Rais Kagame aishutumu Tanzania


Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
15,310
Likes
7,642
Points
280

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
15,310 7,642 280
5th March 10

Rais Kagame aishutumu Tanzania

Mwandishi Wetu

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameituhumu Tanzania kwamba inaruhusu watu wanaoipinga Serikali yake kuendeleza harakati za kuhujumu nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali juzi na taarifa zake kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Kagame alisema atawasiliana na Tanzania ili watu hao wanaoendesha harakati hizo wakamatwe.

Mbali na Tanzania, Kagame pia aliitaja Kenya na Uganda kwamba kuna watu kama hao wanaoendesha harakati dhidi ya serikali yake, lakini akaapa kwamba kamwe hawataweza kuiangusha serikali yake.

Katika mkutano huo, Kagame pia alimshambulia mshirika wake wa zamani wakati wa mapambano ya kuikomboa Rwanda, Luteni Jenerali Kayumba Nyamwasa ambaye alikuwa balozi wa nchi hiyo nchini India kwamba ni miongoni mwa watu wanaoendesha chokochoko dhidi ya serikali yake.

Alisema Kayumba ambaye alivuliwa ubalozi hivi karibuni na sasa amekimbilia Afrika Kusini kuomba ukimbizi wa kisiasa, kuwa wamekuwa na mawasiliano na aliyekuwa mkuu wa mambo ya usalama Luteni Jenerali Patrick Kalegeya katika mipango yao ya kuhujumu Rwanda.

Majenerali hao wote walikuwa washirika wa Kagame lakini sasa wamekimbia nchi kutokana na kutofautiana na Rais huyo huku wakimtuhumu kwa kuendesha nchi kidikteta.

Alimtaja Kayumba kwamba alihusika na mashambulizi ya maroketi jijini Kigali hivi karibuni na kwamba ataiomba Afrika Kusini kumrejesha nyumbani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akijibu tuhuma dhidi yake, Jenerali Kayumba alisema kwamba Rwanda inazidi kuzama katika utawala wa kidikteta na kumtaja Rais Kagame kama mtu asiyetaka kukosolewa na yeyote.

Jenerali Kayumba ambaye amekwisha kupata hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa Afrika Kusini, alisema Rais huyu anataka watu wa kumlamba miguu kumzunguka lakini si watu wanaoweza kutoa mawazo yao.

“Madaraka yasiyokuwa na mipaka huporomoka vivyo hivyo, nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya mtu mmoja tu huku akipingana na wale wenye mawazo tofauti,” alisema Jenerali Kayumba.

Kadhalika, Jenerali Kayumba alikanusha vikali kuhusika na mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni na kusema yalipangwa na serikali ya Kagame mwenyewe kwa nia ya kuwapakazia watu asiowataka.

Rais Kagame alisema Mwendesha Mshitaka Mkuu wa Serikali, Martin Ngoga, hivi karibuni aliwataja Jenerali Kayumba na Jenerali Karegeya kuwa ndio waliopanga mashambulizi hayo.

Wakati Wanyarwanda wakilumbana kuhusu mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni, Nipashe iliwasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya Tanzania kutuhumiwa na Rwanda, lakini alisema yuko safarini Cairo, Misri.

Hata hivyo, alisema kwamba bado serikali hajaipata taarifa rasmi za malalamiko ya Rais Kagame ili iyatazame na kuyatolea tamko.

Hata hivyo, Membe alisema Tanzania wakati wote imesema wazi kwamba haifanyi wala kuunga mkono kitendo chochote cha kuhujumu nchi jirani katika ardhi yake.

Membe alisema Tanzania ilikwisha kutoa msimamo wake wakati taarifa za kuhujumiwa kwa Rwanda zilipotolewa na maofisa wa Umoja wa Mataifa na kuitaja serikali kusaidia waasi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa kusisitiza kwamba imejitolea kwa nguvu zake kuhakikisha kwamba amani inarejea katika ukanda wa Maziwa Makuu.

“Ni jambo lisiloingia akilini kusema kwamba Serikali ya Tanzania inaweza kupanga mkakati au kutoa msaada kwa kikundi chochote kinachokusudia kuvuruga amani katika ukanda huu,” alisema Membe ambaye aliahidi kutoa taarifa zaidi akishawasiliana na ofisi yake.


NIPASHE
 

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2007
Messages
16,498
Likes
182
Points
160

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2007
16,498 182 160
Sielewi kwanini ailaumu Tz ..Kwa hiyo alitegemea Tz imkamatie wapinzani wake na kuwasafirisha kwa ndege hadi Kigali? I bet hayuko serious.
 

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
56
Points
135

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 56 135
Here he comes again. Ajaribu kuitikisa Tanzania atakiona kilichomnyoa Khanga mayonya. Sasa hivi watu wanatafuta kitu cha ku-divert attention na yeye anataka kuwapa excuse.

Naona sasa ameanza kugopa kivuli chake, haiwezekani yeye tu asakamwe na DRC, Uganda, Tanzania na Kenya for what reason, au na yeye anajaribu kudivert attention kutokana na matatizo ya ndani?

Kama anakumbuka vizuri RPF wengi walikuwa wakimbizi na wengine tulikuwa tunasoma nao pale Shycom, kama kuna wahutu wanajaribu kuwarecruit wenzao, kama yeye alivyo arecruit watusi wenzie, atakuwa anakosea kutunyooshea vidole.
 

