Rais ataka wenye vitambulisho wasitozwe ushuru wala tozo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,521
9,325
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameonya kuwa hatamvumilia kiongozi yeyote wa Mkoa, Wilaya ama Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa na Jiji atakayebainika kuhusika kuwatoza ushuru ama tozo yoyote wajasiriamali wadogo waliopatiwa vitambulisho.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi katika Mtaa wa Lumumba Jijini DSM, muda mfupi baada ya kutoka katika Ofisi Ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikoongoza kikao cha viongozi wenzake wa CCM.

Rais Magufuli amefafanua kuwa kiongozi yeyote atakayebainika kuwatoza wajasiriamali wadogo wenye vitambulisho atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuvuliwa madaraka, na hivyo ametaka wajasiliamali hao wasibughudhiwe.

Katika tukio hilo Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambao ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally Kakurwa, wamempokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ambaye ametangaza kurudi CCM ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu tangu alipotangaza kujiunga na chama cha upinzani.

Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani, umoja, udugu na mshikamano na kujielekeza katika ajenda kuu ya ujenzi wa Taifa, badala ya kupoteza muda mwingi kwa marumbano yasiyo na tija.
 
Ngoja tuone kitakachotokea baada ya hilo tamko iwapo hao wajasiriamali hawatanyanyaswa tena! maana wasaidizi wengi wa awamu hii wa mkulu wana masikio marefu mno! kama yale ya twiga au punda.
 
Kuna uzi ulionekana jana hapa ukisema halimashauri moja nchini imesema wajasiliamali wadogo wanaofanya biashara kwenye masoko watatozwa ushuru
 
Hilo ni tatizo kubwa sana halmashauri zinakosa kabisaa mapato hata posho za madiwani zinakuwa ni shida.na ivo vitambulisho unakuta mtu anauza ng'ombe 50 had 100 alafu ameshika kitambulisho.yan ugawaji wa ivi vitambulisho ni shidaaaa na ivi havina jina la muhusika yan wanapeana kama pipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom