Miaka 4 ya Kwanza: Rais Magufuli - Kipimo Mara Mbili cha Ujasiri na Uthubutu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,999
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni dikteta uchwara? Labda! Ni bosi mkali mwenye ukarimu? Inawezekana! Ni kiongozi Mwafrika kwenye utofauti fulani hivi? Bila ya shaka! Kiongozi ambaye Watanzania kwa muda mrefu walikuwa wanamtamania na hatimaye kumpata? Ndiyo! Tangu kuchaguliwa kwake miaka minne iliyopita Rais Magufuli amekuwa ni Rais ambaye anagusa Watanzania kwa namna mbalimbali tena zinazopingana sana. Kwa wengine unapotaja jina lake tu wanajisikia kujikunyata na kubeza, huku wengine wakimsifia. Kwa wengine ukilitaja jina lake wanajisikia fahari na hisia ya uzalendo ambayo haijaonekana ncihni labda tangu Baba wa Taifa alipokuwa akizunguka nchini wakati wa harakati za uhuru miaka ya 1950.

Ingawa yapo mambo mengi ambayo hayalingani kati ya viongozi hawa wawili, ni rahisi kuweza kuona usambamba fulani baina yao. Hili linawezekana kuonekana angalau kwa mambo mawili – Nyerere na Magufuli wanaonesha kwa kiasi kikubwa imani yao isiyofichika juu ya uwezo wa Watanzania kujiletea maendeleo yao wenyewe. Na pili, wote wawili – Nyerere na Magufuli – wanachukulia hasa katika miaka yao ya mwanzo ya uongozi wao kuwa siasa inaweza kuwa ni kizuizi cha maendeleo.

Hata hivyo, mwelekeo wa Nyerere kuhusu mambo hayo unaweza kuelezewa kwa kuangalia masuala ya kihistoria ya zama zake au katika kusoma falsafa yake ya kisiasa – Magufuli ni vigumu kumuelewa kwani misimamo yake ya kisiasa haijaelezwa na kufafanuliwa kwa uwazi kama Nyerere. Kutokana na hilo ni vigumu kama siyo sawa kuwalinganisha viongozi hawa wawili na kufikia hitimisho sahihi. Kupita kwa zaidi ya nusu karne tangu wote wawili washike madaraka ya Urais wa Tanzania kunafanya ulinganishaji wowote wa hawa wawili kuwa mgumu kama usiowezekana kabisa. Hii haina maana kazi za kisomi au uchambuzi wa kihistoria kuhusu viongozi wawili usifanyike au usiwezekane kufanyika na kuweza kupambanua mfanano au utofauti wao.

Kama mtu ambaye nilimuunga mkono wazi Rais Magufuli 2015 naamini ninawajibika kwa kiasi fulani kutoa mawazo yangu juu ya miaka hii minne ya kuuangalia utawala wa Rais Magufuli. Uamuzi wangu ulikuwa ni uamuzi mgumu wakati ule na inawezekana bado hauna maarufu hadi hii leo. Nimepoteza marafiki wengi – au niliwadhania kuwa ni marafiki – kwa sababu ya kumuunga mkono Magufuli. Baadhi ya watu ambao tulianza nao kumuunga mkono Magufuli wakati ule sasa hivi wamegeuka na wanajutia uamuzi wao. Nikiwa mwanademokrasia wa kweli sishangazwi wala sijaumizwa na watu ambao wamegeuka sasa kwani tofauti ya misimamo, maoni, mitazamo nk. ndio msingi wa demokrasia ya kweli na natetea haki ya wanaonipinga kunipinga kwa nguvu zote.

Hata hivyo nimebakia na marafiki wengine wengi ambao hatuna misimamo ile ile; hawakumuunga mkono na mimi sikumuunga mkono mgombea wao. Hili limenipa nafasi ya kipekee kuweza kuelewa hoja mbalimbali za marafiki zangu kuhusu utawala wa Magufuli na kunifanya mara kwa mara nipime maamuzi na misimamo yangu vile vile ya kumuunga mkono Magufuli. Je, nilikosoea kumuunga mkono Magufuli? Je, ningeendelea kuunga mkono Upinzani baada ya ule Usaliti Mkuu wa Upinzani wa 2015? Hivyo basi unaofuata ni sehemu tu ya utetezi wangu juu ya Magufuli; kwa uwazi na kwa makusudi kabisa.

Miaka minne baadaye nimeona nilichoona, nimesikia nilichosikia na nimefikia hitimisho lisilo na utata kuwa Rais Magufuli ni kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamtamania, kuombea na hatimaye kumpata. Ni mtu wa vitendo, akija na kipimo mara mbili cha ujasiri na uthubutu. Ulimi wake unaweza usiwe mzuri sana kiama wengine na mtindo wake usifanane na wa wengine wengi. Kutembea kwake kunaweza kusiwe kwa mbwembwe za mburudishaji na labda ukali wa maneno yake unazidi upanga. Lakini usifanye makosa; Magufuli ni mtu mwenye malengo.

Kuweza kuyaelewa malengo yake kunaweza kuelezewa au kufafanuliwa kwa kuangalia mitazamo au misimamo mikubwa miwili ambayo ndiyo – kwa maoni yangu – inamuongoza. Msimamo wake wa kwanza ni ile imani thabiti, isiyo na utata na wito wake kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla kwamba wajiamini. Siyo kujiamini katika nafasi yao katika ulimwengu tu bali zaidi kuwa na imani katika uwezo wa kujiletea na kuboresha maisha yao. Mara nyingi na katika sehemu nyingi Rais Magufuli amekuwa akizungumza juu ya matamanio yake ya kuona kuwa Watanzania hawajitilii mashaka wao wenyewe. Kwamba, waache kujiona duni na kuwa hawawezi kufikia chochote kile kama taifa na kama mtu mmoja mmoja. Amekataa kuiona Tanzania kama Taifa la watu wa wastani! Wito wake huu wa watu kuwajibika unanguruma kama simba wanaomka kutoka katika jua usingizi wa jua kali ndani mbuga za Serengeti – Tanzania Tunaweza, Afrika Tunaweza!

Mtu anaweza kuchukulia kwa makosa au kupuuzia wito huu na kuona kuwa ni bure na usio na maana. Kwa baadhi yetu hata hivyo, wito huu unanguruma katika mioyo yetu. Unawasha na kuamsha kizazi cha vijana na kuwapa hisia ya kuwajibika kwa Taifa lao na kwao wenyewe. Magufuli anawathubutisha vijana kuzifikia nyota na zaidi! Hakuna lisilowezekana tena kama tukiunganisha akili na nguvu zetu kwa pamoja. Rafiki zangu, haya siyo maneno matupu ya mwanasiasa msomi; Magufuli siyo mmoja wao. Anaona Taifa la watu ambao wanaweza kutamani na kufikia mambo makubwa.

