Che Guevara
JF-Expert Member
- May 22, 2009
- 1,236
- 350
Wakati wa Kagame kuachia ngazi umefika. Akiendelea kukaa madarakani atavuruga mafanikio yote aliyoiletea Rwanda. Kinachomsumbua ni paranoiya inayotokana na mikono yake kujaa damu nyingi tokea alipoitungua ile ndege ya Habyarimana.
Yeye bado ni kijana akitaka azeeke vizuri na kwa usalama, basi inabidi ajitahidi aachie ngazi wakati mambo ni mazuri. Akichelewa yakaharibika sio ajabu akawindwa kama wengine ili na yeye ajibu mashitaka ya mauaji aliyoamrisha.
Mkuu, nina uchungu zaidi na nchi yangu TZ kuliko Rwanda. Nafikiri itakuwa poa sana kama tutaondoa jina la Kagame hapo juu (nimepigia mstari chini) na kuweka la Kikwete.
Wakati wa Kikwete kuachia ngazi umefika.
Zipo sababu halali 51 (Ref. Mwanakijiji).