Rais asiwe anawatambulisha wasaidizi wake madereva na walinzi mbele ya wananchi mikutano ya hadhara

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,907
Nimemwona Rais akiwa Kongwa akitambulisha dereva na mlinzi mbele za wananchi. Si sahihi na pia kumwita mlinzi wake kuacha lindo mgongoni na kwenda kuchangia.

Si sahihi huyo mlinzi kuacha guard post nyuma yake kwenda kufanya majukumu mengine.

Hata pale ikulu Raisi alipokutana na wafanyabiashara alimtoa mgongoni yule mlinzi wake iakamwambia akachukue namba ya mfanyabiashara yule wa mbeya na akamwamuru yule mlinzi ampe namba Yake mlinzi.

Mlinzi niliona anasita Lakini afanyaje akaitoa ile namva yake kwa mfanyabiashara

Anachofanya Raisi kwenye Hilo nadhani Sio sahihi.Hawa watu wanawekwa mazingira magumu ya kazi.Mabosi wao nwelezeni mheshimiwa .
 
Yule ni mpambe wa Rais yupo kumsaidia majukumu madogo madogo kama hayo wenye ulinzi wao wapo kwa kazi hiyo

Wakati jina LA waziri mkuu linapelekwa bungeni na Yule mpambe likapigiwe kura nani huwa anamlinda Rais huko alikobaki
Walinzi wako wengi alipopeleka jina bungeni walikuwepo wengine .Wasaidizi wa Raisi wako wengi aweza mtuma yeyote Kama Kuna umbali Sio kumtoa huyo wa mgongoni .Mbona wako kibao tu na wanafahamiana akitaka kitu kwenye mkutano aweza chomoka yeyote akaenda. Akamkabidhi bosi wake bosi wake akamkabidhi msaidizi wake huyo wa mgongoni bila ya Huyo kutoka
 
Unawafundisha kazi kitengo?
 
Waswasi wako ni nini?,lililopangwa na mungu mwanadamu hawezi kuliziwia,endelea na majukumu yako ya kujitafutia riziki,ya ngoswe muachie ngoswe
 
JamaaAmechanganyikiwa....
 
Yule ni msaidizi binafsi wa Rais sio Mlinzi
Ni ishara ya mamlaka ya Dola sio body guard



Ishara ya kumtambua ni vazi ( uniform)

Ishara ya Uamiri Jeshi

U Rais huwa una kaimiwa lakin uamiri jeshi haukaimiwi

Hata Rais akisimisha madaraka yake kwa mtu mwingine kwa sababu fulan mtu huyo hawezi kuwa na msaidizi wa aina ile kwa kuwa Yule mtu hawezi kuwa kaimu Amiri jeshi

Umewahi kuona Rais mstaafu, PM au makamu wa Rais nyuma yake kuna Uniformed Officer?
 
hakuna matata.
 

Sina hakika na ulichoona...kama unamananisha askari yule ambaye huwa nyuma ya Rais, yule siyo mlinzi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…