchimbi-kikwete-machali.jpg

kikwete-mbatia.jpg

mvungi-kikwete-kuagana.jpg
 
Sam Ruhuza bado anapambana na Kafulila huko Kigoma? Simuoni! Ikulu kumbe patamu namuona Dr. Mvungi anachekelea kwelikweli!
 
Hawana lolote hao kazi kucheka cheka tu.
Washa nunuliwa kama CUF.Njaa mbaya.
 
Tulishaanza kumsahau Mbatia...kumbe naye yupo

Kwa maisha anayoishi kama mwenyekiti wa chama, kina Kafulila hawawezi kuwa na nafasi ndani ya chama. Hata hivyo namsikitikia sana Machali. Nimekuwa mjini Kasulu kwa siku zaidi ya 5 kuanzia tarehe 13 mwezi huu. Hali ya kisiasa kwa Machali na chama chake mjini hapo ni ya mashaka sana.
 
hivi kwa nini? Nchi hii watenda mema wanatoka chadema tu?.acheni ushabiki wa kijinga.au jf siku hizi ni ya cdm tu.si watanzania tusio na vyama na ambao ni wengi kuliko nyie mashabiki wa vyama mnatukwaza,humu kila ki2 cdm!na kuponda wengiof
 
who cares about NCCR MAgeuzi anymore after mrema bolted without bidding anybody who cares bye-bye?
 
Sina chuki na NCCR-Mageuzi au Ikulu lakini ni wazi kuwa sababu za Mbatia kwenda Ikulu ni kumpongeza JK na kupiga picha za ukumbusho. Taarifa ya Premi haina jambo lolote na hakuna mchangiaji JF aliyedokeza kilichoongelewa.
 
hivi kwa nini? Nchi hii watenda mema wanatoka chadema tu?.acheni ushabiki wa kijinga.au jf siku hizi ni ya cdm tu.si watanzania tusio na vyama na ambao ni wengi kuliko nyie mashabiki wa vyama mnatukwaza,humu kila ki2 cdm!na kuponda wengiof

Mkuu kimboka one
Acha kutoka povu utapata pressure bure.Nani kakunyima kuwasifia hao NCCR kama kuna lolote la maana unaona wanalifanyia Taifa?.JF ni mtandao huru.Kila mtu yuko huru kutoa mawazo yake alimradi havunji kanuni za JF
 
Jk bana kama kawaida mwendo wa Kahawa na Kashata za Yemen..

Mbatia kucheka tu yeye Wasira nae achezi mbali na JK.
 
Sina chuki na NCCR-Mageuzi au Ikulu lakini ni wazi kuwa sababu za Mbatia kwenda Ikulu ni kumpongeza JK na kupiga picha za ukumbusho. Taarifa ya Premi haina jambo lolote na hakuna mchangiaji JF aliyedokeza kilichoongelewa.

Mkuu si umeona taarifa yao jinsi walivyomimina sifa kwa JK na serikali yake? Ukisema hao ni CCM C utakuwa umekosea?
 
CUF nao wataomba kukutana tena!!!usicheze na soda za ikulu.

Unaweza kuniangalizia kwenye ratiba sisi wa DP ya Mwenyekiti wangu Mtanganyika C. Mtikila tumepangiwa kukutana lini??
 
Back
Top Bottom