Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 236
Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima
* Yumo Ridhwan Kikwete, Marmo, Gavana Ndulu, Dk Kimei
* Maelfu waachwa 'kwenye mataa'
* Orodha yabanduliwa ghafla
Kashfa ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu muhimu nchini imezidi kushamiri ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao, akiwemo pia motto wa Rais Kikwete, Ridhwan Kikwete, Raia Mwema limebaini.
Uchunguzi wa Raia Mwema katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwemo mikoa ya ya kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, unaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya maeneo vigogo hao wamekuwa wakinunuwa kwa fedha taslimu na baadhi ya maeneo wamekuwa wakijitokeza na kugawiwa na watendaji wa halmashauri na manispaa za maeneo husika, huku maelfu ya wananchi wa maeneo husika wakinyimwa pamoja na kuwa wa mwanzo kuomba na kulipia gharama za fomu ambazo hutumika kupimia viwanja.
Mfano wa hivi karibuni ni mkoani Arusha ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira tata huku maelfu ya wananchi wa mkoa huo walioomba akijikuta wakiwa hawamo katika orodha ya watu waliopata viwanja iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo na kubanduliwa baada ya wananchi kuanza kulalamika.
Sakata hilo la aina yake limetokea katika halmashauri ya Arusha Vijijini mkoani Arusha, ambako Idara ya Ardhi ya Halmashauri hiyo ilikusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi, wakiwemo makabwela, kwa ajili ya kupimiwa viwanja katika eneo la Burka ambavyo hata hivyo vimegawiwa kwa vigogo.
Mbali na Ridhwan, vigogo wengine waliogawiwa viwanja vya Burka huko Arusha Vijijini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri ..
Habari zaidi katika RAIA MWEMA ya leo.