Katika mwanga wa haya, tunaweza kuelewa sababu ya miradi mikubwa ya ujenzi na matumizi makubwa ya umma ambayo ameanzisha au kumalizia au kufikiria kwa upya kabisa. Ni mambo yenye uthubutu, ya kuona mbali, na ni ya lazima. Ujenzi wa Reli katika viwango vya kisasa (SGR), manunuzi ya ndege, Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere, Madaraja, Hospitali na Kliniki na ujenzi wa barabara na mingine mingi ni ishara na uthubutu wa nini kama Taifa tunaweza kufanya.

Msimamo wa pili unaomuongoza Magufuli tunaweza kusema ndio msingi wa ule wa kwanza ni kuwa Magufuli anataka kila Mtanzania siyo tu kujiamini au kuamini uwezo tulio nao lakini pia kuamini na kujua kuwa ndani yetu na ndani ya nchi yetu tuna uwezo na utajiri wa kutosha kuweza kujiletea maendeleo. Kuwa ndani yetu tumejaliwa na Mwenyezi Mungo uwezo wa kuweza kufanya jambo lolote ambalo labda hatukulidhania kuwa tunaweza miaka michache tu iliyopita.

Kufikia mwisho huo Magufuli ameonesha kuwa hatuwezi kuendelea kutegemea misaada ya kigeni kufanya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu. Kuanzia mwanzo wa Urais wake miaka minne iliyopita ameonesha na amejaribu kutukumbusha kuwa tunaweza kujiendeleza sisi wenyewe tu. Mtazamo wa aina hiyo alikuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere miongo zaidi ya mitano nyuma. Haitoshi kujiamini, haitoshi kujua tuna uwezo na utajiri wa asili. Ni lazima tuanze kutenda kama watu ambao wanajiamini. Ni lazima tuanze kujiletea maendeleo sisi wenyewe; hatuwezi kusubiria “wajomba” zetu kutoka ng’ambo kuja kutusaidia.

Hii misimamo miwili – imani katika uwezo wetu kufikia mambo makubwa na kutambua kuwa tuna utajiri wa asili kama nchi na kama watu kuweza kujiletea maendeleo ni kama gundi inayoshikilia mawazo, mipango, malengo, miradi na ndoto za Rais Magufuli. Hata hivyo, ni vizuri kuielewa misimamo hii miwili kuwa inasimama katika nguzo au misingi mikubwa miwili. Bila misingi hii haya yote yanabakia kuwa ni maneno na matamanio tu. Misingi hii kiukweli ndio inaelezea falsafa ya kisiasa ya Rais Magufuli na ukiiangalia ndio inasababisha msuguano na baadhi ya watu. Misingi hii miwili labda haikuwa wazi sana wakati Magufuli akiwa Naibu Waziri au Waziri katika Serikali ya Rais Mkapa au ile ya Rais Kikwete.Kulikuwa na dalili lakini haikufunuliwa kwa uwazi.

Kwanza kabisa, Magufuli amekuwa na toka zamani ameendelea kuwa na hisia ya uharaka wa sasa. Tangu siku ile anazungumza baada ya kuapishwa hadi hivi karibuni kabisa katika mikutano ya hadhara, Magufuli anaona nchi ya Tanzania kama nchi ambayo imechelewa sana kufikia maendeleo. Anaamini kabisa kuwa baadhi ya vitu ambavyo analazimika kuvifanya sasa vilitakiwa viwe vimefanywa miaka mingi huko nyuma. Anatuhumu viongozi waliomtangulia kwa kupoteza fedha, ukosefu wa nidhamu na kukosekana kwa ufanisi. Wakati mwingine anafanya hivi kwa kujificha kidogo lakini wakati mwingine anafanya hivi kwa mashambulizi ya wazi kabisa labda bila kutaja majina lakini sote tunajua ni nani anawazungumzia.

Bahati mbaya anapofanya hivi Magufuli siyo tu anawatuhumu waliomtangulia bali anajituhumu nay eye mwenyewe na chama chake. Na katika hili wengi wa wakosoaji wake naweza kusema wako sahihi kabisa. Tanzania kwa muda wote imetawaliwa na CCM na mtangulizi wake yaani TANU. Sera ambazo zimetekelezwa hadi hivi sasa kwa takribani miaka sitini zote zimetoka kwenye kundi la wasomi ndani ya CCM. Kushindwa kwa utekelezaji au usimamizi ambao umetokea nchini hadi hivi sasa wote umefungwa na jambo moja tu – CCM. Ndio, CCM na serikali yake ndio wanaobeba peke yao na kwa ujumla lawama na aibu yote ya kushindwa kwa kisiasa katika Tanzania. Hakuna chama kingine, hakuna kiongozi mwingine ambaye anayeweza kubeba lawama hizo isipokuwa CCM na viongozi wake. Hivyo, Magufuli anaponyeshea vidole watu wengine yampasa kukumbuka kuwa ni chama chake ndicho kinabeba lawama hizo.

Hili linaelezea kwa kiasi gani kwanini kwenye baadhi ya hotuba zake za hadharani Magufuli ameomba radhi kwa wananchi kwa chama chake kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo. Japo kuwa radhi hizo labda hazikuvutia vichwa vya habari vya magazeti kwa baadhi yetu zilikuwa zinatupa uhakika kuwa Magufuli ni mtu sahihi; hatolei udhuru makosa hayo wala kuyapuuza. Anaelewa kuwa ana wajibu wa kuyasahihisha makosa ya watangulizi wake. Naweza hata kusema kuwa kwa kiasi fulani Magufuli anafuata nyayo za Baba wa Taifa kama alivyoanisha katika ule waraka wake wa kutafakari – Tujisahihishe (1961) au ule wa Tanzania Baada ya Miaka Kumi (1971).

Katika uharaka huu wa sasa, Magufuli pia anafuata ile dhana ya Nyerere ya mwanzoni mwa miaka ya sitini aliposema kuwa “Yatupasa tukimbie wakati wengine wanatembea”. Nyerere alikuwa anazungumzia ile hisia ya kuwa tumechelewa na hivyo Watanzania yawapasa kuwa na moyo wa uharaka na kufanya vizuri ili kuweza kufikia nchi nyingine zilizoendelea. Huwezi kutembea wakati wenzio wanakimbia halafu utarajie kuwafikia.

Magufuli basi anasukumwa na huu “ukali wa uharaka wa sasa” kama Martin Luther King Jr. alivyouita. Hata hivyo inampasa mtu kuwa mwangalifu katika kuufuata uharaka huu. Ni rahisi sana kwa mtu mwenye uharaka kufanya makosa ambayo hayakulazimika kufanywa. Chukulia kwa mfano wakati kujenga majengo fulani ambayo tunasema tunayataka kwa haraka; kama mtu si mwangalifu anaweza kujikuta anapindisha taratibu za uhandisi na ujenzi na matokeo yake majengo ambayo yatakuwa kuishi watu yanaweza kuwa ni ya hatari. Hivyo, hii hisia ya uharaka wa sasa ni lazima iangaliwe na ichukuliwe kwa umakini na uangalifu mkubwa sana kila inapowezekana. Tusije kuingia kwenye mtego wa kuzembea ambao wazee wetu walituasa “Haraka haraka haina baraka”. Lakini vile vile tusije kufanya vitu pole pole mno na kuingia kwenye mtengo wa “pole pole ndio mwendo”. Mtu anaweza kufanya kitu kwa haraka kwa sababu ya papara au akafanya kwa pole pole kwa sababu ya uvivu na uzembe! Ni lazima kutafuta mizani ya mambo haya mawili.

Naweza kuonesha mfano mmoja wa uharaka huu na matokeo yake. Wiki chache zilizopita Waziri Mkuu alitembelea huko Mitengo Mtwara ambapo alioneshwa jengo la Hospitali inayojengwa kwa haraka. Sijui kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo aliona:

(Picha)

Jambo la pili ambalo ni msingi wa misimamo ya Rais Magufuli – kwa maoni yangu - ni jinsi gani anaangalia nafasi ya siasa nchini. Magufuli tangu zamani amekuwa mtu asiyejali usahihi wa kisiasa (political correctness). Hajawahi kuficha jinsi gani asivyopenda siasa. Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akimfuatilia anaweza kuona kuwa Magufuli hajali sana jinsi gani maamuzi yake yanaweza yasiwe na utamu wa kufurahisha wanasiasa. JInsi anavyozungumza na kauli zake zinaweza kuwakwaza wengi; lakini hivi ndivyo alivyokuwa toka akiwa Waziri. Katika hili Magufuli hana jipya. Hii haina maana kuwa Magufuli hatumii siasa kama nyenzo tu kufikia ajenda zake au pale ambapo analazimika kutumia siasa kwa sababu inamfaa.

Ni jambo hili la pili lililomfanya Magufuli aonekane kwa baadhi ya watu kama adui wa upinzani na demokrasia. Ni hili limemfanya kwa kiasi kikubwa kuzuia utajiri mkubwa sa shughuli za kisiasa nchini. Na kwa mara nyingine wakosoaji wake katika hili wako sahihi. Ni wazi kuwa hisia ya uharaka wa sasa ya Magufuli inakinzana na utamaduni wa kidemokrasia ambao tumeuchukua tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Kwa zaidi ya miaka ishirini na mitano tangu vyama vingi virudi Watanzania wamefurahia (japo wakati mwingine kwa jasho na damu) haki za kidemokrasia na za kiraia ambazo zinakuwepo mahali ambapo kuna upinzani ulio haki na wenye nguvu. Tangu zama za Augustino Mrema, Walid Kaborou, James Mapalala hadi Slaa na kutoka kuibuka kwa Zitto hadi Lissu na wengine wengi maisha ya kisiasa ya Tanzania yamekunufaika, kupewa changamoto na yamekua kwa uwepo wa upinzani wenye ujasiri na usiotetereka.

Hata hivyo, hali hii ya kisiasa haiwezi yote kulaumikwa kwa Magufuli. Toka upinzani urejee tumekuwa na hali ya msuguano kati ya serikali na vyama vya upinzani. Hili limekuwa kweli toka wakati wa Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli. Hata hivyo jambo moja lililoko wazi ni kuwa ile hali ya mgongano kati ya upinzani na serikali ambayo ilikuwepo huko nyuma sasa hivi kwa kiasi kikubwa imezimwa. Ile hali ambayo ilisababisha matukio ya Mwembechai, Zanzibar na mauaji mengine yenye mazingira ya kisiasa huko nyuma kwa kiasi chake imeonekana kuwa siyo fanisi sana kama zamani. Imejaribiwa kidogo na mara moja imezimwa bila huruma.

Naamini hata hivyo kuwa msimamo huu wa Magufuli dhidi ya upinzani si wa lazima na wala hautajiki. Ni maoni yangu kuwa kazi yake ambayo inaendelea nchi nzima inatosha kuwa mtetezi wa nia na siasa zake. Inaweza kujitetea yenyewe. Na ninaamini kuwa ili Magufuli afanikiwe na hatimaye kuacha historia ambayo itadumu na labda isiyoweza kufikiwa na mtu mwingine kwa miaka mingi ijayo ni muhimu afikirie upya uhusiano wake na upinzani wa kisiasa. Binafsi siwaoni wapinzani kama kupe mgongoni mwa kiboko; kwamba wanamletea magonjwa na kumsumbua bali kama wale ndege nyangenyange ambao wanatua mgongoni, kuwala kupe na kumsafisha kiboko!

Magufuli anaweza asiwakubali wapinzani au hata kuwapenda; lakini anawahitaji. Anaweza asipende falsafa zao au hata viongozi wake au kwamba tu upinzani upo. Hata hivyo, Katiba yetu ambayo yeye aliiapa kuilinda (na viapo vina maana) basi ni jukumu lake kuona kuwa haki zote za kibinadamu na zile za kiraia zinalindwa na kutetewa. Kwa pumzi ile ile ambayo anatetea miradi na kazi kubwa ambayo anaifanya anatakiwa pia kutetea haki hizi za kisasa na asizione kuwa ni maadui wake. Na hivi viwili havipingani. Na tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani, magufuli ni lazima na muhimu kutafuta namna gani anaweza kufanya kazi na upinzani nchini. Ni muhimu atafute muafaka wa kufanya kazi na upinzani. Tayari nina uhakika wa kutosha kuwa ameshaonesha uthabiti wake wa kufanya kazi na watu mbalimbali na sioni kama kuna tatizo lolote la kulegeza mazingira ya kisiasa nchini ili upinzani uweze kufanya shughuli zake.

