Mnamo Januari 2017,
Taifa lenye nguvu duniani
litakuwa na kiongozi mpya baada ya kampeni
ndefu tena iliyokuwa ghali - lakini uchaguzi wa
Marekani unakuwaje?
Marekani inapochagua rais, haichagui kiongozi
wa taifa na mkuu wa amiri jeshi kubwa duniani.
Ni jukumu kubwa sana. Kwahivyo mpango
unakuwaje?
Nani anayeweza kuwa rais?
Kiufundi kuwania urais , sharti uwe mzaliwa
Marekani, raia, mwenye umri usiopungua miaka
35 na uwe umeishi nchin ikwa miaka 14.
Inaonekana rahisi sio?
Hatahivyo kwa kweli, karibu marais wote tangu
1933 wamewahi kuwa magavana, seneta au
mwanajeshi wa kiwango cha juu. Na hilo ni kabla
ufikirie iwapo utateuliwa katika chama na kuvutia
vyombo vyahabari kitaifa.
Katika uchaguzi mwaka huu 2016 katika kiwango
kimoja ambapo kulikuwa na magavana 10 au
waliokuwa magavana na kumi waliokuwa
masentea au waliokuwa katika wadhifa huo,
hatahivyo wengi walijitoa.
Mtu mmoja anateuliwa kuwa mgombea wa
chama cha Republican na Democratic katika
uchaguzi.
Clinton atabahatika mara ya pili?
Trump atangaza sera zake kuhusu Uhamiaji
Kwanini ni Hillary Clinton v Donald Trump?
Msururu wa uchaguzi unafanyika katika kila
jimbo na maeneo ya ng'ambo, kuanzia Februari,
unaobaini ni nani anayekuwa mgombea rasmi wa
kila chama.
Kila mshindi anakusanya idadi ya wajumbe -
ambao ni wanachama walio na mamlaka ya
kumpigia mgombea kura katika mkutano wa
chama uliofanyika Julai ambapo wagombea
walithibitishwa rasmi.
Democrat Hillary Clinton mwanachama wa
Republican Donald Trump walikuwa washindi wa
wazi mwaka huu na waliteuliwa rasmi katika
mikutano ya vyama vyao.
Waliwateua pia wanaonuia kuwa makamu wao
wa rais - Senata Tim Kaine kutoka Virginia kwa
Bi Clinton, na Gavana wa Indiana Mike Pence
kwa chama cha Republican.
Sera kuu katika kampeni
Kumekuwa na msururu wa mzozo ulioanzishwa
na Donald Trump, tangu mfanyabiashara huyo
alipozindua kampeni yake kwa kuwataja
wahamiaji wa Mexico kama 'wabakaji na
wahalifu'. Ugombea wake umekumbwa na mzozo
kila wiki kadha zinapopita.
Amezusha mzozo wa
maneno na jaji, mwanamitindo wa zamani na
familia ya kiislamu ya mwanajeshimmoja
aliyeuawa vitani.
Amelazimika kutetea kukaidi kwake kuwasilisha
malipo yake ya kodi na pendekezo kwamba
huenda hajalipa kodi kwa miaka 18 na pia
kutetea maswali yanayozuka kuhusu shirika lake
la misaada.
Na Hillary Clinton amekabiliwa na shutuma
kivyake. Mzozo kuhusu barua pepe binafsi
alizotuma zimetia dosari heshima yake kwa
kiwango kizito,na kumekuwa na maswali kuhusu
misaadaya nje wanayotoa kupitia wakfu wao
familia yake - Clinton Foundation.
Trump pia
ameangazia kuhusu jukumu lake katika
kuwanyanyasa wanawake waliodai kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mumewe Bill.
Na
mtandao wa WikiLeaks umekuwa ukifichua barua
pepe zilizovamiwa katika mtandao zilizodhihirisha
mawasiliano ya aibu kai ya wafuasi wa timu yake
ya kampeni.
Barua pepe: Jaji amtaka Clinton kujibu
mashtaka
Clinton afunguliwa kesi kwa mauaji ya Libya
Trump na Clinton walumbana kwenye
mdahalo
Clinton:
Sitojali atakachosema Trump
Ni nani aliyeshinda mjadala wa tatu?
Awali wagombea walijadili sera lakinimjadala
ukapamba moto wakati Bi Clinton alipogeuza
suali kuhusu Wikileaks kuwa shambulio dhidi ya
uhusiano wa Trump na Urusi.
Wakati huo Trump wa kukatiza kauli akarudi na
kuanza kumuita Bi Clinto mrongo na kudai
kwamba yeye ndio kinyago cha Urusi na sio
yeye.
Trump amesema wanawake wanaomshutumu
kuwanyanyasa kingono, aidha ni watu wanaotaka
kujulikana au wafuasi wa kampeni ya Clinton.
Donald Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo
ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala
wa mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton Las
Vegas.
"Nitakuambia wakati huo," alimwambia
muendesha mjadala Chris Wallace.
Kwa siku kadhaa amedai kuwa kuna
'udanganyifu' katika uchaguzi huo.
Ni kauli iliyosalia kwenye vichwa vya habari na
kugubika majadiliano kwa siku kadhaa.
Trump v Clinton:
Nani anaongoza?
Trump na Clinton wapambana tena
Uchaguzi wa Novemba unakuwaje?
Kura zinapigwa Jumanne Novemba 8.
Mgombea mwenye kura nyingi katika kila jimbo
anakuwa mgombea anayeungwa mkono katika
jimbo hilo kuwa rais.
Yote itaishia katika mpango wa uchaguzi
uanojulikana kana the electoral college, kundi la
watu 538 watakao mchagua rais .
Na nusu ya
idadi hiyo inatosha kumchagua rais.
Lakini mjimbo yote hayako sawa - California, kwa
mfano ina zaidi ya mara 10 idadi ya atu wa
Connecticut, kwahivyo kuna tofauti ya uzito.
Kila jimbo ina idadi yake ya wapiga kura hao
kutokna na idadi ya watu katika jimbo.
Wakati raia wanapomchagua mgombea
wanaompendelea, wanawachagua pia wapiga
kura hao.
Lakini katika karibu kila jimbo (isipokuwa
Nebraska na Maine), mshindi huchukua kura zote
- kwa hivyo mtu anayeshinda wapiga kura wengi
mfano New York, for example, atapata kura zote
29 zinazopigwa New York.
Rais anaanza kazi lini?
Siku na wiki kadha baada ya uchaguzi - iwapo
kura zitaamua - mshindi ataunda baraza la
mawaziri na ataanza kuunda sera kamilifuya
uongozi.
Wakati huo huo rais anayeondoka anajitahidi
kuacha sifa nzuri ya uongozi wake na
kufungasha virago vyake.
Kwa mujibu wa katiba ya Marekani, rais
anaapishwa Januari 20 ya mwaka unaofuata
Source: Bbc Swahili