Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

[QUOTE=suzan lema. Ni nchi ya wasofikiri vizur na walologwa ndo wanaona kuwa uadilifu si kigezo cha rais ajaye.
 
Tunataka watanzania wajue,ni rais mwadilifu tu ndiye tunae mhitaji.umasikini wetu ni tunda la ufisadi na rushwa.
 
Sifa kuu ya kwanza kabisa na hili ni muhimu kuliko sifa zote za rais ajaye...

"ASIWE AMETOKA CCM....."
 
Dr Slaa ndio mtu sahihi.. Kwa wakati sahihi, kwa rais sahihi ndio yeye.. Wengine wachovu.. Na mbwembwe kibao...
 
Siku zote uadilifu si kigezo cha mwanasiasa yeyote yule hapa Duniani
Nenda ukapimwe akili.halafu nafikiri hapa JF kungewekwa standard za watoa hoja za kujadili maana sidhani kama unaelewa ulichokiandika.
 
Hayo ndio maswala muhimu ambayo alituahidi jana tunduma rais wa awamu ya tano dr slaa
 
Katika za Karibuni limezuka kundi kubwa sana la Watangaza nia wa Nafasi ya Uraisi katika mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Taifa hili ambao unatarajiwa Kufanyika October Mwaka Huu.... Lakini kitu kimoja cha msingi ambacho tunapaswa kujiuliza sisi Watanzania kama Raia wa Nchi hii wenye Dhamana ya kuhakikisha tunalilinda Taifa letu kutoka mikononi mwa Wanasiasa Maharamia ambao wanaitafuta Ikulu kwa Uchu usio na kifani wakiwa na lengo moja kubwa la kutunisha mifuko na kushibisha matumbo yao kwa kutumia Rasilimali za Taifa hili na watu wake kifisadi, ni kuwa je Mpaka sasa kati ya watangaza nia walioishakwisha Kujipambanua mbele ya Umma wa Watanzania ni Yupi ambae anastahili kuliongoza Taifa Hili? Na Je ni sifa zipi ambazo tunazihitaji toka kwa Rais ajaye wa Awamu ya 5?Manaake tusipokuwa Makini tutaendelea Kulia na Kusaga Meno kwa miaka mingine kumi kutoka sasa (2015-2025)....Fanya Uamuzi Sahihi kwa Manufaa ya Taifa hili kwa Kizazi cha Sasa na Kwa Vizazi vijavyo...AMKA MTANZANIA.
 
Habari WanaJF,

Idadi ya watangaza nia ya kugombea urais inazidi kuongezeka siku hadi siku na ndipo ninapojiuliza ikulu kuna nini mpaka kila mmoja atake kwenda?

Sasa ngoja nijikite kwenye mada yenyewe: tegemeo la watanzania kwa maoni yangu ni kuwa na rais mwenye sifa zifuatazo:

1.Mcha Mungu; Ni Lazima Awe Mtu Mwenye Hofu Ya Mungu.

2.Mpenda Haki; Haki Ndio Msingi Wa Amani Katika Taifa Lolote Lile.

3.Asie Na Kisasi; Katika Hili Ni Vizuri Rais Ajaye Asiwe Na Hali Ya Kutaka Kulipiza Visasi Kwa Wale Waliokuwa Wanampinga Wakati Wa Harakati Zake Kwani Hili Linaweza Kusababisha Uhasama Mkubwa Mara Baada Ya Uchaguzi Na Kusababisha Machafuko

4. Awe Na Uwezo Mkubwa Wa Kuongoza; Naomba Nisisitize Sana Katika Hii, Ni Dhahili Kwamba Nchi Yetu Inazidi Kuwa Na Changamoto Nyingi Sana Za Kiungozi Hivyo Ni Lazima Raisi Ajaye Awe Na Uwezo Mkubwa Wa Kupambanua Masuala Mbalimbali.

5.Achukie Na Kuogopa Sana Rushwa; Ruswa Ni Adui Wa Haki Hivyo Rais Ajaye Asiwe Hata Anayehisiwa Tu Na Rushwa
 
Ndugu wana jamvi, kuna baadhi ya watia nia ya kugombea Urais wamekuwa na kauli za kushangaza. Mtoa nia anasema mambo mengi atakayoyafanya halafu anaongeza "....nitaanzia pale alipoishia Rais Kikwete....". Offcourse ni lazima utaanzia pale alipoishia JK, lakini maana wanayoibeba ni kuendeleza yale yaliyofanywa na JK. Kwakweli watia nia wote wa namna hii HAWATUFAI. Yeyote anaesema ataanzia pale alipoishia JK akatafute shuguli ya kufanya. Ukisema utaanzia alipoishia JK maana yake yale madudu na mauvundo aliyokuwa ameyafanya JK upo likely kuyafanya tena. Nimemsikia
Titus Kamani, Wassira na kama sijakosea na Mwigulu. Kwa hapa awamu ya nne ilipotufikisha tunataka mtu wa kuanza upya na sio wa kuendeleza yalipoishia ya awamu ya 4 ambayo yemetuchosha na kutuchefua wengi wetu.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom