benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Serikali mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na timu ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campain, wamefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 14 kati ya Fatuma Maganga na Said Mkama ambao ni wakazi wa Mtaa wa Ibinzamata.
Fatuma ambaye ni miane amefanikiwa kurejeshewa eneo lake ambalo lilivamiwa na Saidi ambapo Wakili George Moleli alisema baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mjane huo, walifuatilia na kubaini uwepo kwa hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa va Ardhi ilivoiagiza Manispaa ya Shinyanga kumkabidhi Fatuma eneo lake.
Alisema walilazimika kukazia hukumu hiyo ambapo Mkama alikubali kurejesha ardhi aliyokuwa anaimiliki kinvume cha sheria.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Christina Mdeme, alisema kampeni hivo imeleta matokeo chanya mkoani hapa kwa kuhakikisha wananchi waliodhulumiwa stahiki zao za ardhi wanazipata kwa wakati.
"Mkoa wa Shinyanga una migogoro ya ardhi inayochangiwa na baadhi va watendaji wasiokuwa waadilifu, Fatuma ameshinda kesi katika Mahakama ya Ardhi tangu mwaka 2017 lakini kumkabidhi eneo lake ilishindikana," alieleza.
Aliongeza kuwa watahakikisha kampeni hiyo inagusa kila eneo ili kuleta suluhu katika maeneo yenye migogoro va muda mrefu ambayo inachangia kurudisha nyuma shughuli za maendeleo, hivyo aliwataka wananchi kujitokeza kupata huduma a msaada wa kisheria inayotolewa bure.
Naye Fatuma alimshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni hiyo kwa kumpatia haki yake ambayo ilikuwa imeporwa tangu mwaka 2017.
"Mimi ni mjane sina fedha ya kuwalipa mawakili wanisaidie nipate haki yang ila Rais Dk. Samia ametuma watu Shinyanga ambao wamenifuta machozi kwa kunirudishia eneo langu nililoachiwa na mume wangu niweze kuwatunza wanangu," alisema.
Awali, Mkama alikiri kutolinunua eneo hilo kutoka kwa Fatuma lakini alilinunua kutoka kwa maofisa ardhi ambao walimchorea ramani kinyume cha sheria za mipango miji.
"Mgogoro huu ulitengenezwa na maofisa ardhi wasiokuwa waadilifu wakati nanunua eneo hili waliniambia lina viwania viwili kumbe kwenye ramani ya zamani ilionesha kiwanja ni kimoja, baada ya kulipa fedha na kutaka kuliendeleza mgogoro ndipo ulioanza," alisema Mkama.