The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 15,394
- 12,978
`Rais awezeshwe kuteua mawaziri wasio wabunge`
2008-05-02 08:59:18
Na Joseph Mwendapole
Serikali imeshauriwa kufanya mabadiliko ya Katiba ili kumpa fursa Rais kuchagua mawaziri wasio wabunge tofauti na sasa ambapo waziri lazima awe mbunge.
Ushauri huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika la Msaada wa Sheria na Uchumi kwa Walemavu (DOLASED), Bw. Gideon Mandesi, wakati wa mahojiano na Nipashe kuhusu ufisadi nchini.
Bw. Mandesi alisema wako watu wasio wabunge ambao ni safi na wana uwezo wa kumsaidia rais katika masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Alisema mabadiliko hayo yatampa fursa Rais kuwa na wigo mpana wa kuchagua watu wa kumsaidia katika majukumu mbalimbali.
``Si lazima waziri awe mbunge, kuna watu wachapakazi, waadilifu ambao wanaweza kusaidia kuleta mabadiliko lakini si wabunge,`` alisema na kuongeza kwamba itasaidia pia kuwafanya wabunge wengi wabaki kuwa wawikilishi wa wananchi.
Alimshauri Rais Jakaya Kikwete kuangalia mara kwa mara safu yake ya uongozi na kuwaondoa bila aibu wale ambao anaona hawamsaidii katika utekelezaji wa majukumu yake.
Alisema Rais anapaswa kuwachunguza hata mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje na endapo atabaini kuwa baadhi yao si wasafi awaondoe.
``Tunataka serikali iliyojaa watu waadilifu na wanaoweka mbele maslahi ya Taifa badala ya kujinufaisha wenyewe,`` alisema na kuongeza kwamba taasisi za serikali zinapaswa kumsaidia Rais kupata safu nzuri ya viongozi waadilifu wasio na harufu ya ufisadi.
Alimshauri Rais Kikwete kuendelea kufanya kazi na waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiibua masuala mbalimbali kuhusu wizi na ubadhirifu serikalini.
Alionya kuwa tuhuma za ufisadi zisipochukulia hatua pale zinapoibuliwa, wahisani wanaweza kupoteza imani na Tanzania hivyo kuifutia misaada.
SOURCE: Nipashe