Rais Dr. Shein amtoa nje ya Ukumbi Ndugu Shaka Mwenyekiti wa CCM Vijana Zanzibar

5523

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
1,699
1,592
Habari za mwaka mpya nataraji mupo salama buheri wa afya. Mtu wangu karibu zaidii amenijuza haya yaliyojiri katika Kikao cha kwanza CCM kisiwandui ambapo mwekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar Dr Shein. Kikao hichi ni kufutia vikao 2 ambavyo vimefanyika huko huko Zanzibar baada ya sherehe za Mapinduzi kuadhimishi miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo vikao hivi 2 Mwenyekiti wake alikuwa Rais Jakaya mrisho Kikwete.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtoa nje ya ukumbi ndugu Shaka Naibu UVCCM Zanzibar na Rais kuagiza awe chini ya ulinzi.

Hii ilitokana na kikao hicho Baada ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Rais Shein kuanza kutaja matarajio na tathmini ya chama chao 2015 kuelekea uchaguzi mkuu.

Dr Shein alisema "Napenda nipongeze juhudi zinazochukuliwa na chama chetu kwa viongozi wa chama chetu kukiimarisha chama hichi na kua imara zaidi kuliko changuzi za miaka iliyopita mara hii kukuwa kwa kasi zaidi na kuwa na matarajio makubwa ya ushindi mkubwa wa chama chetu.

Ambapo Dr Shein alisema matarajio ya chama Cha Mapinduzi kushinda katika uchaguzi ujao ni kuanzia 52% hadi 58% kwa Zanzibar hivyo ni faraja kubwa. Baada ya kusema hayo alisema kikao kimefunguliwa na mkutano uko wazi wajumbe kuchangia''.

Akaanza kusimama Dr Hussuen Mwenyi Waziri wa Afya na kumtaka Mh Rais pia afafanue mpasuko uliopo ambao unaonekana wazi kukiathiri chama cha Mapinzudi Zanzibar kuhusu Katiba mpya na kuhusu viongozi wa Jumuia ya Uamsho ambao wamefunguliwa mashtaka Tanzania Baraza jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kukiathiri chama chao kwa watu walio wengi kuchukizwa na jambo hilo kwa upande wa Zanzibar.

Baada ya hapo alisimama ndugu Shaka Naibu UVCCM Zanzibar na neno la kwanza alisema ''Mhe Rais chama chetu kimekufa. Akaendelea kusema ''Chama chetu kimekufa na aliyekiuwa chama hichi wewe.

Ndio aliposimama Mh Rais Dr Shein na kumwambia Shaka mbona wewe huna heshima maneno gani hayo unayosema kuniambia mimi. Unapaswa kuniheshimu na viongozi na marais wote wa Zanzibar mumekuwa mukiwa na heshima lakini mimi munakuwa munanivunjia heshima. Na ndio nyinyi mnaosema mimi sigombanii tena Urais wa Zanzibar na hali mimi mwenyewe sijatamka jambo hilo.

Viongozi wote waliopita wa Zanzibar haijawahi kutokezea mtu CCM kusema kiongozi huyo hagombanii tena baada kumaliza kipindi cha miaka 5 isipokuwa mimi tu.

Naomba mara moja utoke nje na nitakuchukulia hatua kwa kunivunjia heshima na nitakuweka ndani ndipo Shaka alipotolewa nje chini ya ulinzi.

Ndipo sasa Aliposimama Asha Bakari mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akaanza kumpongeza rasi kwa juhudi za chama zilipofikia na kupiga hatua zaidi katika kuleta Maendeleo, na pia kumtaka Rais aweze kumsamehe Shaka amchukulie kama mtoto amekosea na mtoto akikosea kiganja hakikatwi bali huoshwa na akachukua ahadi watamwita ndugu Shaka ili kumuonya mara ya pili asirudie tena. Baada ya mkasa huo Rais Shein alikharisha kikao hicho.

Kwenu wadau.
 
viongozi wetu hawapendi ukweli.angemsikilza bwana shaka kwanini anasema chama kimekufa na kwanini anamtuhumu cha kifia mikononi mwake. baada ya hapo angejibu hoja zake ikiwa ni pamoja na hoja za dr.mwinyi.kwakuwa ilikuwa ni kikao mimi sijaona kosa la shaka hapo.
 
Hqta mbingu zimeheshimu maneno ya shaka urudisalama angalia wasikupige namashinezqo kule.....
 
