Baadhi ya Polisi Tanzania ni wauaji na watesaji; OCS na wenzake sita kortini wakituhumiwa mauaji ya raia

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
878
1,599
Tuna changamoto kubwa sana ya uwajibikaji binafsi mpaka mtu awajibishwe na ikifika hatua hiyo inakua kwa aibu sana.

Baadhi ya Polisi Tanzania ni genge la watekaji na wauaji na wanajua kwa sababu wanayaratibu wao wenyewe. Huku Rais anahubiri zile 4R sijui labda akitoka kuhubiri jukwaani behind the scene anatoa maagizo mengine.

But kwa haya yanayoendelea IGP hakupaswa kuendelea kuwa kwenye hicho kiti.
---
Muleba.png

Askari Polisi wanne akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Kata ya Goziba, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, John Mweji na mgambo watatu wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumuua Baraka Lucas.

Mwili wa Lucas (20) aliyekuwa mbeba dagaa wabichi Mwalo wa Kisiwa cha Goziba, ulipatikana ukielea Ziwa Victoria Juni 12, 2024 ikiwa ni siku nne kupita tangu adaiwe kukamatwa na polisi wa kituo hicho Juni 9, mwaka huu.

Ndugu zake baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa ndugu yao na askari wa doria usiku wa manane, walikwenda kituoni bila kufanikiwa kumuona na baadaye Juni 12, 2024 ndipo mwili wake ulionekana kando ya Ziwa Victoria ukielea.

Hii ni kesi ya pili kuhusisha maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya ile ya inayoendelea Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, ikiwahusisha maofisa saba walioshitakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis.

Washtakiwa hao saba ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC-CID) wa Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Gilbert Kalanje na aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi (OCS) cha Mtwara Charles Onyango aliyekuwa Mrakibu Msaidizi (ASP).

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Intelijensia, Nicholaus Kisinza, mkaguzi msaidizi wa Polisi Yesse Msuya, aliyekuwa mganga mkuu zahanati ya polisi akiwa na cheo cha mkaguzi msaidizi, Shirazi Mkupa na mshitakiwa Koplo Salum Juma Mbalu.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wakidaiwa kumuua kwa makusudi Mussa Hamis katika kituo cha Polisi Mitengo wilaya ya Mtwara Januari 5, 2022 na kutupa mwili wake Majengo kata ya Hiari.

Madai ya mauaji Muleba

Katika kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili OCS, John Mweji, washitakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Jumanne Julai 23, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Masesa, huku polisi wakijaribu kuifanya kesi kuwa siri.

Hali hiyo ndiyo iliwapa wakati mgumu wanahabari kuweza kufahamu nani ni mgambo nani askari wa Jeshi la Polisi zaidi ya kuambiwa kuwa katika washitakiwa hao saba, Askari Polisi ni wanne na askari wa Jeshi la Akiba (mgambo) ni watatu.

Washtakiwa wengine mbali na OCS wametajwa kuwa ni Ahmad Rashid, Fransis Hayshi, Ally Jumanne, Emmanuel Massatu, Evodius Makaka na Athumani Malindo na watatu ni Polisi na watatu ni mgambo.

Akisoma shitaka hilo katika kesi hiyo ya mauaji (PI) namba 18914 ya mwaka 2024, Wakili wa Serikali, Agness Owino alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 9, 2024 na hawakutakiwa kujibu lolote na kupelekwa mahabusu gerezani.

Hii ni kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kusikiliza kesi za mauaji huku upande wa mashitaka ukiieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, 2024 itakapotajwa tena.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
 
Time yake inakuja haifiki 2025

Keep this!
Hata waziri wa mambo ya ndani,
Samia anachofanya anasikiliza tuhuma anakupa muda akiangalia jambo au anakuhamisha Ila akijiridhisha unakula mtama!
Kwa jinsi huyu IGP alivyopuyanga na mafaili nayokutana nayo kwenye PDF GH hapo meza kuu, sioni akifika 2025

Britanicca
 
Kuna wananchi fulani, maeneo yanayokaribiana, wanasema wamekamata watu waliowadhuru watoto kwa vitu vyenye ncha kali...

Shule za kimombo media karibu na maeneo hayo, nasikia wamewapa wazazi barua za kuwa makini na watoto wao pindi waendapo shule na kurudi home.

Nasikia hanga-aya/frogi deaf amesema ni darma, akitanguliwa na aijipu aliyesema wanajiita-ka.
 
Time yake inakuja haifiki 2025

Keep this!
Hata waziri wa mambo ya ndani,
Samia anachofanya anasikiliza tuhuma anakupa muda akiangalia jambo au anakuhamisha Ila akijiridhisha unakula mtama!
Kwa jinsi huyu IGP alivyopuyanga na mafaili nayokutana nayo kwenye PDF GH hapo meza kuu, sioni akifika 2025

Britanicca
Kwa namna ulivyotoa utabiri wa kung'olewa Kwenye nyadhifa zao, akina Nape na Makamba, kwa usahihi kabisa, basi na hili napaswa kuliamini Kwa asilimia kubwa kabisa😀
 
Kwa jinsi huyu IGP alivyopuyanga na mafaili nayokutana nayo kwenye PDF GH hapo meza kuu, sioni akifika 2025
Acha kutudanganya, acha kumpa Samia sifa za uongo we chawa wewe.

IGP Wambura na DCI Kingai wameteuliwa na Samia akijua wazi - na kama hajui alipigiwa kelele akaambiwa- hawa wawili ndio walikuwa nguzo za jeshi dhalimu la polisi kwenye serikai za Kikwete na Magufuli. Wana damu mikononi mwao.

Akawateua anyhow. Kwa sababu alijua hawa wanajua jinsi ya kumuwezesha kushikilia dola lisilo na ridhaa ya raia.

Samia hatumbui Kamanda eti kakosa weledi, kaua raia. Yameanza leo haya ?Acha kutufanya sisi wajinga, nenda kadanganye watu Katavi vijijini huko wanaotoka Kivu kwenye makambi ya wakimbizi walikofurika kumuona Samia last week, labda utapata half dead illiterates huko.
 
Jeshi la Polisi kumejaa mabazazi
Ila pia kuna police wengine wanapenda haki, sema omba sana Mungu akutanishe nao pale kila unapopata tatizo la kipolisi,watakusimamia hadi unapata haki yako bila hata ya kutoa hata cent tano!!
 
Ila pia kuna police wengine wanapenda haki, sema omba sana Mungu akutanishe nao pale kila unapopata tatizo la kipolisi,watakusimamia hadi unapata haki yako bila hata ya kutoa hata cent tano!!
Kuna yule mkuu wa kikosi Cha mbwa na farasi Tanzania 🇹🇿, yule hua sio MLA rushwa..serikali imwone...majura
 
Uelewa mdogo wa Polisi wengi kuanzia level za chini mpaka hawa wenye vyeo, wengi wao hupenda kutesa watu bila hata kujua historia za Afya zao, matokeo yake ni kusababisha vifo na kuanza kupindisha mambo ili wawe salama.

Kutesa sasa inapaswa waombe kibali kutoka kwa either RPC au IGP na kuweka na sababu ambazo wote hao watakubaliana mtu lazima ateswe, aina ya mateso iwe clarified na wataalam wa Afya na mteswaji kabla ya yote apimwe Afya yake, iangaliwe historia ya maisha yake nk.
Kuruhusu tu utesaji wa kiholela huko vituoni ndio kunatuletea hizi mambo za mauaji Kila siku.
 
Kwa jinsi ambavyo Jeshi la Polisi Tanzania linavyofanya kazi, halina tofauti kabisa na utendaji kazi wa makundi au Magenge ya Uhalifu Kama vile Kundi la Niko Haram la nchini Nigeria au Genge la Umafia la Sinarowa.

In fact, Tanzania Police Force is like the State-sponsored terrorist group.
 
Time yake inakuja haifiki 2025

Keep this!
Hata waziri wa mambo ya ndani,
Samia anachofanya anasikiliza tuhuma anakupa muda akiangalia jambo au anakuhamisha Ila akijiridhisha unakula mtama!
Kwa jinsi huyu IGP alivyopuyanga na mafaili nayokutana nayo kwenye PDF GH hapo meza kuu, sioni akifika 2025

Britanicca
Mkuu
Jina Lako Ni Kubwa Unakubalika Endapo Watamfuta Kazi Ya Iigiipii
Basi Wampe Wankyo Ramadhan Nyegesa Naye Atabaruku Kidogo Asafishe Jeshi
 
Mkuu
Jina Lako Ni Kubwa Unakubalika Endapo Watamfuta Kazi Ya Iigiipii
Basi Wampe Wankyo Ramadhan Nyegesa Naye Atabaruku Kidogo Asafishe Jeshi
Tatizo lililopo Tanzania Siyo Ubovu wa Manahodha tu peke yake, bali hata Meli yenyewe (Katiba ya nchi) pia ni Mbovu Sana, imetoboka. Kwa hiyo hata ukibadilisha Manahodha mara Milioni bado haitasaidia kitu, meli ya Mv Tanzania lazima itazama tu siku moja.

Suluhisho pekee lililobaki kwa Sasa ni kutengeneza au kuunda Meli Mpya kabisa na kuwaajiri Manahodha Wapya kabisa waliofunzwa vizuri, hawa waliopo hawafai, wamechoka, wamezeeka mwili na akili. Hawana tena uwezo wa kutupeleka mahali popote pale palipo salama.
 
Mifumo mzima kuanzia kuajiri na mafunzo ya hawa askari naamini haupo sasa.
Lakini pia tutambue askari hawa wengi ni wahitimu wa shule zetu za msingi na sekondari ambapo pia wote tunakubaliana mfumo wa elimu haupo sawa.
 
Time yake inakuja haifiki 2025

Keep this!
Hata waziri wa mambo ya ndani,
Samia anachofanya anasikiliza tuhuma anakupa muda akiangalia jambo au anakuhamisha Ila akijiridhisha unakula mtama!
Kwa jinsi huyu IGP alivyopuyanga na mafaili nayokutana nayo kwenye PDF GH hapo meza kuu, sioni akifika 2025

Britanicca
Duuh! Kuna ukweli cc awadhi juma
Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom