Rais John Magufuli tutamlipa nini?

KHALFANI 86

Member
May 16, 2020
14
24
MH.RAISI JOHN MAGUFULI TUTAMLIPA NINI


Hili ni swali ambalo tunaweza kuyapata majibu yake ikiwa tutajituliza na kuipata tafakuli sahihi. Hakuna Mtanzania ambae hajaiona kazi ya Mh.Raisi toka mwaka 2015. Amejitoa kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania inabadilika katika kila eneo lake.

Haikuwa kazi ndogo ujenzi wa barabara zinavyojengwa kwa kasi kiasi hiki ,namna Mahospitali na Vituo vya afya vinavyoboreshwa na kujengwa maeneo mbalimbali nchini, jinsi uboreshaji na ununuzi wa vyombo vya usafiri kuanzia Anga, nchi kavu na majini,Tunazo ndege kubwa na za kisasa tunaweza kwenda nchi yoyote Duniani tunaipasua anga, Reli ndio hizo zinazidi kujengwa na za kisasa ,Meli na vivuko vipya tunaona vinaingizwa majini kwa kuondoa kero ya usafiri huo majini jicho letu ziwa Victoria muda sio mrefu tutaishuhudia MV Mwanza bora na ya kisasa zaidi ,na mashule mengi yamejengwa kipindi hiki kifupi cha miaka mitano.

KHALFANI najiuliza hivi mtu wa namna hii unaweza kumlipa malipo gani ambayo anaweza kufurahishwa nayo kwa aina hii ya utumishi aliotutumikia watanzani? Naendelea kuiangalia TANZANIA ya toka mwaka 2015 mpaka sasa 2020 tumepiga hatua kubwa sana. Wananchi wanafurahia maisha sasa,na kujivunia utanzania wetu. Nenda polisi kituo chochote unapokelewa utadhani umewapelekea zawadi unahudumiwa kwa usawa heshima ipo pande zote ,nenda ofisi yoyote ya Serikali hakuna tena kuzungushana nenda kesho au rudi keshokutwa ni unahudumiwa kulingana na aina ya shida yako, ofisi zote zimeonekana sasa kuwa Mwananchi ndo muajiri.

Ukiamua kuyaongelea mabadiliko ya miaka 5 hapa nchini tutakesha ndugu zangu. Ubungo pale yatakuwa maajabu ambayo hatukuyafikiria kuyaona TANZANIA ni barabara juu ya barabara aiseeee! Tazara sahivi raha sana pale Mfugale ,Mbona pale ukitoka zako Coco kuwahi posta nikupita juu ya Bahari yaaani raha juu ya raha. Kodi zetu zinaonekana nini zinafanya.

Tukiangalia namna ya kumlipa kwa haya aliyotupigania Raisi wetu ni mtihani kwani kaifanya kazi kubwa mno. Tanzania kuna uhuru wa kuabudu na Uhuru huo haupo kwenye nchi nyingi tunazijua,ni Tanzania pekee ukianzisha dini ukafata taratibu za nchi hauna kizuizi kikubwa zingatia tu taratibu za nchi,hata uamue usiabudu uwepo tu hakuna atakae kuhoji.

Wazo langu tuhakikishe tunampa zawadi ya ushindi wa kishindo yaaani tumpe kura mpaka mwenyewe ajishangae hii itakuwa ndio ahsante yetu kwake. Na ili kuufanikisha ushindi huo tuamue kuachia uhuru kwa wagombea wa nafasi zingine turuhusu wagombea wanaokubalika kwa wananchi ili wananchi waingie kwenye uchaguzi vifua vyao havina kwanini ndani mwake wafanye kuzisukuma kura za kutosha. Namaanisha ndani ya chama chetu CCM wale watu wa maamuzi waangalie sana wananchi wanamtaka nani hii itatusaidia kutuweka pamoja Katika hatua za kushambulia msako wa kuzitafuta kura zile za kishindo na awamu hii wapinzani wetu hawatokaa wasahau watakacho kiona kwenye ubao wa matokeo ya kura za jumla.

Tunafaham kuna watu wanaingia kwenye mchakato wakiwa na nia tofauti na mheshimiwa Raisi hao ndio tatizo ambao tunatakiwa kuwawahi mapemaaaa, kwani wakati tukiwaruhusu wajipenyeze tutatembea na kirusi cha kuzififisha juhudi za kuendelea kuijenga Tanzania mpya. Kuna watu hawapendeki lakini kwa kuwa wanahela wanaamini watafanya vyovyote wajipenyeze ili waende kufanya biashara zao kwenye siasa kitu ambacho ni kuidhohofisha kasi ya JPM .

Wananci wanahitaji wabunge wafuatao



Wabunge watakao ishauri vizuri serikali kuwapatia huduma stahiki kupata vituo vya afya na vyenye kuzitoa huduma bora,kuwapigania kuupata umeme ili waweze kujikita kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwenye maeneo yao, kuwajengea ushawishi wa kuwa na vyuo mbali mbali vya ufundi kwenye maeneo ili waweze kuwazalisha wataalam mbali mbali na kuchochea vijana kujiajili, kushirikiana na jamii kuondoa ujinga ,umaskini na maradhi. Wananchi wanahitaji maji barabara na huduma mbali mbali. Mbunge aguswe na maisha ya wana jimbo lake.


