Raia Mwema: Wanamtandao wampa Dk. Slaa ushindi 76%... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia Mwema: Wanamtandao wampa Dk. Slaa ushindi 76%...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TandaleOne, Sep 22, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi gazeti la Raia Mwema limetoa taarifa ikisema "Wanamtandao wampa ....na kuendelea na takwimu ambazo kutokana na ile picha,chanzo ni hapa JF.

  Katika poll ya JF kuna watu elfu 6700 ambao naamini kabisa ndani yake wapo wenye multiple accounts (ni kawaida kwa watumiaji wa forums za aina hii). Tuangalie kwamba JF ina memba kama 21000. That means those who participated in the polls ni around 30% (tusahau kwamba wapo wanaopiga kura hata mara 50.)

  Suala langu ni sampuli hii na mchanganuo wake wenye mapungufu mengi (sitaki kusema kwamba si sahihi) ukiamua kuvaliwa njuga na wanaopenda majibizano na wakaenda mbali wakachambua wakatoa analysis ya hizi polls na mengine yaliyojificha nyuma yake nini itakuwa picha ya gazeti hili mbele ya jamii?Je,katika wapiga kura wa nchi hii zaidi ya million 15 sample space ya watu 7000 (with multiple & fictious names) inafaa kusimamiwa na gazeti linalojiita la uchunguzi na kitaifa?

  Ndo maana asubuhi nimeweza kuona CNN wakiongelea uchaguzi wa Nigeria na si wa Tanzania. Intellectual failure.

  :violin:

  SOMA HABARI HII:

  • Daily News walimkubali kwa 60%
  • Synovate wakana madai ya CHADEMA kumpa 45%
  WAKATI kampuni ya kibiashara inayojihusisha na tafiti ya Synovate Limited ikikanusha taarifa za kubaini kwamba mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa sasa anakubalika zaidi, Watanzania wanaotumia mitandao wamempa mwanasiasa huyo asilimia kubwa ya ushindi kulinganisha na wagombea wengine.

  Ufuatiliaji wa Raia Mwema, katika mitandao mbalimbali ukiwamo ule wa gazeti la Serikali la Daily News (Daily News Online Edition) na mtandao maarufu kwa mijadala wa Jamiiforums unaonyesha kwamba Dk. Slaa anakubalika zaidi katika mtandao kuliko wagombea wengine akiwamo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

  Hata hivyo, kumekuwa na angalizo katika mitandao kwamba si Watanzania wengi wanaotumia mitandao hata kama kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mtandao kupitia simu za mikononi, hoja ambayo bado inaweza kutoa taswira tofauti katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, kutokana na wapiga kura wengi kuishi vijijini na wanaoishi mijini kutofahamu chochote kuhusu mtandao kama anavyosema na mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamiiforums:

  "Ingekuwa JF (Jamiiforums) inasomwa na asimilia 50% tu ya Watanzania wote, basi, Dk. Slaa angepita kiurahisi sana. Lakini kwa kuwa wengi hawapiti humu inabidi juhudi za ziada zifanyike kushinda".

  Kura za maoni zilizokuwa zikiendeshwa na Daily News zikiwa na swali: ‘Will Dr. Slaa win the presidential race? ' (Je, Dk. Slaa atashinda urais?) zilionyesha kwamba kati ya watu 161 wa mwanzo waliopiga kura walionyesha kumpa Dk. Slaa asilimia 60.87 na ‘Hapana' walikuwa asilimia 28.57, kabla ya kura hizo kusitishwa, kutokana na taarifa za kuwapo hofu ya ‘uchakachuaji' uliodaiwa kufanywa na wafuasi au wapinzani wa Dk. Slaa.

