Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Ni kweli ni mzalendo mgawaji mzuri wa vitalu vya gesi! Hawa wazee wana maono kama ya wizi wa ng'ombe huko kwao maana wanasema ni kuchukuwa tu na siyo kuwa wameibiwa!

We ngo'mbe wewe amegawa vitalu wapi? Sisi wafuatiliaji wa mambo hatujawahi kusikia amegawa vitalu hovyo hovyo. kama wazee wa Serengeti walivyowasilisha kile wanachokiamini kwa mtu huyu, nyuma yake yupo wengi tunao support Muhongo agombee. Kama angekua kagawa vitalu hata wazee wanajua wasingesema waliyoyawasilisha.
 
We ngo'mbe wewe amegawa vitalu wapi? Sisi wafuatiliaji wa mambo hatujawahi kusikia amegawa vitalu hovyo hovyo. kama wazee wa Serengeti walivyowasilisha kile wanachokiamini kwa mtu huyu, nyuma yake yupo wengi tunao support Muhongo agombee. Kama angekua kagawa vitalu hata wazee wanajua wasingesema waliyoyawasilisha.

Asante Wazee wa Serengeti mmeona mbali. Hakika tunamwitaji Prof. Muhongo!:yo::yo::yo::yo::yo::yo::yo::yo::yo:
 
Tunalo tatizo la uongozi katika nchi yetu ya Tanzania.

Tatizo hili linatokana na viongozi kujipendekeza badala ya kupendekezwa na wananchi.

Leo tunashuhudia ombwe kubwa katika uongozi wa Taifa kwa sababu walioko sasa madarakani waliamua kujipendekeza wenyewe bila ridhaa ya wananchi walio wengi.

Tatizo la nchi yetu ni kuwa wananchi hawana msukumo wa kutaka kupendekeza aina ya mtu wanayetaka awe kiongozi wao.
Sasa kuelekea uchaguzi ujao natoa mapendekezo yafuatayo kuhusu Rais ajaye;

1. Awe ni Mtu ambaye hajaomba mwemyewe kuwa Rais.

2.Atokane na mapendekezo ya Wananchi
3. Awe na Maadili yanayokubalika.

4. Awe na maelezo yasiyo na Mashaka ya nini kinampeleka kutaka kuwa Rais wa Tanzania.

NB Ongeza Sifa nyingine unazoona zinahitajika kuelekea Urais 2015.

Tunahitaji kiongozi asiye na masihara na Taifa hili la sivyo tutaendelea kupata viongozi Walanguzi na Wahujumu uchumi wa Taifa letu.

Wanaojipendekeza na kuomba wenyewe wanajifahamu. Umemwona Muhongo kaomba mahali? Kizuri chajiuza bwana, hapo inaonesha wamemfuata wenyewe.
 
Nchi inahitaji Rais:
1. Muadilifu
2. Asiyefumbia macho uzembe na uvivu
3. Anayejali wanyonge hasa wa vijijini
4. Mkali asiyevumilia uvunjaji wa sheria
5. Mwenye maono ya Tanzania ya miaka 20-50 ijayo
- maono kuhusu AJIRA
- maono kuhusu NISHATI
- maono kuhusu ELIMU
- maono kuhusu ULINZI WA RASLIMALI ZETU, AMANI, UMOJA, NA MSHIKAMANO WETU
6. Anayechukia RUSHWA, WIZI na UBINAFSI.
7. Anayelinda HAKI ZA RAIA WOTE na MALI ZAO

Rais huyo ni Prof Muhongo.
 
muhongo yule prof. wa miamba ama mwengine?
kama yule tuache uvivu wa kuwaza yule jamaa anakiburi mno cha elimu yake...
 
Bila kujali atatoka kundi gani, upinzani au chama tawala nahitaji rais wangu ajaye awe na sifa zifuatazo
1: Awe na uchungu na rasilimali za taifa[ Hasa mafuta na ges ambavyo ndio kwanza mchakato unaendelea]
2:Atakayethamini taaluma za watu [walimu, ma daktari, ma injinia, wauguzi n.k]
3:Atakayeimarisha ulinzi na usalama wa nchi [ jeshi la chagonja, Mwamunyange safi]
4:Awe na mbinu na fikra mpya za kutoa ajira kwa kuanzisha viwanda vingi ikiwezekana kila mkoa [sio kuja na sera tena ya kutoa mikopo
ni bora mabilioni yaanzishe viwanda kwa ajili ya kuzalisha na kutoa ajira]
5:Atakayetilia mkazo suala la elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu sawa [ Mazingira ya shule za vijijini yaendane sawa na mazingira ya shule za mijini, kama ni madawati,vyoo, madarasa, ofisi, nyumba za walimu, maabara]
6:Atakayeimarisha huduma za afya kwa kujali maslahi ya wauguzi( hawa ndio hushinda na wagonjwa na magonjwa) maslahi ya madaktari
ili wasiwe na tamaa ya kufanya kazi hospital nyingi kwa wakati mmoja, kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa vinapatikana kila hospital kubwa za mikoa.
7:Rais atakayeimarisha bandari zetu tanga, dsm, mtwara [hizi tu zinatosha kuinua uchumi wa taifa]


Zipo nyingi ila kwa leo niishie hapo, unaweza kuongezea na za kwako hapo chini......
 
Kwa Tanzania Labda awe malaika,hakuna mwenye hizo sifa utasubiri sana
 
Ina maaa hata hawa chadema hawana mtu mwenye hizo sifa?? Kwa chama tawala hata mimi nina mashaka sababu sisiemu hii si ile aliyeiacha mwalimu.Hii imepoteza mwelekeo.

Kama tukiruhusu raia akitoka ashtakiwe Kama alimfanya ubadhirifu inawezekana Lakin kwa sasa haiwezekani ujue hivyo najua ukweli unauma
 
Kama tukiruhusu raia akitoka ashtakiwe Kama alimfanya ubadhirifu inawezekana Lakin kwa sasa haiwezekani ujue hivyo najua ukweli unauma
Tukisema ashtakiwe unadhani familia ya mfalme itapona? Haiponi ndio maana katiba ipo kimya juu ya hilo
 
Rais wa namna hiyo anaweza akapatikana,angalau akafanya au akatimiza hata nusu ya sifa hizo.

Issue ni "commitment" tu (ambayo hata wewe hauna!). cardiologue
 
Last edited by a moderator:
Rais wa namna hiyo anaweza akapatikana,angalau akafanya au akatimiza hata nusu ya sifa hizo.

Issue ni "commitment" tu (ambayo hata wewe hauna!). cardiologue
Umasikini wa watanzania unatokana na watanzania wenyewe kama wewe.KAMA UNAONA MWENYE SIFA HIZO ANAWEZA KUPATIKANA TUMPIGIE CHAPUO BASI.....akitoka cuf, sawa...chadema sawa, nccr sawa , tlp sawa ila kwa chama chetu tawala sidhani sababu mwalimu alivokwenda, alikwenda na chama chake kimebaki jina tu sasa....makada wooooooote wanaamini nguvu ya fedha ndiyo itakayowapeleka magogoni na wadanganyika bado wanawashadadia tu.Commitment ninayo kiongozi sema sijaitwa katika siasa bali ktk nyanja hii niliyonayo sasa
 
Re: Jina langu likikatwa nitamuunga mkono mh.wasira

Mada yako umeiweka vizuri sana na nimeipenda na ukweli sifa ya kwanza Rais wa awamu ya tano anatakiwa atoke upinzani na kura za serikali za mitaa zimeonesha wazi wimbi la mabadiliko , sasa tutashangaa kuona kama wapiga kura watahamia upande wa magamba club! Rais mpya mkali na mwenye ubavu wa kuwatupa jela majoka yote yenye makengeza kina Chenge , Betina nk, Rais atakaeziba mianya yote ya ufisadi serikali kuu na serikali za mitaa , rais mcha Mungu anaechukia ufisadi, Rais ataezuia ujangili na kuuzwa wanyama hai ili watalii waje nchini, rais ataezuia safari za mawaziri na bongo movie kula bata nje ya nchi, rais atakeleta elimu na afya bure kama enzi za Nyerere manake mabilioni yetu yapo uswisi na escrow , Rais atakaefufua reli zote na viwanda, Rais atakewezesha kupatika maji safi na salama na umeme wa bei nafuu, Rais atakaesaidia kushuka bei ya petrol, Rais atakajali walimu na madaktari na wafanyakazi wengineo, Rais atakaejenga uwanja mpya wa kiwango wa ndege kama Kenya, Rais atakaejenga barabara za juu kama Kenya na Uganda wasiojua zipo bongo no nginjera tu miaka hamsini sana ya umaskini hakuna kitu! viongozi kazi kuiba mali ya umma tu na kusomesha watoto wao nje ya nchi ndo wanachojua!

Kuna mda nimesoma thread flani ya gamba ilikuwa na list ya majina ya wagombea toka magamba club ila bahati mbaya sana yalikuwa majina yenye ukakasi aliyoweka na a nikashangaa eti sikuona jina hata moja la mgombea mwenye sifa ya kuwa Rais wa nchi tajiri inayofilisiwa na magamba, nchi ya kusadikika ya Danganyika! Rais gani anaweza kutoka magamba club? Rais atakeendeleza uongozi wa nchi ambayo raia wake walio wengi wamenyimwa elimu sahihi ya uraia kwa maana hawajui kuwa kulala na njaa au kuugua na kukosa matibabu ni kosa la serikali , hawajui kuwa kura ni mkataba na serikali wa kupata hali bora ya maisha kwa watu na kama serikali haiwezi kuleta hali bora inatakiwa iwapishe wengine au mwananchi kuchagua serikali toka chama kingine , hivi ndivyo ulaya na marekani wameendelea , serikali ikishindwa kuwapa wananchi hali bora inapigwa chini kwenye uchaguzi mkuu! hii inaitwa SOCIAL CONTRACT THEORY, pale Mlimani wanafundisha vizuri sana. Hata raia unapokosa kazi si kwa uzembe unatakiwa kulipwa unemployment benefit na Tanzania imesaini mkataba huo wa kuondoa njaa na magonjwa na tatizo la ajira kwa raia wake na kukubali jukumu la kuwasaidia raia wake wote wenye shida na njaa na magonjwa, mwaka 2002 huko Geneva, hiyo inaitwa SOCIAL PROTECTION FLOORS na wananchi hawana habari hiyo, hawajaambiwa na serikali yao hadi leo kuhusu huo mkataba uliosainiwa na serikali yao kuwapa hali bora na kuwanasua na umaskini wa kutupa!

System ya uendeshaji wa nchi ya Tanzania sasa imeoza, nchi inanuka kwa ufisadi , kuonea raia, rushwa na umaskini uliokithiri, umaskini unaowatesa watu wake millioni 47 wanaokufa kwa njaa na magonjwa , raia wasio na elimu wala ajira huku majoka machache yenye makengengeza kina
Chenge , Anna Tibaijuka , Werema ( na wengineo wote wanajijua na Mungu anawangoja wafe awachome moto mkali) , wakijilimbikizia mabilioni ya mali ya umma kwenye akaunti zao na kuleta shida kubwa sana kwa raia wa kawaida ya kupata pesa manake haya majoka yenye makengeza na sumu kali yamezitoa pesa kwenye mzunguko wake!pesa ambazo zingepita mahospitalini, kwa mama ntilie, deiwaka, mashuleni, madukani, serikali za mitaa, wizarani nk na kila raia angeambulia japo kidogo ila watemi kina Chenge wamezikwapua zote bila huruma!jamani mtu ana familia ya watoto watatu wazee kama yeye na mke anakwapua millioni elfu nne na mia sita (1.6B) zote anapeleka wapi kama si ulafi na ushetani tu? wanakwapua mabilioni wasiyoyahitaji katika maisha yao ya kila siku, na cha ajabu sana mabilioni wasiyoyatumia!

Ikumbukwe kuwa umaskini wa Tanzania ni wa kujitakia na unasababishwa na mashetani wachache wenye maumbo ya binadamu, mashetani wenye nyadhifa mbali mbali serikali kuu na serikali za mitaa!. ni ajabu sana wadanganyika wana macho na hawaoni jinsi nchi yao inavyoliwa na mafisadi , waziri anakuja kwenye mkutano wa kampeni na TOYOTA LANDCRUISER GX six cylinder iliyotokana na kodi ambazo ni majasho ya walalahoi manake matajiri wanasamehewa kodi bongo, gari inakunywa mafuta kwa siku moja ni bajeti ya mlalahoi kwa mwaka na wanawatimulia vumbi raia waliokaa juani eti kuwasikiliza huku wakisikia njaa kwa kukosa chakula na waliovaa nguo zina viraka na eti wengine wana sugu kwa kuhangaika na jembe la mkono miaka nenda miaka rudi hadi alama za dole gumba zimefutika ila bado masikini hawa wanachagua hawa matajiri kuwaongoza, hivi watu wasiojua njaa inavyouma watakusaidiaje? hivi raia hamjui kuwa foleni ya Dar ni ya kutengeneza ili raia wasi discuss mambo ya maendeleo manake muda wote watu wa Dar wana discuss foleni na kuwaza foleni, eti mtu anaamka saa kumi kukwepa foleni isimkute eti atachelewa kibaruani na huu miungu watu viongozi wetu wakiwa na safari , piki piki ya usalama inapita kuyaamuru magari yakae pembeni wenye nchi wapite , unadhani hao wanaopita na misafara yao wasiojua adha ya foleni wataondoaje foleni?! jamani amkeni miaka hamsini ya umaskini haitoshi tu!

Wakati huo huo Tanzania ni nchi iliyojaa udikteta uliojificha katika kichaka cha demokrasia iliyoishia kwenye makaratasi manake walalahoi wanaojaribu ku exercise demokrasia wanatekwa na kuteswa, na huku vyombo vyenye jukumu la kulinda usalama navyo vinawapiga watu ovyo, vinaua na kuleta vilema kwa raia wasio na hatia , watu wanaoandamana kudai haki zao za kikatiba! bongo ni nchi ya ajabu sana! viongozi na matajiri wako juu ya sheria , akili zangu zinaniambia wafungwa wengi Tanzania wanafungwa kwa kuonewa tu , kwa kuwa kina Chenge wameiba pesa zote za umma na wananchi wanakosa elimu na huduma za afya na matokeo yake hawana ajira wanaishia kukaba na kuiba na kukamatwa na kufungwa manake wanasikia njaa na hawana namna ya kupata chakula na nguo kihalali kama Panya Road, ikumbukwe sitetei uhalifu kamwe!
Magereza zimejaa masikini tu! nawapa pole sana, hata sisi tunaopiga cargo na deiwaka ughaibuni nawaambia ukweli wangu ni effects za kina Chenge pia , manake tumesota sana bongo miaka nenda rudi, tukaanza kuzeekea kwenye umaskini, tumelala na njaa na kukosa matibabu na nguo, tulipopata upenyo bila kuwaza mara mbili mbili tukakimbilia nje!!na wengi wetu hatupendi kabisa kurudi bongo kuona tena nyuso mbaya kabisa za kina Chenge!

Jamani Chenge ni mfano mbaya sana kuwahi kutokea katika historia ya jamii ya Tanzania, ni mfano mbaya sana kwa watoto wa Tanzania. Huyu nyoka mwenye makengeza na sumu kalai anafaa kufundishwa shuleni kama mfano wa raia wahujumu uchumi na vyanzo vya umaskini na uhalifu Tanzania. Chenge ni nyoka mwenye makengeza na sumu kali inayoua raia wa Tanzania , nyoka mbabe alie mstari wa mbele kupeperusha bendera ya ufisadi huku wenzake wakimfuata kwa shangwe nyuma yake. Ndio, yeye na wenzake wote katika chama wanapigana vikumbo kufilisi mali ya wavuja jasho, walalahoi wanaokamuliwa kodi huku matajiri wakipewa misamaha ya kodi.

Chenge na genge lake la majoka yenye makengeza na sumu kali yalio madarakani na yale yaliostaafu tangu uhuru yanaishi kifahari masaki kwa kutumia mali ya umma ambayo ni majasho ya walalahoi wa Tanzania, nani anabisha? Chenge ameonesha wazi stage tuliyofika katika nchi ambapo sasa watawala wetu wako juu ya sheria! mtu ni mwizi wa dhahiri na anagoma kuhojiwa na hafanywi kitu , japo tukumbuke most of viongozi wa Tanzania ni mafisadi na kama huamini taja jina moja lolote na waambie TAKUKURU NA CAG wamkague na utayopata iwe siri yako! Maskini nchi tajiri ya Tanzania iliyojaa rasilimali lukuki imepata bahati mbaya sana kuwa na viongozi mashetani, wezi, walafi, wabinafsi , wasiomjua mungu na madhalimu wakubwa wasiojali mateso wanayopata raia wake. Wananchi shime shime tupigie kura upinzani kwenye uchaguzi mkuu kuyaondoa madarakani majoka haya yenye makengeza na sumu kali inayotuua! gamba mmoja tu akisoma hii comment , i will be extremely happy! . Tanzania bila magamba inawezekana , tumeanza kuona uchaguzi serikali za mitaa!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ninakuomba tuondolee mafisadi katika uongozi wa nchi ya Tanzania, Amen
inauma kwa kweli ila yote yana mwisho kiongozi, hawa nyoka wenye makengeza dawa yao kuomba wapigwe upofu tu.
 
Binafsi rais ajaye afanye yafuatayo! 1. Asishabikie sana wawekezaji wa nje, ahamasishe wawekezaji wa ndani, ili kukuza uchumi wetu. 2. Asiwe mtetea maovu kama rushwa, ubadhilifu na hata ufisadi, apambane na hayo bila kificho na kwa msimamo thabiti hata kama rafiki zake wanahusika kwenye hayo! 3. Asiye wa kushabikia na kutegemea sana misaada ya wahisani na mikopo ya taasisi za fedha za kimataifa, ajenge misingi ya taifa kujitegemea na sio kutegemea wafadhili. 4. Awe mpenda demokrasia ya kweli na sio kinadharia tu! 5. Asiwe mbaguzi kwa raia wake katika kuwaletea maendeleo kwa misingi ya dini, kabila, rangi, kanda atokako mtu, itikadi ya kisiasa na mengineyo. 5. Awe ni mtu anayelipenda taifa letu kwa moyo wake wote bila chembe ya mashaka machoni kwa watanzania wenzake.
 
Umasikini wa watanzania unatokana na watanzania wenyewe kama wewe.KAMA UNAONA MWENYE SIFA HIZO ANAWEZA KUPATIKANA TUMPIGIE CHAPUO BASI.....akitoka cuf, sawa...chadema sawa, nccr sawa , tlp sawa ila kwa chama chetu tawala sidhani sababu mwalimu alivokwenda, alikwenda na chama chake kimebaki jina tu sasa....makada wooooooote wanaamini nguvu ya fedha ndiyo itakayowapeleka magogoni na wadanganyika bado wanawashadadia tu.Commitment ninayo kiongozi sema sijaitwa katika siasa bali ktk nyanja hii niliyonayo sasa

Teh! Si lazima uitwe kwenye Siasa tu ndo uifanyie jamii kitu flan. Kumbuka, asiyekuwa mwaminifu kwa mambo madogo, hawez kuwa mwaminjfu kwa mambo makubwa.

Begin it right there and people will see & call you to politicize your good charity & patriotism in their community & Nation.

Now; kwa upande wangu namwona MIZENGO-PINDA anaweza akayafanya hayo(walau kwa kias kikubwa sana kuliko yeyote ninayemjua ndani ya CCM au UKAWA.

Together?
 
Teh! Si lazima uitwe kwenye Siasa tu ndo uifanyie jamii kitu flan. Kumbuka, asiyekuwa mwaminifu kwa mambo madogo, hawez kuwa mwaminjfu kwa mambo makubwa.

Begin it right there and people will see & call you to politicize your good charity & patriotism in their community & Nation.

Now; kwa upande wangu namwona MIZENGO-PINDA anaweza akayafanya hayo(walau kwa kias kikubwa sana kuliko yeyote ninayemjua ndani ya CCM au UKAWA.

Together?
EEEEEÉH, pinda huyu huyu ambaye tumeshudià tembo wanauwa, twiga wanatoroshwa ndani ya uongozi wake??
Yani pinda huyu huyu anayeshudia madili ya pesa ndefu yakipigwa ndani ya uongozi wake na yuko kimya??
Pinda huyu huyu aliyesema si za umma?? Pinda huyhuyu anayeshudia albino wakiuawa na yuko kimya?? Yani pinda huyuhuyu anayeona raia
wanapigwa tuuuuuuuu na polisi, au kwa sababu alisema wapigwe? Pinda huyu huyu tumeshudia migomo ya madaktari, walimu ndani ya uongozi wake, leo aende magogoni?? Kweli jamani??? NI PINDA HUYU HUYU AU YUPO MWINGINE? kama ni huyu hapana, mimi si rais wangu.
 
Wapendwa wana JF
Nachelea kusema Vyama vya siasa vina sera Nzuri sana ila havipati wasimamizi Imara, wengi huwa na maneno meeengi bila Vitendo.
Naomba anayependa atoe sifa tatu tu ambazo anafikiri Rais mtarajiwa akiwa nazo atatufaa;
Mimi na kuwa wa kwanza
1. Nahitaji Rais atakaweza kusimamia Uchumi na hivyo kuongeza Ajira
2. Rais atakayeweza kuhakikisha kuwa Rasilimali za za Taifa zinawanufaisha watanzania -kwa vitendo sio kwa maneno.
(mfano, wanaoiba au kusaini mikataba feki, wafilisiwe pamoja na kufungwa.
3. Awe na uwezo wa kutolea maamuzi kwa haraka hata kama yatakuwa na ukakakasi kidogo ila yanalenga kuwa na manufaa makubwa kwa taifa. mf. Kama waziri ha perform ni kumtoa sio kusubiri hadi kuvunja baraza?


Angalizo:
Tusitarajie kupata Rais ambaye ni Malaika kutoka mbinguni, Rais atakuwa ni binadam wa kawaida ambaye anaweza kuwa pengine na mapungufu katika utendaji wake huko nyuma; mimi nahisi ni kawaida kwani nafuatilia sana siasa za kimataifa na nimeona Nchi nyingi za wenzetu hata za Ulimwengu wa kwanza (we learn through mistakes). Cha msingi ni; atalifanyia nini Taifa letu!
Kumbuka; Rais mzee, Rais Kijana au Rais mwanamke haitusaidii chochote; Tunataka Rais mwenye uwezo!!!
 
Back
Top Bottom