Rais aapisha tume ya Katiba!

Hongera JK kwa kuanza kutimiza ahadi kuwa kabla ya kuachia madaraka; utahakikisha watz umewaachia zawadi ya KATIBA NCHI
 
chadema walipogoma na kutoka nje wakati mswada upo bungeni watanzania waliwatukana na kuwasema
lakini mchakato mzima tayari ulishakwenda ndivyo sivyo toka awali.
haya mswada kuapitishwa sasa wanaapishwa tuwaangalie watakavyofanya kazi wakienda ovyo naamini wawalikishi wa kweli wa tanzania na wananchi kwa ujumla wetu tusimame kidete kupinga yale mabaya yatakayojiri kwa hili tuwe makini na uwoga tutoe.
kwa sasa tuiache na kuona hiyo tume ianze kazi.halafu tuhakiki na kuchambua utendaji wake
 
Wa Tanganyika msilalame kwani bado kuna nafasi ya kuipinga rasimu hiyo ya katiba kama mtaona haiwafai kupitia katika kura ya maoni.

Nawasihi muwe na subra ikiwa pamoja na kuipa Pumzi na ushirikiano Tume hiyo ili iweze kufanya kazi zake vizuri.

Mkuu umerudi bila hodi? Vipi uchaguzi wa Arumeru umeuonaje? Kulikuwa na udini kama wa Igunga na Uzini? Tupe hekma zako mkuu.
 
na watu walikurupuka siku ya kwanza na kupongeza uteuzi wa tume....nilipinga kwa vigezo nikatukanwa,leo hii kuna watu waliochangia ile thread ya kwanza kabisa Rais alipotangaza majina leo wamepiga U-Turn

Hii ni dalili ya kuwa taiafa la mkumbo na fuata upepo
 
Wa Tanganyika msilalame kwani bado kuna nafasi ya kuipinga rasimu hiyo ya katiba kama mtaona haiwafai kupitia katika kura ya maoni.

Nawasihi muwe na subra ikiwa pamoja na kuipa Pumzi na ushirikiano Tume hiyo ili iweze kufanya kazi zake vizuri.
Wewe unaona itafanya kazi nzuri?

Mkuu unaongea kama "nyie" ndo mnatuletea katiba lol!

Haya bana, ngoja tusubiri kama wataitumia hiyo "rasimu" kupinga.
 
Hawa watu hawaeleweki walitangaza tena kwenye vyombo vya habari kuwa amehairisha kuwapisha leo ijumaa mpaka Jumatatu sasa imekuwaje tena
 
kuapishwa ndo kunafungua milango ya yale tunayotarajia kuyaweka katika katiba tunayoitaka sisi waTz, cha msingi tuwape ushirikiano ili tufike pale tunapotaka na kwa hakika inawezekana [waTz sote tuwe kitu kimoja]
 
Back
Top Bottom