Raia wa China akamatwa kwa wizi kwenye mradi wa SGR

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 11 akiwemo raia wa China, Meng Zhaon Ming (29) kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa saruji na mafuta aina ya Diesel katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 9,2023 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema Ming ambaye ni mtunza stoo anashikiliwa na wenzake sita kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa mifuko 390 kwenye mradi wa SGR huku mmoja akikutwa na Lita 800 za mafuta ya Diesel kutoka kwenye mradi huo.

Kamanda Mutafungwa amesema mifuko hiyo ya saruji ni kati ya mifuko 600 inayodaiwa kuibwa katika mradi huo huku akiwataja watuhumiwa wengine katia wizi huo kuwa ni dereva wa gari lililotumika kusafirisha saruji hiyo, Juma Maiko (29), mnunuzi wa saruji, Masele Shija (35) na mbeba mizigo aliyetumika kushusha saruji hiyo, George
 
Huu Mradi Unajengwa Kwa Wizi Mwingi Lazima Utakuwa Wa Hovyo Hovyo Mno
 
Back
Top Bottom