Wananchi hawataki wabunge wafuatao

Wabunge wa msimu wa uchaguzi baada ya hapo kukutana majaaliwa hawahitaji wabunge wenye mipango yao nje ya changamoto za kijimbo.Wabunge wa kuchagua hii kata siipendi napenda kata ile wabunge wa kugawa watu ,Wananchi hawahitaji wabunge wa kulitumia jimbo kujinufaisha wao binafsi.

Naomba nikishauri chama changu CCM, kwakuwa naamini wanayo mikakati mizuri siku zote ya kuwapata viongozi bora na makini ,basi wazingatie sana wananchi wanataka akina nani hii itatusaidia kufuta upinzani hapa nchini. Wale wanaojiaminisha kushinda ushindi wa kipesa na si ushindi wa kimapendo ya wapiga kura hao tuwa delete kabisaaaa.

Khalfani mwana wa ABUBAKARI mjukuu wa FADHILI namaliza kwa kusema ,ZAWAD ya ushindi wa kishindo kwa Mh.Raisi JOHN MAGUFULI itamuongeza nguvu katika kutupigania Wataanzania.


CHAGUA MAGUFULI 2020 KAZI IENDELEE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyezi Mungu atamlipa kwa niaba yetu, kwani sisi hatuna cha kumlipa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kila mtu ulipwa kwa matendo yake na Mungu utoa adhahu hapahapa duniani pale anapokosewa...

Rais Ana mshahara na pensheni akistaafu... Huko kutaka kumlipa ni kujipendekeza na isiwe sababu ya fadhira au hisani ya kutaka raia wamchague Tena....
 
Hivi mtu anapoapa kuwatumikia watanzania maana yake ni nini hasa? Utumishi kwa mtumishi wa umma sio hisani bali jukumu lake la msingi, ungejenga hoja kwamba mtumishi huyo namba moja ameonyesha kiuhalisia nini maana ya kuwatumikia watanzania, hivyo amefanikiwa kutulipa sisi kile tulichomwagiza kukifanya.
 
Usihusishe mawazo yako na ya kwangu.Ya kwako ni yako na ya kwangu ni yangu.Unataka apewe nini wakati ni wajibu wake,wewe hujui haki yako ya kutendewa,unatushauri sisi tununue haki yetu,tambua haki yako bro,acha ujinga.Hapashwi kupewa chochote nakushauri,bali anatakiwa kuwasikiliza Watanzania wanataka nini.Piga hatua fungua macho uone.
 
Huyu huyu ambae tunamlipa Mshahara na Marupu rupu kibao?

Huyu huyu ambaye alisema ataonesha slip yake ya mshahara ya Mil 9 halafu ametokomea mazima?

Huyu huyu ambaye ameshindwa hata kufuata utaratibu wa likizo kwa mtumishi (ameenda likizo zaidi ya siku 30)

Huyu huyu ambaye ameanza kutumia dini kama sehemu ya kupigia kampeni (Jana ameigiza kiaina kuwa, watu watumie siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato) na Jumapili(Wakristo wa madhehebu mengine) kama sehemu ya kumshukuru MUNGU).

Huy huyu ambaye deni la Taifa limeongezeka mara dufu na % kubwa ya miradi haijafika hata 80%? Na wakati huo huo tunaambiwa Serikali yake ndio imevunja rekodi tangu Uhuru kwa kukusanya Mapato.

Huyu huyu ambaye watu hawajapandishia mishahara na madaraja? Achana na habari za Ajira.

Huyu huyu ambaye Serikaki yake imeshindwa kulipa wakulima wa Korosho mpaka leo?

Huyu huyu ambaye amesimama hadharani na 'kumuagiza' spika Ndugai awashughulikie Wabunge wa Upinzani kule Bungeni na yeye ata-deal nao Uraini.

Huyu huyu ambaye wakati mwingine ametukana watumishi hadharani ambao ameteua mwenyewe kwa kuwaita Wapumbavu? Rejea Mkurugenzi wa Nachingwea.

AU unazungumzia kumlipa nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunahitaji majibu ya akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Maiti za coco beach, kubambikia kesi watu, kutesa watu . Tunahitaji uchunguzi huru wa hayo!
Kaka mkubwa I wish ungemuona huyo unayemuuliza haya maswali.. Huyu ni katika ile timu ya kuandikiwa mada kisha apost... Na sometimes ni mtu mmoja mwenye multiple IDs hivyo hana uwezo ama muda wa kujibu
Hizi zinaitwa post za kupima upepo

Jr
 
Tusimtukuze sana kiasi ajisahau,
Afanyapo vizuri tumsifie,
Afanyapo vibaya tumkosoe.

Kwako mleta mada;
Kwa nini umejitambulisha
kiasi hicho??
 
Back
Top Bottom