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
6,809
Likes
368
Points
180

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
6,809 368 180
What? Huyu jamaa kaanza kuishiwa; nilishawahi kuelezea udhaifu mkubwa wa huyu jamaa somewhere baada ya kutembelea nchi yake last yr; Ni Dikteta kamili; Katika mazungumzo ya kawaida tulifikia kuongelea chaguzi nami nikwaaambia kuwa kwetu tunajitayarisha na uchaguzi mkuu mwaka huu, walistaajabu! kwani wao hata hawajui hata kama kutakuwapo na uchaguzi , ni kama vile wanasubiri afe! Ilinitisha na kuona kuwa yale maendeleo wanayojivunia hayana maana kwa kuwa ikitokea jamaa ana colapse leo the system won't be ready unless kama kuna style like Uganda ambako Mu7 anamwandaa mwanawe!
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
44,157
Likes
28,842
Points
280

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
44,157 28,842 280
wanaipinga serikali yake kivipi? na kama anajua wanaompinga ndani ya serikali ya Tanzania awataje basi sio kuanza kutuchafulia na kutuletea mabalaa hapa..richmonduli na wenzake ni mizigo kwetu tayari.inatosha sasa hivi..now tunangojea viongozi vijana tulioahidiwa na MZEE VASCO katika kipindi chake cha pili hatutaki makashfa mengine
 

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
5,905
Likes
1,836
Points
280

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
5,905 1,836 280
Jamani haya mambo wakati mwingine ni magumu siyo rahisi rahisi...
Unaweza ukute kuna kikundi cha watu nadani ya serikali yetu kinalipwa kifisadi na watu fulani wenye maslahi yao kwa Kagame japo siyo rasmi, kwa Kagame yeye ataona ni Tanzania tu kwa ujumla. Msisahau kashfa ya Tz kuwapitishia silaha waasi wa DRC?
 

N-handsome

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,336
Likes
136
Points
160

N-handsome

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,336 136 160
wanaipinga serikali yake kivipi? na kama anajua wanaompinga ndani ya serikali ya Tanzania awataje basi sio kuanza kutuchafulia na kutuletea mabalaa hapa..richmonduli na wenzake ni mizigo kwetu tayari.inatosha sasa hivi..now tunangojea viongozi vijana tulioahidiwa na MZEE VASCO katika kipindi chake cha pili hatutaki makashfa mengine
Hivi kabakiza kwenda Vatican, Israel, Russia na washirika wake na labda Somalia
 

Cynic

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2009
Messages
5,154
Likes
641
Points
280

Cynic

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2009
5,154 641 280
Kagame kazoea kukorogana na nchi nyingine. Ufaransa wanambabahikia anafikiri na sisi tutampigia magoti.
 

Ben Saanane

Verified User
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,604
Likes
3,785
Points
280

Ben Saanane

Verified User
Joined Jan 18, 2007
14,604 3,785 280
I really hate this politivcal insanity.Mtu nasema watu wanaihujumu serikali yake,kwanza it's very possible huyu jamaa ameua raia wake kwa maroketi just to give him a way to clinch into power

Asituletee matatizo yake ya Ndania.Anatafuta sababu akituchokoza tu,we are going to unleash hell.Aulize waganda

Pia na sisis tanzania tuwe makini maanake sometimes hatuko nyuma kwa dirty games,coz hata akina kabila walikua bongo..waasi kama akina Prof.ernest Wamba Dia Wamba walikua wanafundisha UDSM

Pia tuache mianya ambayo inawapa madikteta excuse ya ku-divert politiacal and socia attention ya matatizo yao ya ndani

Also,we are jeorpadizing our diplomatic merit
 

Watanzania

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Messages
727
Likes
1
Points
0

Watanzania

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2009
727 1 0
I really hate this politivcal insanity.Mtu nasema watu wanaihujumu serikali yake,kwanza it's very possible huyu jamaa ameua raia wake kwa maroketi just to give him a way to clinch into power

Asituletee matatizo yake ya Ndania.Anatafuta sababu akituchokoza tu,we are going to unleash hell.Aulize waganda

Pia na sisis tanzania tuwe makini maanake sometimes hatuko nyuma kwa dirty games,coz hata akina kabila walikua bongo..waasi kama akina Prof.ernest Wamba Dia Wamba walikua wanafundisha UDSM

Pia tuache mianya ambayo inawapa madikteta excuse ya ku-divert politiacal and socia attention ya matatizo yao ya ndani

Also,we are jeorpadizing our diplomatic merit
Kwa nini unamwondoa Kagame kwenye kundi la waasi, kwa vile yeye sasa yupo madarakani?. Kagame ni muasi kama wengine, Kabila, Dia Wamba, Nkunda, ...., ....,.....
 

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Tukumbuke kuwa 85% ya watu wa Rwanda ni Wahutu!Kagame ni mtusi,na hawa wamedestabilise Congo,hata Uganda ya sasa(Mkumbuke na ye Mu7 anasili ya huko).
One man one vote,Kagame hawezi kushinda kihalali.

Hizi ni facts tuzijue!
 

Forum statistics

Threads 1,204,435
Members 457,321
Posts 28,158,249