Rais anapochangiwa hela ya kuchukulia fomu

Rais anapochangiwa hela ya kuchukulia fomu

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
210
Jamani wanaJF nawaombeni mnisaidie kidogo mawazo yenu. Hivi rais aliye madarakani, na ambaye mshahara wake pamoja na marupurupu ni makubwa, ambaye hatumii hata senti moja kununulia ama sukari, unga, mchele, mafuta yawe ya gari au ya kula..nk, anapochangiwa hela za kuchukulia fomu za kuomba kazi ya urais, tena na wanafunzi ambao mara nyingi wamekuwa wakigoma kuingia madarasani kushinikiza wapatiwe mkopo na serikali anayoiongoza huyo rais, je, ni kujikomba, au nikumuonea huruma huyu rais masikini??
Ni mawazo tu yamenisumbua hadi kuwaulizeni wanajamvi wenzangu. Tujadili kidogo!!.
 
Jibu ni rahisi tu, kila mtu anaangalia maslahi binafsi. Ndipo tulipofikia waTz. Ile enzi ya kutanguliza maslahi ya taifa mbele imeshapita. Cha kusikitisha ni kizazi cha kesho tutawarithisha nini ikiwa kila nafasi ya kujiletea maendeleo tunawapa watu wa hovyo ili wawe viongozi wetu?
 
Kwani hiyo hela wamechanga hao wanafunzi?si inarudi ilikotoka,hizo ni propaganda ndugu we huijui CCm nini
 
Ni unyonyaji mtupu........hawa watu hawapati mikopo stahili na kwa wakati....leo unawachangisha halafu amewapa ahadi ambayo kamwe haitotimia...
 
Kwani wale wanafunzi wamechanga au pesa zimepitia kwao ili kumfikia JK? Na zile fulana mpya za njano na kijani wamenunua au wamepewa bure wazivae?

06_10_stknqh.jpg
 
Kuna haja ya kufuatilia uhalali wa hao wanafunzi, isijekuwa ni kama wazee wa DAR ES SALAM.
 
Tafuteni criticiques zilizo relevant, si mnaharibu kazi takatifu ya kum criticize Kikwete.

Kama wanafunzi wameamua kutoa statement kwamba wanampenda Kikwete na wanataka kuonyesha msimamo wao huo symbolically kwa kumnunulia forms je?

Mimi nafikiri watu wa kubanwa vizuri ni hao wanafunzi wanao m sponsor huyu msanii Kikwete. Na kubanwa huku si kwa matumizi ya pesa, maana kila mtu ana uhuru wa kutumia pesa zake atakavyo, bali kwa sababu ya ku sponsor economic and political retardation by way of Kikwete.And this can be debated kwa sababu kuna watu either wanaona Kikwete poa, au wanajua Kikwete bogus ila wanajipendekeza, if you cannot beat them join them style.

Kikwete hela zetu za madafu anaweza hata kuamuru gavana amchapishie noti mpya zenye sura yake by the ton, halafu azipeleke nyumbani kwake/ amuwekee katika akaunti yake.
 
Si tu ni kujipendekeza kwao wale wanafunzi bali pia na uwezo wao mdogo wa ku analyse mambo vikichangiwa na ubinafsi! wale wanafunzi walichanga wenyewe hawakuchangishwa na hiyo ni dalili wazi kuwa Taifa lijalo la Tz litakuwa ni la watu wabinafsi na wanaojali maslahi yao na vigeugeu pia, ni juzi tu hapa wanfunzi hawahawa waligoma eti mikopo haitoshi lakini leo ni wanfunzi hawahawa wanaandamana wakiimba eti wana imani na JK, na ajabu zaidi ili kuodhihirisha ubanafsi na unafiki wao wakaomba wawekwe kwenye timu ya kampeni na Muungana bila hiana akaamuru vijana 36 wajumuishwe kwenye timu yake ya kampeni hasa katika udhamini ule wa watu mia 200, so kwa Dodoma JK sasa anahitaji watu 164 tu ili kukamilisha idaidi ya watu 200 inayotakiwa japo kupata zaidi si dhambi!

Unafiki! unafiki! unafiki tu ndio umewajaaa hawa vijana na njaa yao ndio kaburi lao la maendeleo!
 
ni utaratibu tu ndg yangu wala usihofu. Kumbuka madaraka anayogombea ni ya umma hivyo ni lazima kuwepo uwazi ili isije raise maswali ya namna atakavyorudisha fedha za kuchukulia fomu pamoja na zile za kampeni (baba wa taifa)
 
ni utaratibu tu ndg yangu wala usihofu. Kumbuka madaraka anayogombea ni ya umma hivyo ni lazima kuwepo uwazi ili isije raise maswali ya namna atakavyorudisha fedha za kuchukulia fomu pamoja na zile za kampeni (baba wa taifa)

Utaratibu gani ndugu yangu wa masikini kumchangia tajiri!
 
full kujikomba na fikra finyu..................*** them all those student who contributed
 
Jibu ni rahisi tu, kila mtu anaangalia maslahi binafsi. Ndipo tulipofikia waTz. Ile enzi ya kutanguliza maslahi ya taifa mbele imeshapita. Cha kusikitisha ni kizazi cha kesho tutawarithisha nini ikiwa kila nafasi ya kujiletea maendeleo tunawapa watu wa hovyo ili wawe viongozi wetu?
Ya kale ni dhahabu.....
 
Back
Top Bottom