Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Katuni+Feb+2.jpg
 
Si mgambo wote wa jiji hawana uwezo wa kufanya ya maana, na hata hivyo wanachotimiza hao mgambo ni amri ya seikali chini ya uongozi kutoka Ikulu, kwa hiyo mgambo anatimiza kilichoamuliwa ikulu.
 
Si mgambo wote wa jiji hawana uwezo wa kufanya ya maana, na hata hivyo wanachotimiza hao mgambo ni amri ya seikali chini ya uongozi kutoka Ikulu, kwa hiyo mgambo anatimiza kilichoamuliwa ikulu.

wewe unavyomuona lowasa ana akili za kutosha kuongoza nchi?Mimi huyu jamaa namuona kilaza kabisa.
 
wewe unavyomuona lowasa ana akili za kutosha kuongoza nchi?Mimi huyu jamaa namuona kilaza kabisa.

Nilimuona Kikwete anafaa sana kuongoza nchi, lakini aliyoyafanya ni kinyume na matarajio, Ya Lowasa anafaa sana tu, mengi kayafanya na anaamini ktk maamuzi yake si kigeugeu kama Kikwete.
 
Mzee Kingunge Mda mfupi uliopita kwenye Kipindi Cha Baragumu cha Channel Ten:

Mwandishi: Mzee nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania?
Mzee Kingunge: Ni yule ambaye Wananchi wengi wa Tanzania wanamtaka
Mwandishi: Je unaonaje watu wanaojitokeza kutaka Urais kwa wingi?

Mzee Kingunge: Lazima watu waelewe kuwa Urais ni taasisi kubwa ,mimi nashangaa kila mtu anataka
Urais,wanasambabisha urais kuonekana ni taasisi ndogo ambayo kila mtu anaweza kitu ambacho sio kweli.

Mwandishi: Je wewe utampigia nani kura ya Urais?

Mzee Kingunge: Kura ni Siri,lakini nitampigia yule ambaye Watanzania wengi wanamuona anafaa kuwaongoza.

Mwandishi: Je namna gani Rais huyu umtakaye atapatikana

Mzee Kingunge: Watu wacache waache ubinafsi wa upatikanaji wa Rais,Wananchi wasikilizwe na mimi nina uhakika Rais atatokana na Wananchi
 
Nilimuona Kikwete anafaa sana kuongoza nchi, lakini aliyoyafanya ni kinyume na matarajio, Ya Lowasa anafaa sana tu, mengi kayafanya na anaamini ktk maamuzi yake si kigeugeu kama Kikwete.
Kosa mlilofanya kwa kikwete mnataka kurudia kwa lowasa.Kila la heri
 
Kosa mlilofanya kwa kikwete mnataka kurudia kwa lowasa.Kila la heri

Huwezi wafananisha, mazingira tu hayaruhusu, Mtu aliekulia kanda ya pwani na mtu aliekulia kaskazini ni tofauti ktk utafutaji na matamanio ya kimaendelo, kama unaridhika kula mlo mmoja na mtoto asiende shule achezwe, huwezi fananisha malengo ya mtu anaetaka kula milo 3 na mtoto asome mpaka elimu ya juu, maono yao tofauti.
 
Ndugu watanzania acheni kupotoshwa maana huu mwaka kuna watu watakufa kwa pressure pale majina yao yatakapo kwatwa, kama alivyo kwisha wahi kusema Mh Kikwete Kuhusu swala la rais ajaye alisema watanzania wasubirie kumpata rais mwenye sifa zote tajwa ktk chama. hizi kelele hakuna mtu yeyote atajibu maana baraza la taifa la usalam wameapa kufanya kazi hii ktk usiri mkubwa sana sana hivyo watanzania someni alama za nyakati magazeti na vyombo vya habari acheni njaa kusema mambo yanayo leta hofu kwa taifa maana Rais ajaye ni siri nzit na atakaye teguwa kitendawili hiko ni Rais wa sasa siku ikifika

Yaani unamaanisha rais ajaye atateuliwa na rais aliyepo madarakani?
 
We ngo'mbe wewe amegawa vitalu wapi? Sisi wafuatiliaji wa mambo hatujawahi kusikia amegawa vitalu hovyo hovyo. kama wazee wa Serengeti walivyowasilisha kile wanachokiamini kwa mtu huyu, nyuma yake yupo wengi tunao support Muhongo agombee. Kama angekua kagawa vitalu hata wazee wanajua wasingesema waliyoyawasilisha.

Kampitishe NEC kwanza ndo uje humu kumpigia debe.
 
Huwezi wafananisha, mazingira tu hayaruhusu, Mtu aliekulia kanda ya pwani na mtu aliekulia kaskazini ni tofauti ktk utafutaji na matamanio ya kimaendelo, kama unaridhika kula mlo mmoja na mtoto asiende shule achezwe, huwezi fananisha malengo ya mtu anaetaka kula milo 3 na mtoto asome mpaka elimu ya juu, maono yao tofauti.

hoja dhaifu sana dada yangu.
 
Ni maneno ya mchambuzi wa mambo ya siasa leo asubuhi katika clouds fm radio,kuwa watanzania ni wakati sasa wa kupima viongozi wanaotaka kutuongoza kwa kuwafaamu vizuri juu ya UWEZO WA KUCHAPA KAZI,UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU INAPOBIDI,WEREDI WA MAMBO.na HASIYE MPENDA RUSHWA NA UZEMBE KAZINI,PIA YUKO TAYARI KUWATUMIKIA WATANZANIA.Tuachane na siasa za vyama maana hazisaidi na tuwape nafasi watu ambao tunahakika na uwezo wao na sio siasa za majukwaani maana hazina tija wala dira kwa taifa letu bali mtu mmojamoja tukimpima kwa uwezo wake tunaweza kupata kiongozi bora.
Kwa maana hiyo mimi nimewachambua baadhi na ni yupi kati yao anatufaa kwa uwezo wake kama Rais wetu ajaye.

1, MWAKYEMBE
2 LIPUMBA
3, MAGUFULI
4, SLAA
5, LOWASA
6, Jaji RAMADHAINI
Wanajf nini anaye​tufaa kuwa Rais wetu ajaye?
 
1. asiende kwenye nyumba za ibada kushawishi apewe kura.

2. asiseme atajenga bara bara na kudumisha afya kwani ni wajibu wa serikali kutenda izo kazi na awatumii pesa yao bali ni kodi za wananchi.. sitoi kura ukija na sera za dizaini hii.

3. tunamtaka raisi ataeinua uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na kutoa vipaumbele kwa elimu, kilimo na viwanda. kwanini? hii itasaidia sana kwa vijana wengi kupata ajira, wakulima kuuza bidhaa zao kwa viwanda vya ndanii. Itasaidia kuinua uchumi wa nchi sana kwa kuuza bidhaa za viwandani ndani na nje ya nchi pia wakulima watauza bidhaa na kupata soko nje na ndani. na watanzania wengi watapata ajira.

4. Asiingize siasa kila sekta mfano mzuri ni sekta ya elimu.. Hii sio sekta ya kufanya mambo ya mzaa kama kufaulisha wanafunzi ili upate kura. Watoto hawajui kusoma wanaenda form one.. Hii italeta madhara kwa nchi sanaa kwani kuna ushindani wa kidunia katika ajira sio ajabu kwa mtanzania kuajiriwa marekani, kenya na popote pale. Ila ukiwa na wajinga wenye vyeti vya ufaulu mzuri madhara yake ni makubwa sana ndani ya taifa ndio yalee tunayoyaona kwa baadhi ya vijana, waheshimiwa flani waliokosa uadilifu. Ili taifa liendelee inabidi kuwe na watendaji wenye upeo. Hata ukishinda kwa kufaulisha watu wewe na familia yako mtapata neema ila Tanzania jee?

5. Raisi awe mjasiri asiye yumbishwa, mzalendo ataeweza kuondoa mfumo ulioko sasa wa kujuana ndio ufanikiwe natoa mifano kidogoo katika soko la ajira uwezi kupata mpaka ujue mtu. pili kwa sasa Tanzania kila kitu mpaka uwe mtoto wa mkubwa ndio ufanikiwe hii imeonekana sanaa sehemu nyingi hata katika shindano la miss tz ambae kafoji vyetii sio hukoo tuu ila wenzangu na mimi tukifojii ndio sheria inafanya kazi.. Hatutaki rais ataeendeleza huo upuuzi kila mmoja awe chini ya sheria.

6. rais mwenye msimamo hasa katika maamuzi yake yakiutawalaa... Kazi ya uraisi ni kazi yenye changamoto kubwa sanaa inabidi uweledi wa hali ya juu sana.. Tunamtaka kiongozi asiekata tamaa akipata changamoto za kiutawala kiasi cha kukimbia madarakani. Viongozi wengi walioachia ngazi baada ya kutoa maamuzii yasiyo na weledi na kuachia ngazi hawafai kabisa kwani atafanya jambo kwa taifa na kukimbia nchi.

7. asiwe na skendo zozote za wizi, ufisadi, uroho wa madaraka, mbinafsi, kinyongo, awe mpenda haki na anaesimamia sheria.

