Raia wafunga barabara ikwiriri

Wakusini

JF-Expert Member
May 28, 2011
805
609
Habari nilizozipata kutoka kwa chanzo cha uhakika ni kuwa wananchi wa Ikwiriri rufiji wamefunga barabara iendayo Mtwara,na fujo zikiendelea madai ikiwa ni kama yale ya WANA SONGEA kuwa kuna mauaji ya raia wasio na hatia yanaendelea na jeshi la polisi kutochukua hatua,kituo cha polisi kipo hatarini kupigwa kibiriti!!! Taarifa zaidi!!!!!!!!
NAWASILISHA!!!!!!!!!!!!!!
 
Vurugu kali zaendelea huko Ikwiriri~Rufiji baina ya Wandengereko na Wasukuma; chanzo cha vurugu ni baada ya wasukuma kulisha mifugo yao ktk mashamba ya wandengereko ambapo baada ya malumbano ya muda mrefu, Jana Mndengereko mmoja aliuawa.
Baada ya tukio hilo Wandengereko wakareport Police lkn hawakupata ushirikiano na kuamua kuingia mtaani kimapigano.
Vurugu hizo zimeshika sura mpya baada ya kuvamia makazi ya Police na kuchoma nyumba moja ya Police.
Mapigano yanaendelea,Mwenye info zaidi atupe updates"
 
Wadau naskia tetesi kua wakulima na wafugaji wa ikwiriri huko rufiji wanachapana. Chanzo sijakijua, mwenye updates atumwagie hapa.
 
yaaani natamani mapigano yatawanyike na kusambaa nchi nzima
 
Wadau naskia tetesi kua wakulima na wafugaji wa ikwiriri huko rufiji wanachapana. Chanzo sijakijua, mwenye updates atumwagie hapa.

clouds fm wamekua wakiripot hiyo ishu tangu saa 6 mchana,,,,ni kwamba wakulima na wafugaji wa KISUKUMA wamekua wakipigana na kuna mtu nadhan amepoteza maisha
 
KIla mara serikali imekuwa ikiichukulia suala la hawa wafugaji kimzaha mzaha lakini wananchi wanateseka kweli
 
Nipo safarini kuelekea Dar nikitokea Mtwara, hapa ikwiriri wananchi wameweka magogo kuzuia magari yote yaendayo Dar..polisi ni kama vile wameshindwa kuzuia fujo hizo..tupo hapa takribani masaa mawili...chanzo kinasema ni vurugu kati ya wasukuma( wafugaji) walioua mmoja wa raia wa hapa ikwiriri. So raia wanatumia kinga ya abiria ili waweze kutekelezewa matakwa yao na polisi..
 
Mawazo huru huruhusiwa......ila huo ni mtazamo wa VIJANA....! Ambao hata MKANDA wa vita vya KAGERA hawajuona na wala MAUAJI YA KIMBARI RWANDA ...! Akipata wasaa wa kuona picha hizo sidhani kama atabaki na kauli ya kutamani machafuko yaenee, aweza kutamani machafuko ya kuwatoa watawala na chama fulani lakini akumbuke kuwe hatutabaki salama
 
Je wewe ndinga una akili timamu???
Je wewe ni great tjinker? Je umelelewa katika familia au uchchoroni? Je wewe ni kibaka? Hivyo umezoea kula kunywa kwa vurugu?

VIJANA TUOMBE AMANI NA KUITUNZA KAMA JICHO, SI MNASIKIA MAJIRANI ZETU. Je lile ule mgogoro wa Kilosa- Morogoro ulimalizika?
 
yaaani natamani mapigano yatawanyike na kusambaa nchi nzima
Utakua hukielewi unacho kitamani. Umefikiria waathirika wa unachokitamani? Kama taifa tunayomatatizo Kama hayo ya wakulima na wafugaji lakini suluhu sio kwa mapambano kuenea nchi nzima. Umenisikitisha.
 
Kunasababu gani ya msingi ya mtu kuombea machafuko nchi nzima. Huo ni upuuzi tena mtupu. Kama anapenda si aende huko ikwiriri
 
Vurugu zinazidi kuchukua sura nyingine baada ya Police kuanza kukamata wananchi na kuna maandamano makubwa kiasi kwamba barabara kuu imefungwa na ni piga nikupige baina ya Polisi na wakulima hao(Wandengereko)
Jingine lililo kubwa zaidi ni kwamba tatizo hili linazidi kuchukua sura ya kikabila na kidini.
Wandengereko hawawataki Wakristo huko kwao na kabila hilo la Kisukuma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom