Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Hii hutapata wachangiaji kwa maana haina matusi kwa upandeuleee wa CC..... na pia ni kama unasimanga kundi fulani hivi, ila big up umeandika kizalendo.
 
1. asiende kwenye nyumba za ibada kushawishi apewe kura.

2. asiseme atajenga bara bara na kudumisha afya kwani ni wajibu wa serikali kutenda izo kazi na awatumii pesa yao bali ni kodi za wananchi.. sitoi kura ukija na sera za dizaini hii.

3. tunamtaka raisi ataeinua uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na kutoa vipaumbele kwa elimu, kilimo na viwanda. kwanini? hii itasaidia sana kwa vijana wengi kupata ajira, wakulima kuuza bidhaa zao kwa viwanda vya ndanii. Itasaidia kuinua uchumi wa nchi sana kwa kuuza bidhaa za viwandani ndani na nje ya nchi pia wakulima watauza bidhaa na kupata soko nje na ndani. na watanzania wengi watapata ajira.

4. Asiingize siasa kila sekta mfano mzuri ni sekta ya elimu.. Hii sio sekta ya kufanya mambo ya mzaa kama kufaulisha wanafunzi ili upate kura. Watoto hawajui kusoma wanaenda form one.. Hii italeta madhara kwa nchi sanaa kwani kuna ushindani wa kidunia katika ajira sio ajabu kwa mtanzania kuajiriwa marekani, kenya na popote pale. Ila ukiwa na wajinga wenye vyeti vya ufaulu mzuri madhara yake ni makubwa sana ndani ya taifa ndio yalee tunayoyaona kwa baadhi ya vijana, waheshimiwa flani waliokosa uadilifu. Ili taifa liendelee inabidi kuwe na watendaji wenye upeo. Hata ukishinda kwa kufaulisha watu wewe na familia yako mtapata neema ila Tanzania jee?

5. Raisi awe mjasiri asiye yumbishwa, mzalendo ataeweza kuondoa mfumo ulioko sasa wa kujuana ndio ufanikiwe natoa mifano kidogoo katika soko la ajira uwezi kupata mpaka ujue mtu. pili kwa sasa Tanzania kila kitu mpaka uwe mtoto wa mkubwa ndio ufanikiwe hii imeonekana sanaa sehemu nyingi hata katika shindano la miss tz ambae kafoji vyetii sio hukoo tuu ila wenzangu na mimi tukifojii ndio sheria inafanya kazi.. Hatutaki rais ataeendeleza huo upuuzi kila mmoja awe chini ya sheria.

6. rais mwenye msimamo hasa katika maamuzi yake yakiutawalaa... Kazi ya uraisi ni kazi yenye changamoto kubwa sanaa inabidi uweledi wa hali ya juu sana.. Tunamtaka kiongozi asiekata tamaa akipata changamoto za kiutawala kiasi cha kukimbia madarakani. Viongozi wengi walioachia ngazi baada ya kutoa maamuzii yasiyo na weledi na kuachia ngazi hawafai kabisa kwani atafanya jambo kwa taifa na kukimbia nchi.

7. asiwe na skendo zozote za wizi, ufisadi, uroho wa madaraka, mbinafsi, kinyongo, awe mpenda haki na anaesimamia sheria.

8. afanye mambo kwa maslahi ya taifa na sio kwa ajili ya chama chake sio kiongozi ataewaondoa madarakani wabunge wa chama chake baada ya kuboronga kwa maslahi ya chama bali kwa ajili ya taifa. Na kiongozi akipatikana na kosa lolote mfano la wizii achukuliwe hatua kali ikiwa pamoja na kufungwa kama anastahili.. Sio kusema fedha zirejeshwe na kujiuzulu hapana.. Kwani uraiani ukiiba kuku raia awakwambiii urudishe utafungwa au kuuliwa. Watu woteeee tuwe chini ya sheria na kuwajibika kutokana na matendo yetu.

9. awe na upeo mpana wa kukabiliana na changamoto za kiutalawa, asikie kilio cha wananchi, aweze kushughulikia mambo. Sio kiongozi unaulizwa kwanini nchi yako haina umeme unasema sijui au mimi sio Mungu. Wakati kuna vyanzo vingi vya umeme mfanoo makaa ya mawe, uranium, sio kutegemea umeme wa majii tuu.

10. Tanzania ni nchi yenye mali nyingi sanaa ikiwamo madini, milima,maji,bahari, mbuga za wanyama na vituo vingi vya kitalii n.k japo ni nchi masikini sana. Tunamtaka kiongozi ataeweka sera nzuri zinazotekelezeka ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ya kuzilinda na kuziifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tuipende nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwafikiria wataokuja baada ya kizazi hiki wasikute mashimoo tuu, tembo hakuna, vifaru hakuna wataishi maisha magumu sana kwa ajili ya mababu zao sio jambo jema. Kiongozi bora ni yule anaetaka taifa liwe imara hata baada ya yeye kutoka madarakani.

11. Asimamie katiba iwe katiba itayotoa haki sawa kwa wote bila ubaguzi. Iwe katibaa itayotoa fursa kwa vyama vyote. Hii itasidia sana kwani wananchi wataweza kuwawajibisha vyama na viongozi wao kila uchaguzi unapokuja ila katiba ikiwa inabeba chama kimoja kinashinda hata wakikosea hatutokaa tukaendelea na haina picha nzurii. Ila ukiwa mzalendo wa kweli utaweka mwanya kwa wengine wenye uwezo wa kuendesha nchi.

12. Awe mzalendo na sio mchama kwani chama sio baba wala mama yake pale chama kinapokosea aweze kusema hapana kwa maslahi ya raia wa Tanzania.

13. Kuweza kuweka mfumo utaotoa fursa sawa kwa wote iwe masikini,tajiri, mlemavu, mwanamke, kijana, mwanaume. Tanzania ukimtoa mwalimu jk sioni kiongozi mwingine alietoa fursa sawa kwa wote kama yeye. Mtaani kuna viongozi wengi wazuri hawajapata fursa, kuna wanasayansi wazuri hawajapata fursa, kuna wachezaji wazuri hawajapata fursa kuna vipaji vingi sana vinavyoweza kusaidia nchi ila mfumo uliowekwa wa kujuana unalibomoa taifa kwa kupata wawakilishi wabovu, waatendaji wa bovu sanaa, viongozi wabovu sanaaa. Kuna sekta hawatumiii weledi kabisaaa wengi huko wamewekwa kiundugundugu hata wakiboronga inasafishwa. kwa mtindo huo atutafika kokote kulee. Tutumie talent au vipaji vinavyostahiliii hii itasaidia sanaa ila kwanza tutoe mfumo wa kujuana kwani utaleta madhara sanaa kwa taifa na jamii kiujumla mwisho wa siku. Mwalimu jk angeweza kuweka watoto wake, ndugu zake ila alipenda Tanzania kama nyumba au familia yake.

14, Awe mcha Mungu wa kweli.

15. Tanzania inawahitimu wachache sana wa vyuo vikuu walio na shahada na kuendelea. Tunamtaka kiongozi ataeweza kuwaondolea changamoto ya ajira kwani ni asilimia ndogo sanaa yani 10% haifiki ilaa wakoo mtaani. Kwanini wasifufue viwanda wakati kuna mainjinia waandisi hawana ajira, fani nyingi sanaaa ziko mtaani. Kuna sekta kama ya mambo ya ndani pia inahitaji sana wasomi kule. kwani kuna mambo mengine hayaitaji Nguvu ni akilii na mengine nguvu ila siku zote unaanza kwa kutumia akilii ndio ikishindikana nguvuu.

16. Aweze kuwawajibisha watendaji wake na kuwasimamia ipasavyoo ikiwa ni pamoja na kuweka sekta chache zile za muhimu kwa taifa.

MWISHO. Tanzania ni yetu sotee na kila mmoja anayohaki ya kufaidi matunda ya nchi ikiwa ni pamoja na kuishii kwa Amani na Upendo. Mungu ibariki Tanzania.

Kama tungekuwa na watu wenye mtazamo kama huu hata mia nchi ingebadirika
 
1.Sifa ya kwanza awe mtu anayekijua chama nje ndani kwakuwa mtu huyo atakuawa mwenyekiti mtarajiwa wa chama 2.Sifa ya pili Mch apakazi anayekubalika mpenda watu na anayependwa na watu 3. Sifa ya tatu Kupunguza ama kusetisha matumizi yote yasiyo ya lazima 4, Rafiki wa vijana anayezijua changamoto za vijana
 
Ccm wanahangaika bure sasa mwenye hizo ndani ya ccm ni nani?raisi atatoka nje ya ccm
 
Hizo sifa zimetajwa na Katibu mkuu wa hilo jumuiya Sixtus Mapunda-gazet mtanzania leo Ijumaa ukurasa wa tatu
 
Anayeweza kumaliza ufisadi hawakuiweka? kumbe mtoto wa nyoka ni nyoka tu, hawa mafisadi watarajiwa wana akili kweli?
 
mOD MMEUNGANISHA THREAD MBILI ZISIZO SHABIHIANA , HII YA UVCCM NI YA JUIA MADHUBUTI YA CHAMA KIKUBWA, HIYO YA AWALI NI YA MEMBER TU SI YA JUMUIYA MAHSUSI YA CHAMA SAMAHANI LAKINI HZIPASWI KUWA KAPU MOJA KUNA VITU VYA MSINGI MTU ANAPATA, NADHANI UMEZUIA WACHANGIAJI NAFASI
 
jamani watanzania wenzangu mngependa rais ajaye hawe na sifa gani? ni apiganie mambo gani hili kumuokoa mtanzania dhidi ya maisha magumu ya umasikini? karibuni
 
Asiwe mtu ambaye alisha tuhumiwa kwa ufisadi wa aina yeyote hapa Tanzania
 
Ndugu zangu watanzania,huu si wakati Wa ushabiki Wa kisiasa. Si wakati Wa kuwa Mayuda tunaokubali kuuza utanzania wetu kwa vipande vya fedha. Si wakati Wa kuiweka nchi yetu rehani kwa wezi na Magenge ya waharifu.

Kwa mantiki hiyo, tunamtaka Rais ajaye awe na sifa zifuatazo;
1. Mwanadiplomasia atakayeweza kubalance kati ya maslahi ya taifa na mahusiano ya kimataifa. Hatumtaki Rais dikteta, rais mkurupukaji Wa maamuzi kwa kudhani kuwa huo ndiyo urais. Dunia pamoja na siasa same zimebadilika hivyo tujifunze kwa wenzetu. Mabavu na pupa hayana nafasi katika dunia hii inayoongozwa na diplomasia na ujanja wa kucheza na akili za wakubwa ili kuliweka taifa upande salama. Hatutaki rais atakayetuvuruga!

2. Tunataka rais atakayekemea rushwa na kuongoza mapambano dhidi yake kwa vitendo.
3. Tunataka rais asiye na visasi maana atatucheleweshea maendeleo kutokana na kuchelewa kuhangaikia maadui.

4. Tunataka rais atakayetusemea kimataifa. Hivyo tunamtaka Mwenye uwezo Wa kuzungumza, siyo bubu!

5. Tunamtaka rais msikilizaji zaidi.

6. Tunamtaka rais atakayeendeleza "giance" ya taifa letu katika uwezo Wa kupatanisha migogoro ya mataifa mengine na si yule atakayejifungia ndani na kusema shauri yao majirani wetu!

7. Tunamtaka rais Mwenye mipango inayotekelezeka siyo mnafiki mridhisha watu kwa mambo ambayo yeye mwenyewe hajawahi hata kuyatekeleza kabla.

8. Tunamtaka rais Mpenda Amani.

9. Tunataka rais asiye na sura ya ukanda,udini, ukabila na urafiki na mafisadi.
10. Tunamtaka rais atakayeutambua na kuulinda utakatifu Wa Ikulu na hivyo NAE pia kuuishi utakatifu huo. Tunataka atakayetambua kuwa Ikulu ndiyo ofisi juu ya nchi na kuwa ndiyo kielelezo cha ustaarabu Wa watanzania na pia utawala bora na kimbilio la watanzania wote. Hatumtaki ambaye akishaapishwa tu ataalika mafisadi wenzie na kusherehekea kwa shampeni. Ikulu siyo kasino!. Si sehemu ya kupigia dili!
 
MJENGA,

..Dr.Sla/a na Tundu Lissu wanatosha ktk sifa hizo ulizoziorodhesha.
 
Last edited by a moderator:
Wako team Jk wanahamia team EL iki wapate u waziri na wengine wanakwenda team Ukawa na watapata uwaziri.
 
1. Aweze kuwaunganisha Watanzania

2. Aweze kubuni na kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania na kukuza kipato.

3. Aweze kubuni sera na kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana.

4. Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika

5. Aweze kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na matumizi ya Serikali.

6. Aweze kutumua fursa yetu ya kijiografia kibiashara.

7. Aweze kusimamia matumizi ya rasilimali .

Sifa zote hizi anazo Lowassa pekee. Twende na Lowassa 2015 mpaka magogoni, mpaka Ikulu
 
mkuu mbona hakuna sifa ya kuhakikisha kuna kuwa na uwajibikaji na uadilifu?
 
Back
Top Bottom