8. afanye mambo kwa maslahi ya taifa na sio kwa ajili ya chama chake sio kiongozi ataewaondoa madarakani wabunge wa chama chake baada ya kuboronga kwa maslahi ya chama bali kwa ajili ya taifa. Na kiongozi akipatikana na kosa lolote mfano la wizii achukuliwe hatua kali ikiwa pamoja na kufungwa kama anastahili.. Sio kusema fedha zirejeshwe na kujiuzulu hapana.. Kwani uraiani ukiiba kuku raia awakwambiii urudishe utafungwa au kuuliwa. Watu woteeee tuwe chini ya sheria na kuwajibika kutokana na matendo yetu.

9. awe na upeo mpana wa kukabiliana na changamoto za kiutalawa, asikie kilio cha wananchi, aweze kushughulikia mambo. Sio kiongozi unaulizwa kwanini nchi yako haina umeme unasema sijui au mimi sio Mungu. Wakati kuna vyanzo vingi vya umeme mfanoo makaa ya mawe, uranium, sio kutegemea umeme wa majii tuu.

10. Tanzania ni nchi yenye mali nyingi sanaa ikiwamo madini, milima,maji,bahari, mbuga za wanyama na vituo vingi vya kitalii n.k japo ni nchi masikini sana. Tunamtaka kiongozi ataeweka sera nzuri zinazotekelezeka ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ya kuzilinda na kuziifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tuipende nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwafikiria wataokuja baada ya kizazi hiki wasikute mashimoo tuu, tembo hakuna, vifaru hakuna wataishi maisha magumu sana kwa ajili ya mababu zao sio jambo jema. Kiongozi bora ni yule anaetaka taifa liwe imara hata baada ya yeye kutoka madarakani.

11. Asimamie katiba iwe katiba itayotoa haki sawa kwa wote bila ubaguzi. Iwe katibaa itayotoa fursa kwa vyama vyote. Hii itasidia sana kwani wananchi wataweza kuwawajibisha vyama na viongozi wao kila uchaguzi unapokuja ila katiba ikiwa inabeba chama kimoja kinashinda hata wakikosea hatutokaa tukaendelea na haina picha nzurii. Ila ukiwa mzalendo wa kweli utaweka mwanya kwa wengine wenye uwezo wa kuendesha nchi.

12. Awe mzalendo na sio mchama kwani chama sio baba wala mama yake pale chama kinapokosea aweze kusema hapana kwa maslahi ya raia wa Tanzania.

13. Kuweza kuweka mfumo utaotoa fursa sawa kwa wote iwe masikini,tajiri, mlemavu, mwanamke, kijana, mwanaume. Tanzania ukimtoa mwalimu jk sioni kiongozi mwingine alietoa fursa sawa kwa wote kama yeye. Mtaani kuna viongozi wengi wazuri hawajapata fursa, kuna wanasayansi wazuri hawajapata fursa, kuna wachezaji wazuri hawajapata fursa kuna vipaji vingi sana vinavyoweza kusaidia nchi ila mfumo uliowekwa wa kujuana unalibomoa taifa kwa kupata wawakilishi wabovu, waatendaji wa bovu sanaa, viongozi wabovu sanaaa. Kuna sekta hawatumiii weledi kabisaaa wengi huko wamewekwa kiundugundugu hata wakiboronga inasafishwa. kwa mtindo huo atutafika kokote kulee. Tutumie talent au vipaji vinavyostahiliii hii itasaidia sanaa ila kwanza tutoe mfumo wa kujuana kwani utaleta madhara sanaa kwa taifa na jamii kiujumla mwisho wa siku. Mwalimu jk angeweza kuweka watoto wake, ndugu zake ila alipenda Tanzania kama nyumba au familia yake.

14, Awe mcha Mungu wa kweli.

15. Tanzania inawahitimu wachache sana wa vyuo vikuu walio na shahada na kuendelea. Tunamtaka kiongozi ataeweza kuwaondolea changamoto ya ajira kwani ni asilimia ndogo sanaa yani 10% haifiki ilaa wakoo mtaani. Kwanini wasifufue viwanda wakati kuna mainjinia waandisi hawana ajira, fani nyingi sanaaa ziko mtaani. Kuna sekta kama ya mambo ya ndani pia inahitaji sana wasomi kule. kwani kuna mambo mengine hayaitaji Nguvu ni akilii na mengine nguvu ila siku zote unaanza kwa kutumia akilii ndio ikishindikana nguvuu.

16. Aweze kuwawajibisha watendaji wake na kuwasimamia ipasavyoo ikiwa ni pamoja na kuweka sekta chache zile za muhimu kwa taifa.

MWISHO. Tanzania ni yetu sotee na kila mmoja anayohaki ya kufaidi matunda ya nchi ikiwa ni pamoja na kuishii kwa Amani na Upendo. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom