Ruto asalimu amri, asema yuko tayari kwa mazungumzo yasiyohusu kugawana madaraka na Raila Odinga

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,821
Odinga anazidi kukaza,amkalia Ruto kama Vile Beberu USA alivyomkalia Putin Hadi akakimbia Mkutano wa Brics 😁😁

-----
Rais wa Kenya, Dk William Ruto, amesema yuko tayari kufanya mazungumzo kuhusu masuala yanayo waathiri Wakenya, na siyo yale yahusuyo kugawana madaraka na kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga.

Mtandao wa Nation umelipoti leo kuwa Rais Ruto, akiwa katika Mji wa Kericho jana, alihutubia taifa katika siku ya kwanza ya maandamano ya kitaifa ya siku tatu, yakilenga kupinga ongezeko la kodi na gharama za maisha, huku akiwataka Polisi kuwashugulikia ipasavyo watu aliowaita wahalifu na wavurugaji wa amani ya nchi.

"Tuliawaambia wapinzani wetu kutushirikisha mazungumzo ya hoja zao kupitia uwakilishi wa wabunge wao, lakini wamechagua maandamano. Wanatakiwa kutumia njia zinazokubalika kisheria na kikatiba kuwasilisha madukuduku yao," amesema Rais Ruto

Ruto aliongeza kuwa uongozi wake haukinzani na vifungu vya Katiba vinavyoruhusu maandamano lakini; "Hatutakuwa Taifa la vurugu na migogoro...mtu yeyote asitutimie vifungu hivi kuchochea machafuko, sisi ni taifa la Kidemokrasia na lenye amani," alisema Ruto muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa uzalishaji maji wa Kimugu wenye thamani ya Sh1.5 bilioni (za Kenya).

"Hatuna spare parts (vipuli) vya hili taifa letu. Ni mahala pekee tunapopaita nyumbani lazima tukubaliane kwa pamoja kupalinda na kulinda demokrasia yetu. Siasa zetu ziwe za ushindani lakini zisiwe na vurugu wala uhalifu," alisema

Wakati huo, Makamu wa Rais, Rigathi Gachagua amemshutumu Rais Mstaafu, Uhuru Kenyatta kufadhiri maandamano hayo yanayoongozwa na Odinga huku akimtaka kujitokeza hadharani kuongoza maandamano hayo ya kitaifa.

Gachagua aliutaka upinzani nchini humo kutambua kuwa uchaguzi umemalizika muda mrefu na wananchi wanatakiwa kutulia kupisha Serikali itekeleze miradi yake.

Wakati huo, Rais Ruto amesitisha uingizwaji wa vyakula na bidhaa zinazotengenezeka ndani ya nchi ili kutengeneza fursa za ajira, ubunifu na soko kwa viwanda vya ndani.

"Waagizaji wa samani kutoka nje ikiwemo viti, vitanda na meza kutoka China, Ulaya na Marekani kuanzia sasa tumesitisha....taarifa ziwafikie kwamba mkiingiza mtakutana na kodi kubwa," alisema

Rais Ruto alisema uongozi wa Jimbo la Kericho nchini humo imetenga Sh500 milioni (za Kenya) kwa ajili ya kuongeza tija katika mnyonyoro wa thamani wa mazao ya kilimo ili kukuza kipato cha wakulima nchini humo.

Ili kukuza kilimo, Ruto alitangaza kupunguza kwa pembejeo za kilimo kutoka Sh3, 500 hadi 2,500; " Tutaongeza uagizaji wa mbolea kwa ajili ya wakulima wetu kutoka magunia milioni moja za sasa hadi milioni nane kuongeza uzalishaji na kuongeza ajira nchini."

Chanzo: Mwananchi
 
Asa ndio nini? Alitakiwa akaze buti asimlegezee odinga, kama ndio hivyo akubali tu wagawane madaraka vurugu ziishe. Odinga atakuwa mshindi na anajua kucheza na siasa za kenya
 
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?"
 
sasa alinua na wakati uhuru akimpa hand shake odinga.....sasa hivi UHURU anachochea ile nguvu ya odinga Mpaka ruTo na yeye atoe handshake..odinga ana wafuasi wanaomtii zaidi ya nusu ya wapiga kura...jumlisha wezi vibaka na jobless..akiitisha maandamano pananoga...
 
Back
Top Bottom