`Rais awezeshwe kuteua mawaziri wasio wabunge`

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,394
12,978
`Rais awezeshwe kuteua mawaziri wasio wabunge`

2008-05-02 08:59:18
Na Joseph Mwendapole


Serikali imeshauriwa kufanya mabadiliko ya Katiba ili kumpa fursa Rais kuchagua mawaziri wasio wabunge tofauti na sasa ambapo waziri lazima awe mbunge.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika la Msaada wa Sheria na Uchumi kwa Walemavu (DOLASED), Bw. Gideon Mandesi, wakati wa mahojiano na Nipashe kuhusu ufisadi nchini.

Bw. Mandesi alisema wako watu wasio wabunge ambao ni safi na wana uwezo wa kumsaidia rais katika masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Alisema mabadiliko hayo yatampa fursa Rais kuwa na wigo mpana wa kuchagua watu wa kumsaidia katika majukumu mbalimbali.

``Si lazima waziri awe mbunge, kuna watu wachapakazi, waadilifu ambao wanaweza kusaidia kuleta mabadiliko lakini si wabunge,`` alisema na kuongeza kwamba itasaidia pia kuwafanya wabunge wengi wabaki kuwa wawikilishi wa wananchi.

Alimshauri Rais Jakaya Kikwete kuangalia mara kwa mara safu yake ya uongozi na kuwaondoa bila aibu wale ambao anaona hawamsaidii katika utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema Rais anapaswa kuwachunguza hata mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje na endapo atabaini kuwa baadhi yao si wasafi awaondoe.

``Tunataka serikali iliyojaa watu waadilifu na wanaoweka mbele maslahi ya Taifa badala ya kujinufaisha wenyewe,`` alisema na kuongeza kwamba taasisi za serikali zinapaswa kumsaidia Rais kupata safu nzuri ya viongozi waadilifu wasio na harufu ya ufisadi.

Alimshauri Rais Kikwete kuendelea kufanya kazi na waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiibua masuala mbalimbali kuhusu wizi na ubadhirifu serikalini.

Alionya kuwa tuhuma za ufisadi zisipochukulia hatua pale zinapoibuliwa, wahisani wanaweza kupoteza imani na Tanzania hivyo kuifutia misaada.

SOURCE: Nipashe
 
Hili tulisha lisema siku za nyuma sana hapa JF .Wabunge na hasa wa CCM sijui kama watakuwa wako tayari maana wao wana control ya kila kitu ndani ya Chama chao kwa faida ya Chama chao na si Nchi .Msuguano huu .Lakini tumesha kisema hili siku nyingi sana .
 
Hili tulisha lisema siku za nyuma sana hapa JF .Wabunge na hasa wa CCM sijui kama watakuwa wako tayari maana wao wana control ya kila kitu ndani ya Chama chao kwa faida ya Chama chao na si Nchi .Msuguano huu .Lakini tumesha kisema hili siku nyingi sana .

Katika hali kama hii ya ufisadi wa karibia kila mtu aliyegombea ubunge, ni wakati muafaka kabisa kuwa na mawaziri nje ya wabunge... pia itapunguza watu kutumia uwaziri (rasilimali za umma) kufanya kampeni majimboni mwao kwa kisingizio cha ziara ya kiserikali! Na pia kujipendelea (kwa kupeleka miradi ya maendeleo majimboni mwao) ili mtu azidi kuchaguliwa!
 
Katiba iliyopo imekuwa kikwazo kikubwa kwa mambo mengi maana imempa Rais Madaraka mengi ya kuteua.Inawezekana ikawa sababu ya makundi ya watu fulani kuendesha kampeni ktk chaguzi mbalimbali maana wakiwini watateuana.
 
Mpaka hapo sirikali na CCM watakapokubali mtazamo wa Watanzania walio wengi kwamba tunahitaji katiba mpya badala ya hii katiba bomu tuliyokuwa nayo sasa, hili litaendelea kuwepo kwa manufaa ya chama twawala.
 
..Kikatiba Raisi ana mamlaka ya kuteua wabunge 10 anaowataka yeye.

..suala la kujiuliza ni kwanini Raisi hatumii upenyo huo kuteua watu waadilifu na wenye uwezo ktk nafasi za uwaziri?

..so far kwenye hizo nafasi 10 Raisi amewateua Tom Mwangonda, Mustafa Mkullo, Yussuf Makamba, na Mzee Ngombale Mwiru.

..nikiangalia hayo majina nadhani Raisi wetu amekosa umakini. naamini kabisa he could have done a better job. huenda Raisi wetu "alishauriwa vibaya."

..Lakini siyo wabunge na mawaziri tu, Raisi ana mamlaka ya kuteua majaji, makatibu wakuu,makamishna,mabalozi,washauri etc toka sekta yoyote ile Tanzania na nje ya nchi. mfano mdogo ni Dr.Benno Ndulu aliyeteuliwa toka World Bank.
 
Sasa Kikwete ameishiwa wabunge wazuri wa kuwa mawaziri. Hawa wabunge wengi wana skendo sasa je ni nani atakuwa waziri??. Imefikia wakati medical doctor anakuwa waziri wa ulinzi wakati hajui hata kambi ziko wapi!. Kuna wasomi wengi na safi lakini hawajulikani vijijini na ni vigumu kuwa wabunge, sheria inalazimisha watendaji wa serikali kuwa wanasiasa. Vilevile mimi naona tungebakia na makatibu tu kama hapa marekani kwani ni raisi kuwachukulia watu hatua kama wapo kwenye msingi mmoja wa serikali badala ya serikali na bunge. Kama wewe ni mzalendo na umezaliwa mijini hata kama una elimu nafasi ni chache sana za kuwa mbunge sehemu za mijini na vijijini hujulikani kwani ulikuwa unaenda kusalimia babu na bibi tu. Hivyo raisi anabakia na wabunge walewale miaka nenda rudi kuwa mawaziri maana hakuna sehemu nyingine ya kuchagua. Kama wabunge wote wakiwa wanasheria basi mawaziri wote watakuwa wanasheria hata waziri ya afya!.Hivyo sababu mojawapo ya ufisadi ni mfumo wa kizamani.
Kuna wabunge wazuri ambao hawana uwezo wa kuongoza hivyo hii sheria imepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom