Raia wa Marekani wapiga kura kumchagua Rais mpya kati ya Donald Trump anayewania muhula wa pili au mpinzani wake Joe Biden

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
776
2,404
Trump, rais wa 45 wa Marekani anajivunia rikodi ya kuimarisha uchumi na kupunguza kwa kiwango kikubwa ukosefu wa ajira lakini anakosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia janga la virusi vya corona.

Biden, mwanasiasa anayegemea sera za wastani za mrengo wa shoto ameahidi kulinda haki ya wamarekani kupata huduma za afya, mafao kwa wazee na kutengeneza nafasi mpya za kazi kupitia sekta ya nishati jadidifu.

Mchuano ni mkali na wasiwasi umetanda juu ya kuzuka mabishano baada ya uchaguzi huu, baada ya Rais Trump kutishia kujitangazia ushindi hata kabla ya matokeo kukamilika.

=========================UPDATES====================

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.

Mpaka sasa Joe Biden anaongoza kwa kura za wajumbe maalum 131 na Trump akiwa na idadi ya kura 98 za wajumbe maalum. Matokeo yanaendelea kutangazwa.

Wamarekani zaidi ya milioni Mia moja wamepiga kura ya kuamua iwapo watamrudisha madarakani Donald Trump au wataamua kuleta mabadiliko kwa kumchagua mgombea wa chama cha Demokratik Joe Biden, baada ya wanasiasa hao wawili kupambana vikali kwenye kampeni zao katika muktadha wa janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Idadi hiyo inaashiria kwamba ushiriki wa wapiga kura utavunja rekodi ya karne. Washindani hao walikamilisha kampeni zao kwenye majimbo muhimu. Kura za maoni zinaonyesha kuwa Biden yuko mbele lakini kinyang'anyiro kinakwenda bega kwa bega katika majimbo yanayoweza kuamua mshindi.
 
Huo uchaguzi hatujasikia watu wametekwa, kujeruhiwa wala kuuwawa wala kwamba zimepatikana kura feki.

Waafrika tulilaaniwa na tunajifanya kuigiza kufanya uchaguzi kimakosa kabisa wakati hatujui hata nini maana ya uchaguzi.

Marehemu Pieta Bother aliwahi kusema mwafrika hakuumbwa kutawala ila kutawaliwa tu. Today we're witnesses to what Bother said well over 40 years ago.
 
Huo uchaguzi hatujasikia watu wametekwa, kujeruhiwa wala kuuwawa wala kwamba zimepatikana kura feki.

Waafrika tulilaaniwa na tunajifanya kuigiza kufanya uchaguzi kimakosa kabisa wakati hatujui hata nini maana ya uchaguzi.

Marehemu Pieta Bother aliwahi kusema mwafrika hakuumbwa kutawala ila kutawaliwa tu. Today we're witness to what Bother said well over 40 years ago.
Daah nakusikitikia sana Ndugu yangu
 
Back
Top Bottom