Katika mwanga wa haya yote, ninapoangalia miaka minne iliyopita ya Urais wa Magufuli naweza kuona matumaini katikati ya waliokata tamaa, mwanga kwenye mwisho wa handaki, na naweza kuona maisha bora kwelikweli huko mbeleni itakapofikia tamati yake. Naweza kumuona Magufuli kama daktari wa chumba cha wagonjwa wa dharura; jukumu lake la kwanza siyo tu kumponya mgonjwa bali kuzuia umwagikaji wa damu, kuziba majeraha na kutibu matatizo ya msingi kwanza ili kumweka mgonjwa katika hali ya usalama ili aweze kupatiwa matibabu ya ndani zaidi. Kwa mtu mwingine, hatua hizi zinaweza kuonekana ni kali na za kikatili; lakini kwa mtu anayeleewa anaweza kuona kuwa hatua hizi ni za lazima na za dharura. Ni maoni yangu kuwa ngwe ya pili ya Magufuli itakuwa na utofauti mkubwa na hii ya kwanza, kwani miaka mitano ijayo itakuwa ni suala la kuacha alama bora za kudumu ambazo zitaacha historia. Katika hili sina mashaka.

Ni dikteta uchwara? Labda! Ni bosi mkali mwenye ukarimu? Inawezekana! Ni kiongozi Mwafrika kwenye utofauti fulani hivi? Bila ya shaka! Kiongozi ambaye Watanzania kwa muda mrefu walikuwa wanamtamania na hatimaye kumpata? Ndiyo! Ngwe mbili za Magufuli zitakapofikia kikomo chake Watanzania watakuwa na furaha ya kuwa na mtu aliyethubutisha muda kwa kuwa jasiri na mwenye malengo yenye kipimo mara mbili cha ujasiri na uthubutu. Tunapoangalia ujio wa 2020 na baadaye, Magufuli atakuja kuhukumiwa na historia siyo kwa majengo na miradi mikubwa ambayo atakuwa amefanikisha (hilo litakuwa sehemu tu) lakini ni kwa kiasi gani ameacha Taifa na wananchi wake wanajisikiaje. Kwa ufupi, atahukumiwa kwa jinsi gani ameweza kudhibiti hisia na mitazamo yake na misingi ya mitazamo hiyo ambayo nimeifafanua hapo juu.

Anapoenda kwenye miaka mitano ijayo; kuna kila dalili kuwa siyo Magufuli anaweza kuwashangaza Watanzania na dunia kwa mambo ambayo atakuwa ameyakamilisha lakini naamini kuna jambo kubwa ambalo liko mbeleni. Kwa wakosoaji na maadui zake wa kisiasa; naamini Magufuli anaweza kuacha demokrasia yenye nguvu zaidi kuliko wakati wowote wa historia yetu. Kama daktari bingwa sasa hivi inaonekana kwa baadhi ya watu hali ni mbaya; lakini hili lote ni katika kuponya madhara ya mfumo wa utawala wa kifisadi. Mgonjwa akiponywa na akianza kurejea kwenye afya yake kamili Tanzania itakuwa ni taifa la aina yake na watu wake watatembea tena kifua mbele. Magufuli, shughuli!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Kuna matatizo katika nchi yetu hakuna maana kwenye ujasiri wa mtu tunaweza kudhani ni mwema kumbe tunampa msaada katika maisha yake.

Kwa mfano juzi tumesikia kauli za Rais Benjamin MKAPA, kwamba aliruhusu pesa za umma (EPA) zitumike kwa maslahi ya watu wachache ndani ya CCM. Lakini hata baada ya kustaafu, hakuna anayeweza kimwajibisha.

Pia na yeye ipo siku atasema 1.5trillion alikula yeye na familia yake hizo tunazo jua lakini kuna kuna za nyuma ya pazia. Ukubwa wa katiba kwa rais ndio matatizo ya nchi yetu.

Tubadilike kwenye hoja ili tuweze kusaidia nchi.
 
Kama ungefahamu kwamba nchi haikutoa ajira kwa miaka 4 sasa wala kuongeza mshahara wa wafanyakazi hata mara moja basi bila shaka ungetazama upya hoja yako , Lingine ni hili , umewahi kujiuliza sababu hasa ya watu kuutaka urais wa nchi ? hebu rudi kaangalie kwanini mtu anaomba urais wa nchi , ukiongeza na yale ya Kikatiba , hasa majukumu ya Rais ni yapi ?
 
Binafsi nilimuunga mkono 2015 baada ya Chadema kubadili gia angani kisa tu kwenda Ikulu bila kujali nani tunaenda nae.

Hata baada ya miaka hii minne bado sijaona mbadala wake hasa kutoka upinzani , naamini mbadala wa kweli wa Magufuli atatoka ndani ya CCM.

Kuminya vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, kutoheshimu mihimili mingine, kujiamulia matumizi nje ya bajeti, Kubambikia Wapinzani kesi, kuwapa viongizi vijana nguvu zilizo nje ya uwezo wao.

Ni vitu ambavyo vinampunguzia Rais thamani mbele ya walio wengi.

Akiweza kurekebisha hayo anaweza kuwa Rais bora kabisa ukianza na Mzee Mwinyi....
 
Ulivyo toa Hoja yako ni kama vile unaona ni sawa sawa kukanyaga Sheria ili mambo yaende kwa Haraka na papo hapo una sahau Sababu ya Sheria kuwepo.

Hayo ya Reli /Bwawa la kufua Umeme /Ununuzi wa Ndege ni baadhi ya mambo yanayo fanywa na Serikali nyingi ,lakini hayo yanaleta maana na kuwa ni mazuri na yenye tija kama Sheria zita zingatiwa ili yatekelezwe

Unajenga Barabara unawavunjia Watu Nyumba zao lakini haufuati Sheria ina maana yoyote kweli hiyo ?.(Wakazi wa Kimara ni mfano mzuri).

Serikali makini na inayo jali Haki za Binadamu wengine ikiwa inaboresha Maisha ya Raia wake inapaswa kuwa makini kwa kufuata utaratibu tulio jiwekea, sio unaamua tu kununua Ndege kesho unaagiza na kulipa Cash bila ya ushirikishwaji wa Wananchi ambao Kodi yao ndio inatumika.Endelea tu kutetea Mkuu.
 
Mzee Mwanakijiji
Nasubiri utakapo zungumzia vifo/Kupotea kw akina Mawazo, Anzory, Ben saanane na wengine wengi bila kusahau maiti z akwenye Viroba Ruvu na Oyster-bay beach.

Nasubiri utakapo tambua na kuzungumzia dhuluma zilizofanywa na TRA kwa wafanya bashara kwa amri zake na dharahu zake na sasaamejirudi na kujifanya sio yeye.

Nasubiri utakapozungumzia sukari 1800 na kwa amri zake na fujo leo sukari 2500.

Nasubiri utakapozungumzia waliofilisika na kujua kwa maamuzi ya gafla ya kufuta viroba(Konyagi) na kuacha kufuata mfumo bora makamba.

Nasubiri utakapuzungumzia uvunjwaji wa sheria na katiba, mahakama na bunge giza na udhalilishaji wa CAG.
 
MKuu Tumuulize kwanini tulimfukuza MKOLONI ?
 
Kuna matatizo katika nchi yetu hakuna maana kwenye ujasiri wa mtu tunaweza kudhani ni mwema kumbe tunampa msaada katika maisha yake.

Kwa mfano juzi tumesikia kauli za Rais Benjamin MKAPA, kwamba aliruhusu pesa za umma (EPA) zitumike kwa maslahi ya watu wachache ndani ya CCM. Lakini hata baada ya kustaafu, hakuna anayeweza kimwajibisha.

Pia na yeye ipo siku atasema 1.5trillion alikula yeye na familia yake hizo tunazo jua lakini kuna kuna za nyuma ya pazia. Ukubwa wa katiba kwa rais ndio matatizo ya nchi yetu.

Tubadilike kwenye hoja ili tuweze kusaidia nchi.

Umeongea ya Msingi sana ,tatizo lipo kwenye Katiba hasa Madaraka ya hawa Wakuu wa Nchi kuto shitakiwa.Tumepoteza zaidi Sababu alie shikilia kijiti aliwahi kutamka kuwa Katiba sio kipaumbele chake kabisa.
 
Mimi niwapongeze tu wote walioweza kusoma pumba lote hapo juu la mtu anayejitafutia kushibisha tumbo lake.

Yataka Moyo Sana Kujifyatua Akili
 
Binafsi nilimuunga mkono 2015 baada ya Chadema kubadili gia angani kisa tu kwenda Ikulu bila kujali nani tunaenda nae.

Hata baada ya miaka hii minne bado sijaona mbadala wake hasa kutoka upinzani , naamini mbadala wa kweli wa Magufuli atatoka ndani ya CCM.

Kuminya vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, kutoheshimu mihimili mingine, kujiamulia matumizi nje ya bajeti, Kubambikia Wapinzani kesi, kuwapa viongizi vijana nguvu zilizo nje ya uwezo wao.

Ni vitu ambavyo vinampunguzia Rais thamani mbele ya walio wengi.

Akiweza kurekebisha hayo anaweza kuwa Rais bora kabisa ukianza na Mzee Mwinyi....
Kama hana mbadala kwanini usikubaliane na udikteta wake pia ?
 
Hawezi kwa sababu hapo atakuwa hasifii bali anakosoa
Mzee Mwanakijiji
Nasubiri utakapo zungumzia vifo/Kupotea kw akina Mawazo, Anzory, Ben saanane na wengine wengi bila kusahau maiti z akwenye Viroba Ruvu na Oyster-bay beach.

Nasubiri utakapo tambua na kuzungumzia dhuluma zilizofanywa na TRA kwa wafanya bashara kwa amri zake na dharahu zake na sasaamejirudi na kujifanya sio yeye.

Nasubiri utakapozungumzia sukari 1800 na kwa amri zake na fujo leo sukari 2500.

Nasubiri utakapozungumzia waliofilisika na kujua kwa maamuzi ya gafla ya kufuta viroba(Konyagi) na kuacha kufuata mfumo bora makamba.

Nasubiri utakapuzungumzia uvunjwaji wa sheria na katiba, mahakama na bunge giza na udhalilishaji wa CAG.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni dikteta uchwara? Labda! Ni bosi mkali mwenye ukarimu? Inawezekana! Ni kiongozi Mwafrika kwenye utofauti fulani hivi? Bila ya shaka! Kiongozi ambaye Watanzania kwa muda mrefu walikuwa wanamtamania na hatimaye kumpata? Ndiyo! Tangu kuchaguliwa kwake miaka minne iliyopita Rais Magufuli amekuwa ni Rais ambaye anagusa Watanzania kwa namna mbalimbali tena zinazopingana sana. Kwa wengine unapotaja jina lake tu wanajisikia kujikunyata na kubeza, huku wengine wakimsifia. Kwa wengine ukilitaja jina lake wanajisikia fahari na hisia ya uzalendo ambayo haijaonekana ncihni labda tangu Baba wa Taifa alipokuwa akizunguka nchini wakati wa harakati za uhuru miaka ya 1950.

Ingawa yapo mambo mengi ambayo hayalingani kati ya viongozi hawa wawili, ni rahisi kuweza kuona usambamba fulani baina yao. Hili linawezekana kuonekana angalau kwa mambo mawili – Nyerere na Magufuli wanaonesha kwa kiasi kikubwa imani yao isiyofichika juu ya uwezo wa Watanzania kujiletea maendeleo yao wenyewe. Na pili, wote wawili – Nyerere na Magufuli – wanachukulia hasa katika miaka yao ya mwanzo ya uongozi wao kuwa siasa inaweza kuwa ni kizuizi cha maendeleo.

Hata hivyo, mwelekeo wa Nyerere kuhusu mambo hayo unaweza kuelezewa kwa kuangalia masuala ya kihistoria ya zama zake au katika kusoma falsafa yake ya kisiasa – Magufuli ni vigumu kumuelewa kwani misimamo yake ya kisiasa haijaelezwa na kufafanuliwa kwa uwazi kama Nyerere. Kutokana na hilo ni vigumu kama siyo sawa kuwalinganisha viongozi hawa wawili na kufikia hitimisho sahihi. Kupita kwa zaidi ya nusu karne tangu wote wawili washike madaraka ya Urais wa Tanzania kunafanya ulinganishaji wowote wa hawa wawili kuwa mgumu kama usiowezekana kabisa. Hii haina maana kazi za kisomi au uchambuzi wa kihistoria kuhusu viongozi wawili usifanyike au usiwezekane kufanyika na kuweza kupambanua mfanano au utofauti wao.

Kama mtu ambaye nilimuunga mkono wazi Rais Magufuli 2015 naamini ninawajibika kwa kiasi fulani kutoa mawazo yangu juu ya miaka hii minne ya kuuangalia utawala wa Rais Magufuli. Uamuzi wangu ulikuwa ni uamuzi mgumu wakati ule na inawezekana bado hauna maarufu hadi hii leo. Nimepoteza marafiki wengi – au niliwadhania kuwa ni marafiki – kwa sababu ya kumuunga mkono Magufuli. Baadhi ya watu ambao tulianza nao kumuunga mkono Magufuli wakati ule sasa hivi wamegeuka na wanajutia uamuzi wao. Nikiwa mwanademokrasia wa kweli sishangazwi wala sijaumizwa na watu ambao wamegeuka sasa kwani tofauti ya misimamo, maoni, mitazamo nk. ndio msingi wa demokrasia ya kweli na natetea haki ya wanaonipinga kunipinga kwa nguvu zote.

Hata hivyo nimebakia na marafiki wengine wengi ambao hatuna misimamo ile ile; hawakumuunga mkono na mimi sikumuunga mkono mgombea wao. Hili limenipa nafasi ya kipekee kuweza kuelewa hoja mbalimbali za marafiki zangu kuhusu utawala wa Magufuli na kunifanya mara kwa mara nipime maamuzi na misimamo yangu vile vile ya kumuunga mkono Magufuli. Je, nilikosoea kumuunga mkono Magufuli? Je, ningeendelea kuunga mkono Upinzani baada ya ule Usaliti Mkuu wa Upinzani wa 2015? Hivyo basi unaofuata ni sehemu tu ya utetezi wangu juu ya Magufuli; kwa uwazi na kwa makusudi kabisa.

Miaka minne baadaye nimeona nilichoona, nimesikia nilichosikia na nimefikia hitimisho lisilo na utata kuwa Rais Magufuli ni kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamtamania, kuombea na hatimaye kumpata. Ni mtu wa vitendo, akija na kipimo mara mbili cha ujasiri na uthubutu. Ulimi wake unaweza usiwe mzuri sana kiama wengine na mtindo wake usifanane na wa wengine wengi. Kutembea kwake kunaweza kusiwe kwa mbwembwe za mburudishaji na labda ukali wa maneno yake unazidi upanga. Lakini usifanye makosa; Magufuli ni mtu mwenye malengo.

Kuweza kuyaelewa malengo yake kunaweza kuelezewa au kufafanuliwa kwa kuangalia mitazamo au misimamo mikubwa miwili ambayo ndiyo – kwa maoni yangu – inamuongoza. Msimamo wake wa kwanza ni ile imani thabiti, isiyo na utata na wito wake kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla kwamba wajiamini. Siyo kujiamini katika nafasi yao katika ulimwengu tu bali zaidi kuwa na imani katika uwezo wa kujiletea na kuboresha maisha yao. Mara nyingi na katika sehemu nyingi Rais Magufuli amekuwa akizungumza juu ya matamanio yake ya kuona kuwa Watanzania hawajitilii mashaka wao wenyewe. Kwamba, waache kujiona duni na kuwa hawawezi kufikia chochote kile kama taifa na kama mtu mmoja mmoja. Amekataa kuiona Tanzania kama Taifa la watu wa wastani! Wito wake huu wa watu kuwajibika unanguruma kama simba wanaomka kutoka katika jua usingizi wa jua kali ndani mbuga za Serengeti – Tanzania Tunaweza, Afrika Tunaweza!

Mtu anaweza kuchukulia kwa makosa au kupuuzia wito huu na kuona kuwa ni bure na usio na maana. Kwa baadhi yetu hata hivyo, wito huu unanguruma katika mioyo yetu. Unawasha na kuamsha kizazi cha vijana na kuwapa hisia ya kuwajibika kwa Taifa lao na kwao wenyewe. Magufuli anawathubutisha vijana kuzifikia nyota na zaidi! Hakuna lisilowezekana tena kama tukiunganisha akili na nguvu zetu kwa pamoja. Rafiki zangu, haya siyo maneno matupu ya mwanasiasa msomi; Magufuli siyo mmoja wao. Anaona Taifa la watu ambao wanaweza kutamani na kufikia mambo makubwa.

Katika mwanga wa haya, tunaweza kuelewa sababu ya miradi mikubwa ya ujenzi na matumizi makubwa ya umma ambayo ameanzisha au kumalizia au kufikiria kwa upya kabisa. Ni mambo yenye uthubutu, ya kuona mbali, na ni ya lazima. Ujenzi wa Reli katika viwango vya kisasa (SGR), manunuzi ya ndege, Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere, Madaraja, Hospitali na Kliniki na ujenzi wa barabara na mingine mingi ni ishara na uthubutu wa nini kama Taifa tunaweza kufanya.

Msimamo wa pili unaomuongoza Magufuli tunaweza kusema ndio msingi wa ule wa kwanza ni kuwa Magufuli anataka kila Mtanzania siyo tu kujiamini au kuamini uwezo tulio nao lakini pia kuamini na kujua kuwa ndani yetu na ndani ya nchi yetu tuna uwezo na utajiri wa kutosha kuweza kujiletea maendeleo. Kuwa ndani yetu tumejaliwa na Mwenyezi Mungo uwezo wa kuweza kufanya jambo lolote ambalo labda hatukulidhania kuwa tunaweza miaka michache tu iliyopita.

Kufikia mwisho huo Magufuli ameonesha kuwa hatuwezi kuendelea kutegemea misaada ya kigeni kufanya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu. Kuanzia mwanzo wa Urais wake miaka minne iliyopita ameonesha na amejaribu kutukumbusha kuwa tunaweza kujiendeleza sisi wenyewe tu. Mtazamo wa aina hiyo alikuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere miongo zaidi ya mitano nyuma. Haitoshi kujiamini, haitoshi kujua tuna uwezo na utajiri wa asili. Ni lazima tuanze kutenda kama watu ambao wanajiamini. Ni lazima tuanze kujiletea maendeleo sisi wenyewe; hatuwezi kusubiria “wajomba” zetu kutoka ng’ambo kuja kutusaidia.

Hii misimamo miwili – imani katika uwezo wetu kufikia mambo makubwa na kutambua kuwa tuna utajiri wa asili kama nchi na kama watu kuweza kujiletea maendeleo ni kama gundi inayoshikilia mawazo, mipango, malengo, miradi na ndoto za Rais Magufuli. Hata hivyo, ni vizuri kuielewa misimamo hii miwili kuwa inasimama katika nguzo au misingi mikubwa miwili. Bila misingi hii haya yote yanabakia kuwa ni maneno na matamanio tu. Misingi hii kiukweli ndio inaelezea falsafa ya kisiasa ya Rais Magufuli na ukiiangalia ndio inasababisha msuguano na baadhi ya watu. Misingi hii miwili labda haikuwa wazi sana wakati Magufuli akiwa Naibu Waziri au Waziri katika Serikali ya Rais Mkapa au ile ya Rais Kikwete.Kulikuwa na dalili lakini haikufunuliwa kwa uwazi.

Kwanza kabisa, Magufuli amekuwa na toka zamani ameendelea kuwa na hisia ya uharaka wa sasa. Tangu siku ile anazungumza baada ya kuapishwa hadi hivi karibuni kabisa katika mikutano ya hadhara, Magufuli anaona nchi ya Tanzania kama nchi ambayo imechelewa sana kufikia maendeleo. Anaamini kabisa kuwa baadhi ya vitu ambavyo analazimika kuvifanya sasa vilitakiwa viwe vimefanywa miaka mingi huko nyuma. Anatuhumu viongozi waliomtangulia kwa kupoteza fedha, ukosefu wa nidhamu na kukosekana kwa ufanisi. Wakati mwingine anafanya hivi kwa kujificha kidogo lakini wakati mwingine anafanya hivi kwa mashambulizi ya wazi kabisa labda bila kutaja majina lakini sote tunajua ni nani anawazungumzia.

Bahati mbaya anapofanya hivi Magufuli siyo tu anawatuhumu waliomtangulia bali anajituhumu nay eye mwenyewe na chama chake. Na katika hili wengi wa wakosoaji wake naweza kusema wako sahihi kabisa. Tanzania kwa muda wote imetawaliwa na CCM na mtangulizi wake yaani TANU. Sera ambazo zimetekelezwa hadi hivi sasa kwa takribani miaka sitini zote zimetoka kwenye kundi la wasomi ndani ya CCM. Kushindwa kwa utekelezaji au usimamizi ambao umetokea nchini hadi hivi sasa wote umefungwa na jambo moja tu – CCM. Ndio, CCM na serikali yake ndio wanaobeba peke yao na kwa ujumla lawama na aibu yote ya kushindwa kwa kisiasa katika Tanzania. Hakuna chama kingine, hakuna kiongozi mwingine ambaye anayeweza kubeba lawama hizo isipokuwa CCM na viongozi wake. Hivyo, Magufuli anaponyeshea vidole watu wengine yampasa kukumbuka kuwa ni chama chake ndicho kinabeba lawama hizo.

Hili linaelezea kwa kiasi gani kwanini kwenye baadhi ya hotuba zake za hadharani Magufuli ameomba radhi kwa wananchi kwa chama chake kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo. Japo kuwa radhi hizo labda hazikuvutia vichwa vya habari vya magazeti kwa baadhi yetu zilikuwa zinatupa uhakika kuwa Magufuli ni mtu sahihi; hatolei udhuru makosa hayo wala kuyapuuza. Anaelewa kuwa ana wajibu wa kuyasahihisha makosa ya watangulizi wake. Naweza hata kusema kuwa kwa kiasi fulani Magufuli anafuata nyayo za Baba wa Taifa kama alivyoanisha katika ule waraka wake wa kutafakari – Tujisahihishe (1961) au ule wa Tanzania Baada ya Miaka Kumi (1971).

Katika uharaka huu wa sasa, Magufuli pia anafuata ile dhana ya Nyerere ya mwanzoni mwa miaka ya sitini aliposema kuwa “Yatupasa tukimbie wakati wengine wanatembea”. Nyerere alikuwa anazungumzia ile hisia ya kuwa tumechelewa na hivyo Watanzania yawapasa kuwa na moyo wa uharaka na kufanya vizuri ili kuweza kufikia nchi nyingine zilizoendelea. Huwezi kutembea wakati wenzio wanakimbia halafu utarajie kuwafikia.

Magufuli basi anasukumwa na huu “ukali wa uharaka wa sasa” kama Martin Luther King Jr. alivyouita. Hata hivyo inampasa mtu kuwa mwangalifu katika kuufuata uharaka huu. Ni rahisi sana kwa mtu mwenye uharaka kufanya makosa ambayo hayakulazimika kufanywa. Chukulia kwa mfano wakati kujenga majengo fulani ambayo tunasema tunayataka kwa haraka; kama mtu si mwangalifu anaweza kujikuta anapindisha taratibu za uhandisi na ujenzi na matokeo yake majengo ambayo yatakuwa kuishi watu yanaweza kuwa ni ya hatari. Hivyo, hii hisia ya uharaka wa sasa ni lazima iangaliwe na ichukuliwe kwa umakini na uangalifu mkubwa sana kila inapowezekana. Tusije kuingia kwenye mtego wa kuzembea ambao wazee wetu walituasa “Haraka haraka haina baraka”. Lakini vile vile tusije kufanya vitu pole pole mno na kuingia kwenye mtengo wa “pole pole ndio mwendo”. Mtu anaweza kufanya kitu kwa haraka kwa sababu ya papara au akafanya kwa pole pole kwa sababu ya uvivu na uzembe! Ni lazima kutafuta mizani ya mambo haya mawili.

Naweza kuonesha mfano mmoja wa uharaka huu na matokeo yake. Wiki chache zilizopita Waziri Mkuu alitembelea huko Mitengo Mtwara ambapo alioneshwa jengo la Hospitali inayojengwa kwa haraka. Sijui kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo aliona:

(Picha)

Jambo la pili ambalo ni msingi wa misimamo ya Rais Magufuli – kwa maoni yangu - ni jinsi gani anaangalia nafasi ya siasa nchini. Magufuli tangu zamani amekuwa mtu asiyejali usahihi wa kisiasa (political correctness). Hajawahi kuficha jinsi gani asivyopenda siasa. Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akimfuatilia anaweza kuona kuwa Magufuli hajali sana jinsi gani maamuzi yake yanaweza yasiwe na utamu wa kufurahisha wanasiasa. JInsi anavyozungumza na kauli zake zinaweza kuwakwaza wengi; lakini hivi ndivyo alivyokuwa toka akiwa Waziri. Katika hili Magufuli hana jipya. Hii haina maana kuwa Magufuli hatumii siasa kama nyenzo tu kufikia ajenda zake au pale ambapo analazimika kutumia siasa kwa sababu inamfaa.

Ni jambo hili la pili lililomfanya Magufuli aonekane kwa baadhi ya watu kama adui wa upinzani na demokrasia. Ni hili limemfanya kwa kiasi kikubwa kuzuia utajiri mkubwa sa shughuli za kisiasa nchini. Na kwa mara nyingine wakosoaji wake katika hili wako sahihi. Ni wazi kuwa hisia ya uharaka wa sasa ya Magufuli inakinzana na utamaduni wa kidemokrasia ambao tumeuchukua tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Kwa zaidi ya miaka ishirini na mitano tangu vyama vingi virudi Watanzania wamefurahia (japo wakati mwingine kwa jasho na damu) haki za kidemokrasia na za kiraia ambazo zinakuwepo mahali ambapo kuna upinzani ulio haki na wenye nguvu. Tangu zama za Augustino Mrema, Walid Kaborou, James Mapalala hadi Slaa na kutoka kuibuka kwa Zitto hadi Lissu na wengine wengi maisha ya kisiasa ya Tanzania yamekunufaika, kupewa changamoto na yamekua kwa uwepo wa upinzani wenye ujasiri na usiotetereka.

Hata hivyo, hali hii ya kisiasa haiwezi yote kulaumikwa kwa Magufuli. Toka upinzani urejee tumekuwa na hali ya msuguano kati ya serikali na vyama vya upinzani. Hili limekuwa kweli toka wakati wa Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli. Hata hivyo jambo moja lililoko wazi ni kuwa ile hali ya mgongano kati ya upinzani na serikali ambayo ilikuwepo huko nyuma sasa hivi kwa kiasi kikubwa imezimwa. Ile hali ambayo ilisababisha matukio ya Mwembechai, Zanzibar na mauaji mengine yenye mazingira ya kisiasa huko nyuma kwa kiasi chake imeonekana kuwa siyo fanisi sana kama zamani. Imejaribiwa kidogo na mara moja imezimwa bila huruma.

Naamini hata hivyo kuwa msimamo huu wa Magufuli dhidi ya upinzani si wa lazima na wala hautajiki. Ni maoni yangu kuwa kazi yake ambayo inaendelea nchi nzima inatosha kuwa mtetezi wa nia na siasa zake. Inaweza kujitetea yenyewe. Na ninaamini kuwa ili Magufuli afanikiwe na hatimaye kuacha historia ambayo itadumu na labda isiyoweza kufikiwa na mtu mwingine kwa miaka mingi ijayo ni muhimu afikirie upya uhusiano wake na upinzani wa kisiasa. Binafsi siwaoni wapinzani kama kupe mgongoni mwa kiboko; kwamba wanamletea magonjwa na kumsumbua bali kama wale ndege nyangenyange ambao wanatua mgongoni, kuwala kupe na kumsafisha kiboko!

Magufuli anaweza asiwakubali wapinzani au hata kuwapenda; lakini anawahitaji. Anaweza asipende falsafa zao au hata viongozi wake au kwamba tu upinzani upo. Hata hivyo, Katiba yetu ambayo yeye aliiapa kuilinda (na viapo vina maana) basi ni jukumu lake kuona kuwa haki zote za kibinadamu na zile za kiraia zinalindwa na kutetewa. Kwa pumzi ile ile ambayo anatetea miradi na kazi kubwa ambayo anaifanya anatakiwa pia kutetea haki hizi za kisasa na asizione kuwa ni maadui wake. Na hivi viwili havipingani. Na tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani, magufuli ni lazima na muhimu kutafuta namna gani anaweza kufanya kazi na upinzani nchini. Ni muhimu atafute muafaka wa kufanya kazi na upinzani. Tayari nina uhakika wa kutosha kuwa ameshaonesha uthabiti wake wa kufanya kazi na watu mbalimbali na sioni kama kuna tatizo lolote la kulegeza mazingira ya kisiasa nchini ili upinzani uweze kufanya shughuli zake.

Katika mwanga wa haya yote, ninapoangalia miaka minne iliyopita ya Urais wa Magufuli naweza kuona matumaini katikati ya waliokata tamaa, mwanga kwenye mwisho wa handaki, na naweza kuona maisha bora kwelikweli huko mbeleni itakapofikia tamati yake. Naweza kumuona Magufuli kama daktari wa chumba cha wagonjwa wa dharura; jukumu lake la kwanza siyo tu kumponya mgonjwa bali kuzuia umwagikaji wa damu, kuziba majeraha na kutibu matatizo ya msingi kwanza ili kumweka mgonjwa katika hali ya usalama ili aweze kupatiwa matibabu ya ndani zaidi. Kwa mtu mwingine, hatua hizi zinaweza kuonekana ni kali na za kikatili; lakini kwa mtu anayeleewa anaweza kuona kuwa hatua hizi ni za lazima na za dharura. Ni maoni yangu kuwa ngwe ya pili ya Magufuli itakuwa na utofauti mkubwa na hii ya kwanza, kwani miaka mitano ijayo itakuwa ni suala la kuacha alama bora za kudumu ambazo zitaacha historia. Katika hili sina mashaka.

Ni dikteta uchwara? Labda! Ni bosi mkali mwenye ukarimu? Inawezekana! Ni kiongozi Mwafrika kwenye utofauti fulani hivi? Bila ya shaka! Kiongozi ambaye Watanzania kwa muda mrefu walikuwa wanamtamania na hatimaye kumpata? Ndiyo! Ngwe mbili za Magufuli zitakapofikia kikomo chake Watanzania watakuwa na furaha ya kuwa na mtu aliyethubutisha muda kwa kuwa jasiri na mwenye malengo yenye kipimo mara mbili cha ujasiri na uthubutu. Tunapoangalia ujio wa 2020 na baadaye, Magufuli atakuja kuhukumiwa na historia siyo kwa majengo na miradi mikubwa ambayo atakuwa amefanikisha (hilo litakuwa sehemu tu) lakini ni kwa kiasi gani ameacha Taifa na wananchi wake wanajisikiaje. Kwa ufupi, atahukumiwa kwa jinsi gani ameweza kudhibiti hisia na mitazamo yake na misingi ya mitazamo hiyo ambayo nimeifafanua hapo juu.

Anapoenda kwenye miaka mitano ijayo; kuna kila dalili kuwa siyo Magufuli anaweza kuwashangaza Watanzania na dunia kwa mambo ambayo atakuwa ameyakamilisha lakini naamini kuna jambo kubwa ambalo liko mbeleni. Kwa wakosoaji na maadui zake wa kisiasa; naamini Magufuli anaweza kuacha demokrasia yenye nguvu zaidi kuliko wakati wowote wa historia yetu. Kama daktari bingwa sasa hivi inaonekana kwa baadhi ya watu hali ni mbaya; lakini hili lote ni katika kuponya madhara ya mfumo wa utawala wa kifisadi. Mgonjwa akiponywa na akianza kurejea kwenye afya yake kamili Tanzania itakuwa ni taifa la aina yake na watu wake watatembea tena kifua mbele. Magufuli, shughuli!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
CCM ni ile ile ufisadi upo palepale ununuzi wa Ndege ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni ufisadi mkubwa ndiyo maana kaamua kumtoa kafara CAG apate kupumua
 
Back
Top Bottom