Shein alipaswa kumjibu au angemtaka mtoa hoja afafanue jinsi anavyoona kuwa yeye(rais)amekiua chama. Rais anaonekana ni mtu mwenye hasira na jazba asiye weza kuvumilia mawazo tofauti na yeye. Namuona kuwa na hali fulani ya kidikteta
 
Hakuitwa m-CHADEMA kama mimi niitwavyo humu JF? Kiukweli,chama kina hali ngumu.Hatutachoka kusema ukweli humu na kwingineko.

Mzee Tupatupa

Na hiyo ndo inayofanya wanachama wenu waone bora kuzungumza na vyombo vya habari kuliko vikaoni. Anyway nyumba ya adui yako ikiwa inateketea msaidie kumnunulia petrol ili kuuzima
 
Shaka anatia shaka kama jina lake lilivyo, alipaswa kumshangilia Shein, kumfurahia na kumchekea Mkubwa hakosei. Hahahahahaa CCM CCM hao
MANI pita huku fasta
 
Last edited by a moderator:
Habari za mwaka mpya nataraji mupo salama buheri wa afya. Mtu wangu karibu zaidii amenijuza haya yaliyojiri katika Kikao cha kwanza CCM kisiwandui ambapo mwekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar Dr Shein. Kikao hichi ni kufutia vikao 2 ambavyo vimefanyika huko huko Zanzibar baada ya sherehe za Mapinduzi kuadhimishi miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo vikao hivi 2 Mwenyekiti wake alikuwa Rais Jakaya mrisho Kikwete.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtoa nje ya ukumbi ndugu Shaka Mwenyekiti Vijana CCM Zanzibar na Rais kuagiza awe chini ya ulinzi.

Hii ilitokana na kikao hicho Baada ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Rais Shein kuanza kutaja matarajio na tathmini ya chama chao 2015 kuelekea uchaguzi mkuu.

Dr Shein alisema “Napenda nipongeze juhudi zinazochukuliwa na chama chetu kwa viongozi wa chama chetu kukiimarisha chama hichi na kua imara zaidi kuliko changuzi za miaka iliyopita mara hii kukuwa kwa kasi zaidi na kuwa na matarajio makubwa ya ushindi mkubwa wa chama chetu.

Ambapo Dr Shein alisema matarajio ya chama Cha Mapinduzi kushinda katika uchaguzi ujao ni kuanzia 52% hadi 58% kwa Zanzibar hivyo ni faraja kubwa. Baada ya kusema hayo alisema kikao kimefunguliwa na mkutano uko wazi wajumbe kuchangia’’.

Akaanza kusimama Dr Hussuen Mwenyi Waziri wa Afya na kumtaka Mh Rais pia afafanue mpasuko uliopo ambao unaonekana wazi kukiathiri chama cha Mapinzudi Zanzibar kuhusu Katiba mpya na kuhusu viongozi wa Jumuia ya Uamsho ambao wamefunguliwa mashtaka Tanzania Baraza jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kukiathiri chama chao kwa watu walio wengi kuchukizwa na jambo hilo kwa upande wa Zanzibar.

Baada ya hapo alisimama ndugu Shaka Mwenyekiti vijana wa CCM na neno la kwanza alisema ‘’Mhe Rais chama chetu kimekufa. Akaendelea kusema ‘’Chama chetu kimekufa na aliyekiuwa chama hichi wewe.

Ndio aliposimama Mh Rais Dr Shein na kumwambia Shaka mbona wewe huna heshima maneno gani hayo unayosema kuniambia mimi. Unapaswa kuniheshimu na viongozi na marais wote wa Zanzibar mumekuwa mukiwa na heshima lakini mimi munakuwa munanivunjia heshima. Na ndio nyinyi mnaosema mimi sigombanii tena Urais wa Zanzibar na hali mimi mwenyewe sijatamka jambo hilo.

Viongozi wote waliopita wa Zanzibar haijawahi kutokezea mtu CCM kusema kiongozi huyo hagombanii tena baada kumaliza kipindi cha miaka 5 isipokuwa mimi tu.

Naomba mara moja utoke nje na nitakuchukulia hatua kwa kunivunjia heshima na nitakuweka ndani ndipo Shaka alipotolewa nje chini ya ulinzi.

Ndipo sasa Aliposimama Asha Bakari mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akaanza kumpongeza rasi kwa juhudi za chama zilipofikia na kupiga hatua zaidi katika kuleta Maendeleo, na pia kumtaka Rais aweze kumsamehe Shaka amchukulie kama mtoto amekosea na mtoto akikosea kiganja hakikatwi bali huoshwa na akachukua ahadi watamwita ndugu Shaka ili kumuonya mara ya pili asirudie tena.

Kwenu wadau.

Habari hii ina dalili ya kutokua na ukweli ila sina maana ya kusema mwandishi ni muongo .inawezekana mtu wake wa karibu amempotosha . Bi asha bakari ni mgonjwa sio muda amerudi india na alifanyiwa upereshen/upasuaji wa moyo na hii ilitokana na kule kuanguka kwake katika bunge maalum la katiba .aliamuua kwenda kuangalia afya yake alipoona afya yake haijaimarika vizuri hapa nchini .kufika kule akaonekana na tatizo katika moyo wake na ndipo aliambiwa analazimika afanyiwe upasuaji. Pia aliambiwa ajipumzishe kwa kipind kikubwa kuepusha matatizo alirudi nchini.kimya kimya yupo anajiuguza kwa kweli ni mgonjwa wa kuangaliwa .
Sasa hapa ndipo muandishi anapoleta utata kidogo kuleta wasi wasi na mada .
Kuhusu chama kufa halitaki taa chama kimekufa sana kinana juzi alihutubia watu kidogo sana katika ngome ya ccm jang'ombe mpaka alishikwa na aibu.
 
message imetumwa, imefika na kaisoma. Halafu huyu eti ssem wamataka kutukeletea bara agombee urais!!! Lisu atakuwa anaimba jukwaani
 
Na hiyo ndo inayofanya wanachama wenu waone bora kuzungumza na vyombo vya habari kuliko vikaoni. Anyway nyumba ya adui yako ikiwa inateketea msaidie kumnunulia petrol ili kuuzima

Ninaamini vyama vingine hiyo ndio nafasi sahihi kuwasaidia kuzima huo moto kwa petrol. CCM ina hali mbaya mpaka kiongozi wa kitaifa anakili kuwa uwezekano wa kushinda ni 52%!!!!! unajua kuwa hiyo ni marginal winning. What if upepo unabadilika kura zikapungua? CCM Zanzibar wajiandae kisaikolojia kuwa chama cha upinzani.
 
Habari hii ina dalili ya kutokua na ukweli ila sina maana ya kusema mwandishi ni muongo .inawezekana mtu wake wa karibu amempotosha . Bi asha bakari ni mgonjwa sio muda amerudi india na alifanyiwa upereshen/upasuaji wa moyo na hii ilitokana na kule kuanguka kwake katika bunge maalum la katiba .aliamuua kwenda kuangalia afya yake alipoona afya yake haijaimarika vizuri hapa nchini .kufika kule akaonekana na tatizo katika moyo wake na ndipo aliambiwa analazimika afanyiwe upasuaji. Pia aliambiwa ajipumzishe kwa kipind kikubwa kuepusha matatizo alirudi nchini.kimya kimya yupo anajiuguza kwa kweli ni mgonjwa wa kuangaliwa .
Sasa hapa ndipo muandishi anapoleta utata kidogo kuleta wasi wasi na mada .
Kuhusu chama kufa halitaki taa chama kimekufa sana kinana juzi alihutubia watu kidogo sana katika ngome ya ccm jang'ombe mpaka alishikwa na aibu.

Mkuu umechangia kwa ustaarabu wa Hali ya juu.......utaniwia radhi kama nitakukosea maana sijui upo upande gani lkn Kiukweli mwenye uchangiaji wa kistaarabu hvi Ni Mh.Mbowe.......salute Kwako brother,umenikumbusha Kamanda Mbowe akiwa mjengoni.
 
Hii habari ni sahihi kabisa ccm huwa wanamsema Rais Shein sana kwamba amepojea sana kukiendesha chama cha Mapinduzi, hachangamshi chama na wanasema ni mzito wa maamuzi siku moja nilimsikia Kada 1 wa ccm akisema sisi binafsi tumemuandikia barua amfukuze mkuu wa Mkoa wa ................. lakini hakufanya hivyo.

CCM imekufa Zanzibar, namtabiria maalim seif 95% ya ushndi 2015 inshaalah.
 
Back
Top Bottom