Raila odinga katoboa jipu, watanzania tuamke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raila odinga katoboa jipu, watanzania tuamke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ras Cutty, Nov 23, 2010.

 1. Ras Cutty

  Ras Cutty Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mhe waziri Mkuu wa \kenya RAILA ODINGA Jana ametupasha na kutufungua macho watanzania woooteee wakati akiwa Mwanza. Najua wana JF woote wenye nia njema na Tanzania ya leo tutakuwa tunaungana na hoja yake kwamba "SUALA LA KATIBA MPYA NI SHAURI YETU WENYEWE". Hapo ametuelekeza vizuri sana akiwa kama mwanamapinduzi wa Kenya MPYA. Sisi wana JF tujithidi kusambaza ujumbe huu kwa wananchi wenye woga ili waelewe kuwa hata jirani zetu Kenya wanatutakia kheri ili tuweze kwenda mbele. Maana kizazi cha leo hakiwezi kuishi kwa mfumo wa zamani (katiba) Lets wake uuuuuppppp???????
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha wakenya wameona hilo but sisi tunalifumbia macho WAKE UP CCM! WAKE UP!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa Kauli hiyo KUTOKA kwa mmoja kati ya watu watu wachache wanaoheshimika sana Barani Africa kwa kuleta MAPINDUZI YA KWELI KWA FAIDA YA WANANCHI WA KAWAIDA, Ndugu Raila Odingakutoa ushauri kwetu, nasema taasisi mbalimbali zijitokeze na kuungana na Jopo la Wasomi Tanzania, Vyama vya Wafanyakazi, Wakulima, pamoja na CHADEMA ili tukaunde haraka Kamati ya Taifa (Tanzania National Steering Committee for New Constitution) ya Kuandika Upya Katiba yetu.

  Pia, tutume wanaharakati wa kweli kwenda kuazima uzoefu nchini Kenya na Afrika ya Kusini kuhusu mchakato mzima wa Kuandika Katiba Mpya.

  Kamiti hiyo pia iandike Ratiba ya kitu gani kinaanza lini ili wananchi tupate kushiriki ipasavyo.

  Vile vile kamati hiyo itume barua ya mwaliko kwa wadau wote wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo CCM, SMZ, CHADEMA, TUCTA, Faith-Based organisations, Sisi Wamachinga, DARUSO, UDASA, UDOM, na wengine wengi kuchagua kuja kushiriki kwenye mchakato.

  Hii ni kwa sababu KATIBA Si MALI ya serikali KATIBA ni mali yetu sisi Wananchi wenyewe hapa. Na tunapoamua kukibadilisha basi hatutarajii vikwazo na hasa kutoka kwa serikali wezi waliojichagulia KUVUNJA KATIBA kwa makusudi.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  usimsahau mzee punch kwenye list ya wadau
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uwezo Tunao, sijakuelewa maana unavyozungumza ni kama vile kauli ya Odinga tayari ni andiko ambalo limeshakubalika. Umepoteza nguvu nyingi kuelezea Kamati itakavyofanya kazi as if tayari tumeanza mchakato. Isn't it pre-mature?
   
 6. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Katiba mpya ni suala la muhimu maana hata Dr. Slaa na Chadema wamefungua watu macho kuwa chanzo cha umaskini wetu inaweza kuwa ni katiba iliyopo kutokuweka mkazo kwenye mambo ya msingi imekuwa inarekebishwa kwa manufaa ya watu wachache kuwanyonya tulio wengi.

  Mfano ni Rais kuwa na madaraka makubwa sana kiasi cha kuyatumia vibaya hata pale wananchi na bunge wanapokuwa kinyume na rais unakuta katiba imekuwa inambeba rais na Chama tawala.

  Mfano ni Rais kuwa na mamlaka ya kuwateua viongozi wa taasisi kama PCCB, NEC, Msajili wa vyama, Spika wa Bunge, Jaji mkuu, Mkuu wa Jeshi, mkuu wa polisi bila kuangalia uadilifu na utendaji kazi wa mtu.

  Hatisemi rais ateue watu wanaokubalika kwa upinzani la hasha, tunachotaka ni Rais ateue mtu ambaye anakwenda kutumikia wananchi na si chama na rais kama ambavyo tumeona wakijikanyaga kumbeba JK wakati wa kampeni.

  Nampongeza sana Mwema na Mwamunyange kwa Kutumukia wananchi kwani tumeona kazi yake wakati wa kampeni na uchaguzi. Ingawaje CCM imeanza kuwaandama Wakuu wa polisi kwa maeneo ambayo CCM imeshindwa.

  Mwisho naunga mkono hoja ya kubadili katiba na kuwa na katiba mpya ya wananchi wa Tanzania, kwani katiba ya mwaka 1997 imepitwa na wakati na hata hivyo vitu vingi wlikuwa wana copy na kupaste

  Peoples Power
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Amesema suala la katiba ni la WANAINCHI WATANZANIA WENYEWE KUAMUA kenya wamebadili katiba walioikuta baada ya 47yrs sisi 49yrs hatujaona umuhimu wa katiba mpya?wana Jf procedure ya kufuata ni zipi kupata katiba mpya?
   
 8. T

  Tanganyika Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba iliyoko ni kwa ajili ya kulinda watawala...........hili ni kinyume kwani katiba ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, ndugu zangu Watanzania tuamke tupiganie Katiba mpya kwa nguvu zetu wote, tusiwaachie tu wanaharakati na wanachadema. kupata katiba mpya ni faida kwa kila mtanzania. Wanaharakati na wanachadema msichoke tushirikisheni wananchi wote........tuko tayari hata kuandamana kila siku ili kupata katiba mpya! Na nyie wanaccm tuweni kitu kimoja kupigania katiba mpya.......haya ni maendeleo yetu! Wabunge wa CCM simameni, badilikeni, kuweni wazalendo, acheni nidhamu ya uoga.........ya kuwasikiliza na kuwaogopa mafisadi, taifa kwanza chama baadaye! Nyie wakuu wa serikali kwanini hamtaki katiba mpya? inaonyesha kuna madhambi mmefanya hivyo katiba mpya itawapelekea mahali pabaya.......mngekuwa wasafi hili swala lisingekuwa na ubishi, ninataka kuwaambia tu kwamba mkubali msikubali katiba mpya inakuja kwani watanzania ndo wenye maamuzi........hii nchi na mali zake ni za watanzania wote , Mungu alikuwa na makusudi kutupatia nchi tajiri ili Watanzania wote wafahidi na si kikundi cha watu wachache, tumemwita Mungu na tunaendelea kmwita mpaka kusudio lake litimie.

   
 9. m

  mwanza JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Naungana na wote wanaotaka katiba mpya, ila nadhani ili tufanikiwe tunatakiwa kwanza tujue mapungufu ya katiba iliyopo kwani hata hao wananchi tunaowaambia tunataka katiba mpya hawaelewi maana yake, Kenya waliorozesha mapungufu ya katiba (kama mambo ya ardhi) na wananchi wakaelewa kwa nini kuna haja ya katiba mpya.
  Nashauri kama kuna wanasheria ambao wanaelewa mapungufu ya katiba basi watupe mwongozo ili wote tuelewe kwa nini tunahitaji katiba mpya.
   
 10. s

  seniorita JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya kilio cha Watanzania; jamani tuungane wooote wenye kuitakia nchi yetu mema.
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mchakato wa katiba unaweza kuanza hata leo kama viongozi walio madalakani wataona kunaumuhimu ila tatizo lililopo ni kuwa katiba ya kale inawalinda wachache hivyo na kwa kuwa hao wachache ndio wapo madalakani tunahitaji nguvu ya hali ya juu kulata hayo mabadiliko,tusikate tamaa yawezekana

  mapinduziiiiiiii daimaaaaaaaaa
   
Loading...