Rais Jakaya Kikwete awasili Afrika ya kusini kuaga mwili wa Mandela

Pasco, mbona unaandika kinafiki? Yaani kukaa siku nne kuomboleza msiba wa pacha wa baba wa taifa we unaona nongwa?

Baada ya mazishi atarudi Tanzania. After two weeks ataenda tena SA kuhani msiba kwa takriban siku 7. Baada ya hapo itakuwa tayari 2014 imefika si itamlazimu aanza kupita kwenye nchi zooooote alizotembelea akiwa Rais kuaga.
 
Hili ni jambo jema kwa rais wa nchi yetu, kama Mandela, alipokuwa wa kwanza kuja nchini kwetu vivyo hivyo rais wetu awe wa kwanza kuhudhuria ila pia nadhani ni mapema mno, kama mazishi ni Jumamosi, na leo ndio kwanza Jumanne, inamaana rais wetu amekwenda kuaga tuu na kutoa heshima za mwisho na sio kuzika?, au kutokana na ukubwa wa msiba, na ukaribu wetu na Madiba, then tunamlilia Kiafrika, kulala 3 nights, ya 4 kunawa maji?.
Rip Madiba.
Pasco

Hongera kwa sarcastic comment!
 
Rais wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete ameshawasili nchini Afrika ya Kusini kuhudhuria msiba wa Rais wa kwanza mweusi marehem Nelson Mandela.

Kwa safari hii itakuwa ni safari ya 370 na akiwa huko kwa average ya siku 3 akiwa nje ya nchi atakuwa amekaa nje ya Tanzania 370*3= 1,110.

Ni sawa na siku 1,110\365= Miaka 3 yuko nje ya nchi

"Minimum".....R.I.P Madiba
 
Kumbe mandela ni mkara?sikujua kama ni pacha wa nyerere..lajini mbona hakuja kumzika pacha wake
Nyerere ni Mzanaki sio Mkara!, Wakara ni kabila dogo wanaoishi kwenye visiwa vya Ukara vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria!. Wenyeji wa Ukara ni wavuvi. Kutokana umbali na udogo wa visiwa hivyo, havikuwa na shule yotote enzi za ukoloni, hivyo Wakara wengi wa enzi zile hawakubahatika kusoma na ndio waliokuwa wavuvi, makuli na wasukuma mikokoteni jijini Mwanza, kama vile Wagogo wanavyouza bucha, Wachagga wanavyo brush viatu, Wahaya na kale kabiashara!, Wasichana wa Iringa na kazi za u-tx etc!.

Wakara walisifika Mwanza kwa ushirikina!, ikidaiwa ukimdhulumu, anakutumia mamba!, lazima utakwenda ziwani, utajisikia kuogelea, mamba atakufuata na kukuzamisha, atakubebe chini kwa chini mpaka Ukara, huku ataibuka na kukuacha pwani ya ziwa na ndipo atakapojitokeza yule ulio mdhulumu na utakiona cha mtema kuni!.

Mwalimu Nyerere alitolea tuu mfano wa kabila hili pale Kilimanjaro Hoteli na nilikuwepo!.
Rip Madiba.
Pasco
 
Jamani wakaguliwe hawa viongozi wetu wanapopita viwanja vya ndege. Tena safari ya SA. Mwakyembe angalia hii kitu.
 
JK alihusika na lolote kuhusu ukombozi wa SA? Je ameondoka na wazee ambao angalau wana makovu ya SA? Je mama Maria Nyerere amefikiriwa?
 
akitoka hapo atapitia visiwa vya shelisheli kwa mapumziko.....nape jitu patel...
 
Dah, sikujua kuwa kuna mburulaz wengi humu JF wasiojua ulinganisho wa NM na JN

Nyerere alikua mtu wa visasi ndio mana hata alivyopewa nafasi ya kuongoza Tanganyika huru aliwanyanga'nya wakolon mali zao mwishowe uchumi wetu ukazidi kuporomoka.
 
Mkuu, bila shaka viroba vya kinondoni vimekuathiri sana kiasi cha kujitoa ufahamu. Pole sana mkuu

Aksante pole nawewe kwa sembe ilivyo kuathiri kwani hata upeo wako wakufikiri umeporomoka. Huwezi kumlinganisha Madiba na JKN kwani yeye aliwafukuza makaburu kwa kuzitaifisha mali zao wakati Madiba aliwafanya kua sehemu ya watu wake.
 
Kumbe mandela ni mkara?sikujua kama ni pacha wa nyerere..lajini mbona hakuja kumzika pacha wake
Mbona mandela alitoa taarifa kipindi kile akasema hawezi kuhudhuria mazishi kwa sababu ya hari yake ya afya ingebadilika kutokana na uchungu na ukaribu na nyerere. Lakini baada ya mazishi alikuja kutoa pole. Inaonekana kipindi hicho ulikuwa mdogo!
 
Sherehe za uhuru ndio zilikua zinamchelewesha vinginevyo angeenda siku ileile madiba alipo kufa.
 
huyu mzee asipojua kuendesha ndege atakuwa na kichwa kigumu sana aisee
 
Rais wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete ameshawasili nchini Afrika ya Kusini kuhudhuria msiba wa Rais wa kwanza mweusi marehem Nelson Mandela.

Kwa safari hii itakuwa ni safari ya 370 na akiwa huko kwa average ya siku 3 akiwa nje ya nchi atakuwa amekaa nje ya Tanzania 370*3= 1,110.

Ni sawa na siku 1,110\365= Miaka 3 yuko nje ya nchi

Huyu bwana mkubwa sijui mama yake alikuwa anakula sana miguu ya kuku! manake aaah
 
Back
Top Bottom