  Kwa upande wa mtandao wa Jamiiforums, zaidi ya watu 6,420 wamepiga kura hizo za maoni na kuonyesha kwamba Dk. Slaa amekubalika kwa watu 4, 895 sawa na asilimia 76.25 akifuatiwa na Kikwete ambaye anaonekana kukubalika kwa watu 779 katika mtandao huo, sawa na asilimia 12.13 akifuatiwa kwa karibu zaidi na Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 448 (6.98%) wakati mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akikubalika kwa watu 205 (3.19%) na Mutamwega Mugahywa wa TLP akikubalika kwa watu 93 (1.45%).

  Mwazilishi wa mada hiyo ya kura za maoni aliweka swali "Je,Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?" Kabla hata ya majina ya wagombea kutangazwa na yeye mwenyewe kutangaza kuwania nafasi hiyo, Dk. Slaa alikuwa akitajwa kuwania nafasi hiyo na orodha ya majina kubandikwa mtandaoni badaa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza orodha ya wagombea hao.

  Wachangiaji wengi katika mtandao huo wa Jamiiforums ambao baadhi ya watu wanautuhumu kupendelea wapinzani, wamekuwa wakitoa sifa kuu za mtu anayestahili kuwa Rais wa Tanzania na kumchambua Kikwete kuwa amepoteza sifa za kuendelea na nafasi hiyo kutokana na kushindwa kupambana na ufisadi kikamilifu kama alivyoahidi wakati akiingia madarakani mwaka 2005.

  Miongoni mwa sifa walizoanisha katika mtandao huo ni pamoja na kuwa Rais ajaye anatakiwa awe ni msomi, mkimya, mchapa kazi, hana makundi na asiye na chembe ya ufisadi.

  Kabla ya majina ya wagombea kutangazwa, wachangiaji waliwataka wagombea wa Upinzani mwaka 2000 na 2005 wasijitokeze tena mwaka huu akiwamo Freeman Mbowe wa CHADEMA, Lipumba wa CUF, Augutine Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP kwa maelezo kwamba matokeo ya nyuma yanaonyesha kwamba hawana jipya mwaka huu.

  "Wanachotakiwa kukifanya sasa hivi ni kumchagua mtu tofauti kabisa. CCM hawawezi kubadilika. Rais ni nafasi ya Slaa sasa kwa ajili ya kusafisha na kuziba mianya ya ufisadi mkubwa. Baada ya hapo tunaweza kuchagua Rais mchumi ili ajenge uchumi wa nchi. Kwa sasa lazima tuondoe ufisadi kwanza, CCM hawawezi kuuondoa.

  "Kikwete alisema anawajua wala rushwa, wauza madawa ya kulevya, wezi wa EPA waliorudisha fedha na wale wahujumu wa Bandarini lakini kashindwa kuwataja wala kuchukua hatua ilhali yeye tumempa mamlaka yote kikatiba ili ailinde nchi hii na mali zake.

  "Slaa ni mzalendo wa kweli maana pamoja na kuwa hana mamlaka ya kuwafanya lolote mafisadi lakini kawataja hadharani bila woga au kuumauma maneno ingawa anajua hatari inayomkabili kupambana na watu wa aina hiyo. Huyu akipewa mamlaka ya kuongoza nchi mafisadi, wezi wa mali za umma nk, itabidi wakajichimbie makaburi wajizike wenyewe. Slaa ndio Rais anayefaa kwa wakati huu tulionao," anasema mchangiaji mmoja wa Jamiiforums.

  Baadhi ya vyombo vya habari wiki hii vilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisema kuwa CHADEMA ina matokeo ya kura za maoni za Synovate yanayoonyesha kuwa Dk. Slaa anakubalika kwa asilimia 45 akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 41, kauli iliyowalazimu Synovate kukanusha.

  Akizungumza na waandishi wa habari juzi Jumatatu, Meneja wa Synovate Limited, Aggrey Oriwo alisema taarifa hizo ni za kughushi, hazina ukweli wowote na zinaupotosha umma kwa kuwa hawajawahi kufanya utafiti wowote unaohusu kukubalika kwa wagombea wa urais.

  Oriwo alisema kwa kawaida kampuni yao hufanya utafiti wa hali ya kisiasa kila baada ya miezi mitatu na kwamba wanatarajia kufanya hivyo kabla ya Oktoba 31 na kutoa taarifa yao, kauli iliyotolewa pia na Taasisi ya Mpango wa Utafiti na Elimu Demokrasia Tanzania (Redet), ambao nao wanatarajia kufanya utafiti wa mgombea anayekubalika.

  Source: Raia Mwema
   
 2. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  wewe mwenyewe ndio umevote mara nyingi baada ya kuona jahazi lako linazama
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Roho isikuume sana.

  Jibu linaweza kuwa rahisi kwa mawazo yako; je ukienda kule Daily News gazeti ambalo lipo negative sana na Dr Slaa kulionyesha takwimu zipi?

  Anyway; labda ungechukua reason ambayo inakuwa sahii kabisa ni kuwa; wasomao mtandao wengi wanaweza kuwa ni wasomi, ambao ni wachache, wengi waliopo nje, mijini, suala la multiple voters ni negligible. Kama hivyo ni rahisi Daily News wangekuwa wa kwanza ku-fake IDs. Maji yako shingoni; this is 2010!!

  You Must reap what you saw.
   
 4. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha wazalendo wote wanamhitaji Slaa kuwaongoza
   
 5. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  tandale0ne...broda kwanini huamini au hutaki ku-ukubali ukweli kuwa CHADEMA na Slaa "kwa sasa ndio chaguo la MUNGU" na wanapendwa na watanzania wengi waliochoshwa na "UHUNI" unaofanywa na sisiemu pale "PATAKATIFU PA PATAKATIFU"...aka.. mjengoni???... KIFANYIKE NINI ILI UWEZE KULIELEWA HILI "JAMBO KUU WALOFUNULIWA HATA WATOTO WADOGO NA KUFICHWA KWA WAFALME NA MAJEMADARI WAKUU??.... NI UHURU WA KUONGEA NA MAONI YANGU TUUU YASOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE
   
 6. S

  Selemani JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Chief--Slaa ni chaguo la Allah sio? Haya bwana. Na una uhakiki kabisa? Nadhani ungesema kwamba I pray to Allah kwamba Slaa awe chaguo la waTanzania ingekuwa sawa zaidi. My 2 cents. Nobody knows what God's choice for Tanzania presidency.
   
 7. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  TandaleOne, Jey Keyi, Malaria Sugu, na wengine wanaofanana na hao wote ni vibaraka ambao wanatumika kuupotosha umma na kwa kuwa wanaowatuma wanashikilia dora wanatumia kila mbinu kufanikisha malengo yao maovu kwa kupitia vyombo vya habari, propaganda chafu kama walivyofanya 2005.

  Kwa bahati mbaya kila janja wanayotumia inawaongezea umaarufu wale waliotarajiwa kuchafuliwa kutokana na ukweli kwamba mwaka huu wamekosa ushawishi wa vyombo vya habari kama walivyofanikiwa 2005 na kwa kuwa wigo wa kupashana habari umeongezeka; internet, e-mails na public forums ni changamoto mpya ambayo hawakutarajia inaweza kuwa na ushawishi wa kiasi hiki.

  Karata yao sasa ni kutumia nguvu na kuwatisha wapiga kura hasa vijijini ili wasithubutu kulinda kura zao zisiibiwe. Hii ikishindwa watakimbia nchi mmoja mmoja
   
 9. k

  kiparah JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hivi Daily news linamilikiwa na nani vile? halafu kama vile umechukua sehemu tu ya huo utafiti, mbona hujauweka ule wa Daily News Online Edition? ambao waliamua kuuchakachua baada ya kuona maji ya shingo. Dr. Slaa is our new president, PERIOD.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tandale one. Ni kweli kuwa watu wenye ID zaidi ya moja walipiga kura za maoni humu JF, lakini watu hao(wenye ID zaidi ya moja) wote walimpigia kura Kikwete na ndio maana angalau amepata hizo kura chache alizoambulia.
  Vinginevyo angepata 0%
   
 11. p

  pierre JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DR.SLAA ANAKUBALIKA KAKA.Nilipata maoni kutoka kwa Bibi yangu kijijini akinieleza kuwa kuna mgombea urais amefika kijijini kwao ndio wanamtaka ila amesahau jina lake,nikamwuliza Kikwete akanijibu hapana.Alichonihakikishia ni kuwa huyu mgombea ameteka mioyo ya wanakijiji wote kuanzia mtoto hata wazee.Kaka kubali matokeo.
   
 12. fige

  fige JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaomba utafiti tofauti kama upo ,kama haupo basi hatuna haja ya ku challenge bila data.
   
 13. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  The ishu si utafiti tofauti bali validity ya utafiti uliopo.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  "TUTAFAKARI TUCHUKUE HATUA SAHIHI NA TUKAPIGE KURA"

  1.Rais wa kwanza duniani kudanganywa vibaya mno na wasaidizi wake
  2.Rais wa kwanza kuwa na rekodi ya kuanguka anguka mbele ya kadamnasi
  3.Rais wa kwanza duniani kufanya safari nyingi za nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakaini
  4.Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hajui umaskini wa watu wake unatokana na nini.
  5. Rais wa kwanza duniani kuchakachuliwa mafuta kwenye gari yake ikazima barabarani
  6. Rais wa kwanza anaechukulia wingi wa magari kama kipimo cha maisha bora!
  7. Rais wa kwanza duniani anaepata ulinzi wa nguvu za Giza.(mnajimu)
  8. Rais wa kwanza aliyesema watoto wadogo wa shule kupata mimba ni kiherehere chao....
  9. Rais wa kwanza anayeogopa mafisadi.
  10.Rais wa kwanza duniani aliyetumia mabango yote ya biashara nchini kwake kujinadi wakati wa kampeni mpaka picha za kampeni
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  TandaleOne,
  Mkuu wangu hivi hata unaposimama peke yako ktk hoja huoni kwamba wengi wanamuunga mkono Dr.Slaa pamoja na kwamba unajaribu sana kutafuta sababu?.. iweje leo hii ktk mada zako zote unapata ushindani mkubwa na pengine huna hata Utetezi bado unafikiria kwamba kuna mchezo unafanyika.

  Mkuu wangu, mwaka 2005 wengi ya hawa watu walishindwa ktk kura za maoni kwa JK ktk tovuti ya Uchaguzi ambayo nadhani ilikuwa ikiendeshwa na hawa hawa vijana wa JF. Wengi hawakuamini pia matokeo yake lakini siku ya siku JK aliibuka mshindi kama ilivyokuwa imewekwa. Na hakika wananchi wengi walimchagua JK kwa sababu walifiikiria atakuja ondoa yote ya Mkapa kama alivyowaahidi wapiga kura. Siku ya kwanza tu madarakani akaanza kuwakana na kusema ataendeleza ya Mkapa na ndipo wananchi walipogundua wamepigwa changa la macho..

  Nitakwambia tatizo kubwa la JK ni kuwabeba Mafisadi, kukubali kuendeshwa na Lowassa ambaye alimfungia gunia la baraza la mawaziri lote bomu. Leo tena anaendelea kumkumbatia Lowassa kuchagua hata wagombea wa Ubunge ambao wengi wake ni bomu. Ushindi wa JK utakuwa mgumu sana kwanza hakuna dalili, na kama nilivyowahi kusema kumshinda JK ni swala linalowezekana kabisa kwani CCM wameshindwa kuwaletea wananchi mafanikio. Leo hi wananchi wamemchoka JK kama walivyomchoka Mkapa awamu ya pili. Na kibaya zaidi mahesabu ya CCM pengine ilikuwa JK kuwa rais wa awamu moja ili Lowassa achukue nafasi baada yake.
  Mwenyezi Mungu kapindua kibao..
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwani gazeti lako la uhuru au mzalendo limezuiwa na nani kuweka poll?
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tandaleone ni kweli cnn hawawezi kuongelea ucjhaguzi katika nchi na vyama vya siasa visvyokuwa na no "political accountability" kama Tanzania na CCM. As long as obsolete radar and Richmond suspects are still in the helm of the ruling party nad the country's politics Tanzania can forget about intrenational coverage.

  Like Kenya, the international press will come in once the people's power takes control in ousting fisadis' and their puppets like TandaleOne and others
   
 18. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Utafiti umekamilika.That wa theft kwa walionunua gazeti kwa kile kichwa cha habari.Watanzania tutalala daima na siasa za uchochoroni.
   
 19. M

  Mutu JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  • Daily News walimkubali kwa 60%
  • Synovate wakana madai ya CHADEMA kumpa 45%
  WAKATI kampuni ya kibiashara inayojihusisha na tafiti ya Synovate Limited ikikanusha taarifa za kubaini kwamba mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa sasa anakubalika zaidi, Watanzania wanaotumia mitandao wamempa mwanasiasa huyo asilimia kubwa ya ushindi kulinganisha na wagombea wengine.

  Ufuatiliaji wa Raia Mwema, katika mitandao mbalimbali ukiwamo ule wa gazeti la Serikali la Daily News (Daily News Online Edition) na mtandao maarufu kwa mijadala wa Jamiiforums unaonyesha kwamba Dk. Slaa anakubalika zaidi katika mtandao kuliko wagombea wengine akiwamo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

  Hata hivyo, kumekuwa na angalizo katika mitandao kwamba si Watanzania wengi wanaotumia mitandao hata kama kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mtandao kupitia simu za mikononi, hoja ambayo bado inaweza kutoa taswira tofauti katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, kutokana na wapiga kura wengi kuishi vijijini na wanaoishi mijini kutofahamu chochote kuhusu mtandao kama anavyosema na mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamiiforums:

  “Ingekuwa JF (Jamiiforums) inasomwa na asimilia 50% tu ya Watanzania wote, basi, Dk. Slaa angepita kiurahisi sana. Lakini kwa kuwa wengi hawapiti humu inabidi juhudi za ziada zifanyike kushinda”.

  Kura za maoni zilizokuwa zikiendeshwa na Daily News zikiwa na swali: ‘Will Dr. Slaa win the presidential race? ‘ (Je, Dk. Slaa atashinda urais?) zilionyesha kwamba kati ya watu 161 wa mwanzo waliopiga kura walionyesha kumpa Dk. Slaa asilimia 60.87 na ‘Hapana’ walikuwa asilimia 28.57, kabla ya kura hizo kusitishwa, kutokana na taarifa za kuwapo hofu ya ‘uchakachuaji’ uliodaiwa kufanywa na wafuasi au wapinzani wa Dk. Slaa.

  Kwa upande wa mtandao wa Jamiiforums, zaidi ya watu 6,420 wamepiga kura hizo za maoni na kuonyesha kwamba Dk. Slaa amekubalika kwa watu 4, 895 sawa na asilimia 76.25 akifuatiwa na Kikwete ambaye anaonekana kukubalika kwa watu 779 katika mtandao huo, sawa na asilimia 12.13 akifuatiwa kwa karibu zaidi na Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 448 (6.98%) wakati mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akikubalika kwa watu 205 (3.19%) na Mutamwega Mugahywa wa TLP akikubalika kwa watu 93 (1.45%).

  Mwazilishi wa mada hiyo ya kura za maoni aliweka swali “Je,Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?” Kabla hata ya majina ya wagombea kutangazwa na yeye mwenyewe kutangaza kuwania nafasi hiyo, Dk. Slaa alikuwa akitajwa kuwania nafasi hiyo na orodha ya majina kubandikwa mtandaoni badaa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza orodha ya wagombea hao.

  Wachangiaji wengi katika mtandao huo wa Jamiiforums ambao baadhi ya watu wanautuhumu kupendelea wapinzani, wamekuwa wakitoa sifa kuu za mtu anayestahili kuwa Rais wa Tanzania na kumchambua Kikwete kuwa amepoteza sifa za kuendelea na nafasi hiyo kutokana na kushindwa kupambana na ufisadi kikamilifu kama alivyoahidi wakati akiingia madarakani mwaka 2005.

  Miongoni mwa sifa walizoanisha katika mtandao huo ni pamoja na kuwa Rais ajaye anatakiwa awe ni msomi, mkimya, mchapa kazi, hana makundi na asiye na chembe ya ufisadi.

  Kabla ya majina ya wagombea kutangazwa, wachangiaji waliwataka wagombea wa Upinzani mwaka 2000 na 2005 wasijitokeze tena mwaka huu akiwamo Freeman Mbowe wa CHADEMA, Lipumba wa CUF, Augutine Mrema wa TLP na John Cheyo wa UDP kwa maelezo kwamba matokeo ya nyuma yanaonyesha kwamba hawana jipya mwaka huu.

  “Wanachotakiwa kukifanya sasa hivi ni kumchagua mtu tofauti kabisa. CCM hawawezi kubadilika. Rais ni nafasi ya Slaa sasa kwa ajili ya kusafisha na kuziba mianya ya ufisadi mkubwa. Baada ya hapo tunaweza kuchagua Rais mchumi ili ajenge uchumi wa nchi. Kwa sasa lazima tuondoe ufisadi kwanza, CCM hawawezi kuuondoa.

  “Kikwete alisema anawajua wala rushwa, wauza madawa ya kulevya, wezi wa EPA waliorudisha fedha na wale wahujumu wa Bandarini lakini kashindwa kuwataja wala kuchukua hatua ilhali yeye tumempa mamlaka yote kikatiba ili ailinde nchi hii na mali zake.

  “Slaa ni mzalendo wa kweli maana pamoja na kuwa hana mamlaka ya kuwafanya lolote mafisadi lakini kawataja hadharani bila woga au kuumauma maneno ingawa anajua hatari inayomkabili kupambana na watu wa aina hiyo. Huyu akipewa mamlaka ya kuongoza nchi mafisadi, wezi wa mali za umma nk, itabidi wakajichimbie makaburi wajizike wenyewe. Slaa ndio Rais anayefaa kwa wakati huu tulionao,” anasema mchangiaji mmoja wa Jamiiforums.

  Baadhi ya vyombo vya habari wiki hii vilimnukuu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisema kuwa CHADEMA ina matokeo ya kura za maoni za Synovate yanayoonyesha kuwa Dk. Slaa anakubalika kwa asilimia 45 akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 41, kauli iliyowalazimu Synovate kukanusha.

  Akizungumza na waandishi wa habari juzi Jumatatu, Meneja wa Synovate Limited, Aggrey Oriwo alisema taarifa hizo ni za kughushi, hazina ukweli wowote na zinaupotosha umma kwa kuwa hawajawahi kufanya utafiti wowote unaohusu kukubalika kwa wagombea wa urais.

  Oriwo alisema kwa kawaida kampuni yao hufanya utafiti wa hali ya kisiasa kila baada ya miezi mitatu na kwamba wanatarajia kufanya hivyo kabla ya Oktoba 31 na kutoa taarifa yao, kauli iliyotolewa pia na Taasisi ya Mpango wa Utafiti na Elimu Demokrasia Tanzania (Redet), ambao nao wanatarajia kufanya utafiti wa mgombea anayekubalika.

  Source: Raia Mwema
   
 20. M

  Mutu JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya jamiiforums imenukuliwa
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...