Rais Jakaya Kikwete atembelea mashamba ya mananasi Ghana

So sorry for hime....so shameful. Sijui Waziri husika Ana kazi gani kama hayo mananasi yana umuhimu.
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nafikiri kuwa rais wa nchi ndiyo mtu mwenye akili kuliko wengine wote. Lakini nilipofikia utu uzima nimegundua ni kinyume chake, nikitumia kielelezo kutoka Tanzania.
 
Kutokana na hizo picha,hilo shamba na kiwanda ni kama yaliyopo huku Tanzania! Ulimaji na upandaji wake ni sawa sawa na inavyofanyika kule Mkongoro na Bitale mkoani Kigoma. Ningewaona wa maana kama wangetumia matrekta/powertiller kupanda na kuvuna hayo mananasi. Vinginevyo, hamna kipya hapo!
 
1. Upande mmoja nashawishika kuamini kuwa tatizo si mh. Rais Kikwete wala maeneo anayotembelea wakati wa ziara zake nje ya nchi bali waandishi wa habari anaofuatana nao. Nashawishika kuwa hawa (waandishi) ama wanaufahamu mdogo kwa kazi yao au kwa makusudi wanaripoti visivyo ziara za Rais wetu. Sitaki kuamini kuwa katika ziara hii ya Ghana jambo la muhimu sana alilofanya JK ni kutembelea na kushangaa shamba la mananasi; au alipokwenda Brazil ilikuwa nyanya tu. Naona watoa taarifa huacha mambo ya msingi ambayo huhusisha ziara za Rais na kuripoti kushangaa kwake nyanya, muhogo (Jamaica), matikiti na sasa mananasi.

2. Upande mwingine wa akili yangu nashawishika kuamini kuwa huenda Rais au wanaoratibu ziara zake hawajui nini na wapi pa kumpeleka Rais. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Mh.JK tangu aingie madarakani mara kadhaa ameripotiwa kuonana na watu au makundi yasiyo na tija katika maendeleo ya Tz au kushangaa na vitu amabavyo hata hapa Tz vipo tena kwa kiwango kikubwa shida tu hakuna nguvu/ msukumo/ kuungwa mkono na serikali yetu. Na hili linatoa picha kuwa huenda tuna Rais asiyefahamu nchi yake na watu wake au anafahamu lakini anafanya kusudi.
Hebu tujiulize Mh.JK hasikii kilio cha watafiti wa kilimo katika vituo vya SUA, UYOLE, MPWAPWA, TENGERU, UKILIGURU nk juu ya kukosa fedha za kufanya utafiti? Na hata pale walipofanya utafiti na matokeo chanya kupatikana Serikali hii na zilizopita imepuuza kuzifanyia kazi na kutenga bajeti ya kuhakikisha maarifa na stadi hizi zinawafikia wakulima wadogo?

Nikiacha upande wa utafiti. Je, ni kweli mananasi yanaooza Chalinze, Geita, Muleba na kwingineko ni kutokana na kuwa wakulima wanalima aina isiyo na soko la kimataifa? Iko wapi jitihada ya JK na serikali yake kuwasaidia wakulima hawa wa matunda kutumia kikamilifu soko la ndani. Ni kweli JK hajui hata uzalishaji wa mananasi pale Miono jirani na kijiji chao?
Ni lini JK atazungumzia na kutenga fedha kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya usindikaji matunda hapa nchini?
Ni vema JK kabla ya kufikiri uzalishaji wa mbegu ya nanasi na matunda mengine yenye soko nje ya nchi aoneshe jitihada kuwezesha wakulima kunufaika na soko la ndani. Aoneshe jitihada kuhakikisha anawasaidia wakulima kupunguza hasara itokanayo na matunda kuozea shambani au pale Chalinze stand, Segera, Soni, nk.

Kinyume cha hapo ni bora Mh. Rais apumzike nchini kuliko kupoteza fedha zetu kwa kwenda kushangaa vitu vinavyopo hapa nchini tena kwa wingi! Naamini hata hao wenyeji wetu (huko anakotembelea) wanatuona mazuzu kushangaa vitu wanavyojua tunaweza sana kuzalisha


EJL
 
sisi huku kwetu (ambapo ni Afrika pia) huwa mtu akija msibani ni kuhudhuria matanga tu na hairuhusiwi hata kutumia huo muda wa msiba kusalimia hata majirani, maana ni wakati wa huzuni na wote mnakutana msibani!
Sasa mara umekuja msibani alafu kumaliza tu mazishi unaenda kwa 'Ta Muganyizi' kuangalia au kuomba mbegu nzuri ya migomba kwa hakika inatia shaka kama kilichokupeleka ni msiba au ulikuwa na lako jambo!!!


Ndio maana hamuendelei.
 
Kuna siku alisafiri katika moja ya nchi za kusini mwa Afrika, akatembelea 'ranchi' za ng'ombe akashangaa sana ukubwa wa ng'ombe wale aliowaona, akasema, namnukuu, 'sijawahi kuona ng'ombe wakubwa kiasi hiki' na akauliza jinsi wanavyowatunza. Kwa tukio zuri alikuwa na mmoja wa wataalaamu wa mifugo akamwambia mzee Iringa kuna ng'ombe wakubwa kuliko hawa. Mkuu akabaki anashangaa hana cha kusema kusikia nchini kwake kuna ng'ombe wakubwa kuliko wale.

Yaani mkuu anajua shughuli zinazofanywa na nchi za watu kuliko nchini mwake. Ningemsifu kama angekuwa anavaa viatu vya tope kama mwalimu na kutembelea mashamba ya nyanya ya Iringa, mashamba ya mpunga ya Ifakara, sio kwenda nchi za watu kutumia kodi nyingi bila tija yoyote.

JK uone aibu sasa, umeshatalii vya kutosha hebu miaka iliyobaki tulia nyumbani, sio utoke ikulu ukiwa hujatuachia hata vijisenti kidogo vya kuendesha nchi.
Mkuu mbona unazunguka sana?!!!! sema hiyo ziara ilitakiwa ifanywe na maofisa kilimo pale wizarani kilimo na chakula na wakitoka hapo waende kila wilaya ya Tanzania kupeleka elimu ya walichojifunza kwa wakulima wetu
 
Jaman mbona kama hamjui si mnajua watu wa Pwan, nikwl ziara kama hz hazina tija kwa watanzania walitakiwa waende wahusika wenyewe, Rais dhaifu rais dicteta kila tukio yupo hapo alipo wallah anataman awe na vyeo vyote mpaka ukuu wa wilaya.
 
Back
Top Bottom