Rais Kikwete akabidhi Polisi Magari 399 mapya kati ya 777 leo Kurasini jijini Dar es Salaam

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amewakabidhi Askari Polisi Magari 399 mapya kati ya 777 yaliyoagizwa
ili kufanikisha Shughuli ya Uchaguzi.

Magari haya yatawasaidia Polisi kufika Sehemu Mbalimbali kwa Wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi.

Naye Naibu IGP Abdulrahman Kaniki kamshukuru Rais kwa kuja kuungana nao. Kasema "Kwa wale wachache ambao wanataka kutulazimisha kutumia shuruti, hatutasita kufanya hivyo na hatutakua na ajizi kwa sabuabu hilo ni jukumu letu tulilopewa kisheria na tutahakikisha kwamba sheria inachukua mkondo wake.

Lakini pia nikuhakikishie kuwa, hatutamuonea mtu wala hatutampendelea au Kumuogopa mtu kwa nafasi yake yoyote aliyo nayo. Sisi ni kuhakikisha kwamba sheria inachukua mkondo wake na nchi inaendelea kuwa na amani kama ilivyo kisiwa cha amani.

Vifaa hivi tulivovipata tutahakikisha tunatumia kwa uangalifu na utaratibu uliopo ili vilete tija kwa sababu tunatambua kwamba ni kodi za watanzania zimetumika kupata magari haya na vifaa vingine.

Tunakushukuru kwa kuja kuungana nasi katika tukio hili.



======================================

p1.jpg


p2.jpg


p3.jpg


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe, IGP Ernest Mangu wakati akikagua sehemu ya magari mapya 399 kati ya 777 aliyokabidhi kwa jeshi la polisi leo Jumanne Oktoba 20, 2015 huko katika Chuo cha Polisi Kurasini Dar es salaam.

PICHA NA IKULU
 
Last edited by a moderator:
I wish ningesoma haya
  • Rais akabidhi ambulances 777
  • Rais akabidhi certificates of good performance to professors 777
  • Rais apokea hati ya achievement for leading the country from being one of the poorest country to a leading economy in Africa

Otherwise nyingine ni mbwembwe tu na vitisho

Imagine siku nne kabla ya uchaguzi, unakabidhi vitisho kwa wananchi
 
Mmmmh kweli hataki toka madarakani..
777 yote hayo hata kama ni 100mil ni hela nyingi sana
 
I wish ningesoma haya
  • Rais akabidhi ambulances 777
  • Rais akabidhi certificates of good performance to professors 777
  • Rais apokea hati ya achievement for leading the country from being one of the poorest country to a leading economy in Africa

Otherwise nyingine ni mbwembwe tu na vitisho

Imagine siku nne kabla ya uchaguzi, unakabidhi vitisho kwa wananchi


Rais azindua vituo vya afya kila kata.
Rais akomesha ufisadi.
Rais kukarabati shule mbovu nchi nzima.
Rais kuongeza mishahara watumishi wa umma.
Rais kuzindua reli ya kisasa kwenda nchi jirani.
 
Vile vile zitakuwa chache sana. Chukua vituo vya kupiga kura takriban 60,000. Gawa kwa gari 777. Ina maana gari moja litahudumia vituo vya kupiga kura kama 77. Wapi na wapi!
 
Duh! Kweli ameamua kunoresha jeshi la polisi, the only problem n timing
 
Upumbavu wa CCM ndio huu

Hospital hazina ambulance

Shule hazina madawati

Mabadiliko lazima

Garama zote hizo, sababu kuu ni kubaka democracy.

Shida zako unaweza tueleza tangu asubuhi hadi jioni na usifikiri hatuzijui.
 
Back
Top Bottom