RAIA MWEMA: Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

* Yumo Ridhwan Kikwete, Marmo, Gavana Ndulu, Dk Kimei
* Maelfu waachwa 'kwenye mataa'
* Orodha yabanduliwa ghafla

Kashfa ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu muhimu nchini imezidi kushamiri ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao, akiwemo pia motto wa Rais Kikwete, Ridhwan Kikwete, Raia Mwema limebaini.

Uchunguzi wa Raia Mwema katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwemo mikoa ya ya kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, unaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya maeneo vigogo hao wamekuwa wakinunuwa kwa fedha taslimu na baadhi ya maeneo wamekuwa wakijitokeza na kugawiwa na watendaji wa halmashauri na manispaa za maeneo husika, huku maelfu ya wananchi wa maeneo husika wakinyimwa pamoja na kuwa wa mwanzo kuomba na kulipia gharama za fomu ambazo hutumika kupimia viwanja.

Mfano wa hivi karibuni ni mkoani Arusha ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira tata huku maelfu ya wananchi wa mkoa huo walioomba akijikuta wakiwa hawamo katika orodha ya watu waliopata viwanja iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo na kubanduliwa baada ya wananchi kuanza kulalamika.

Sakata hilo la aina yake limetokea katika halmashauri ya Arusha Vijijini mkoani Arusha, ambako Idara ya Ardhi ya Halmashauri hiyo ilikusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi, wakiwemo ‘makabwela’, kwa ajili ya kupimiwa viwanja katika eneo la Burka ambavyo hata hivyo vimegawiwa kwa vigogo.

Mbali na Ridhwan, vigogo wengine waliogawiwa viwanja vya Burka huko Arusha Vijijini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri…………………………..

Habari zaidi katika RAIA MWEMA ya leo.
 
Duh!! Hawa watu huwa hawajui kama kuna Mungu Mwenyezi? Hawajui kwamba ipo siku umma utashika nchi na wao kujikuta katika hali mbaya sana? Historia poipote duniani inaonyesha hivyo...
 
Nikiwatukana ntakua nimewapa cheo bora nikae kimya tu nife kimya kimya
 
Halafu eti wanasema wanaasisi amani na kututaka kudumisha amani. Hakyanani vile haya majitu yanatia hasira mno haya
 
FOMU ILIKUA SH 10000 WATU WALIOCHUKUA FOMU 12700 VIWANJA 700 KILA SQUARE METER SH 8500.WALIOPATA MAWAZIRI MAKATIBU WATOTO WA VIGOGO MADIWANI WA CCM.HATA WAKATI WA KUJAZA FOMU SIFA MOJAWAPO UWE MKEREKETWA WA CCM!wana jf tuchukue hatua gani?MIMI NA WEWE 20 x40 sq meter sh 9M tutaweza huku yule mgiriki kafidiwa kwa kodi zetu???
 
Mwana JF aliye arusha ai post list ya waliopata tuone hatua ya kuchukua!tena walitaimu karibu na election ndio wakatoa fomu sh 20 000 zinaniuma jamani
 
:doh::A S angry::A S angry::doh::doh::A S angry: :A S-cry: Nikiongea nitatukana Aaargh, hakuna emotions za kutosha kuonyesha hasira zangu w*****$####, !@*****, testa di merda,
 
fomu ilikua sh 10000 watu waliochukua fomu 12700 viwanja 700 kila square meter sh 8500.waliopata mawaziri makatibu watoto wa vigogo madiwani wa ccm.hata wakati wa kujaza fomu sifa mojawapo uwe mkereketwa wa ccm!wana jf tuchukue hatua gani?mimi na wewe 20 x40 sq meter sh 9m tutaweza huku yule mgiriki kafidiwa kwa kodi zetu???

uvundo kama huu umetokea hata huko kongwa-dodoma, watu wameomba viwanja toka 2004 na kulipishwa shs. 100,000= kwa plot moja ya medium size, lakini hadi leo wanapigwa dana dana.

Sababu kuu wanayo dai watu wa ardhi pale kongwa niza kipuuzi tu na haziingii akilini... Kama wameshindwa kuwapa watu hivyo viwanja ni bora wawarudishie fedha zao.

Nchi hii nadhani kila kitu ni siasa tu, kwani cha ajabu viongozi wanapewa viwanja na wanajenga ila mwana-kongwa wa kawaida toka 2004 hadi leo ni blaa blaa tu.
 
Wana JF mimi ni mmoja wa watu walio apply hivyo viwanya,kwa kweli inaumiza sana kuona KIGOGO MMOJA ANACHUKUA VIWANJA (KUMI) 10 MWENYEWE,wananchi wengine wanakosa hata kimoja,inasikitisha na inaumiza sana sana sana.
 
Hizi ni sababu moja wapo zinazowafanya wakumbatie uongozi wa nchi; wanajua siku wakitoka, kitakachowafuata kiko wazi kabsa...:A S angry:
 
Ndiyo walivyo hawamafisadi nasikia hata karume alipokaribia kumaliza muda wake amegawa kwa ndugu zake viwanja, hotel vilivyo kuwa vinamilikiwa na serikali ya Zanzibar
 
uvundo kama huu umetokea hata huko kongwa-dodoma, watu wameomba viwanja toka 2004 na kulipishwa shs. 100,000= kwa plot moja ya medium size, lakini hadi leo wanapigwa dana dana.

Sababu kuu wanayo dai watu wa ardhi pale kongwa niza kipuuzi tu na haziingii akilini... Kama wameshindwa kuwapa watu hivyo viwanja ni bora wawarudishie fedha zao.

Nchi hii nadhani kila kitu ni siasa tu, kwani cha ajabu viongozi wanapewa viwanja na wanajenga ila mwana-kongwa wa kawaida toka 2004 hadi leo ni blaa blaa tu.
Hapo kwenyeRED color, wanatoa sababu gani, hebu tujuze ili tujue namna ya kuwabana
 
Hapo kwenyeRED color, wanatoa sababu gani, hebu tujuze ili tujue namna ya kuwabana

Sababu kubwa wanayodai ni kuwa, bado hawajapata fungu la kuwalipa wale wanao-yamiliki maeneo kwa sasa (may be compasation). Wanadai iwapo Hazina au mkoa watatoa hilo fungu basi ndo wataanza kugawa hizo plot, kwani zilishapimwa tayari.

Swali kwetu sisi wa Kongwa ni je, huo Mkoa au Hazina toka 2004 hadi sasa bado haujapata fedha ya kuwalipa wamiliki wa maeneo hayo?
 
Ethics za wanahabari zetu ziko wapi? Ukisoma unaona hii makala ni ya kichochezi.

Mwandishi anadrop names za Jakaya. Ridhiwani, Marmo bila kuweka vielelezo, sources, hata quotes za watendaji ili kutupa evidence sisi wasomaji. In this way, anybody with a big chunk of land, can be me or you we will stand to be accused.

Kitu kibaya zaidi, mwandishi was betting on ignorance of waTanzania wa kutoweza kuona mapungufu ya hii makala. And sadly great thinkers wa Jambo Forum fell into Mwandishi's trap. Hii makala is a prime example ya kutumia media kueneza chuki dhidi ya watu wengine. What else can you call this piece?
 
vigogo wajipa ardhi kwa fujo nchi nzima

* yumo ridhwan kikwete, marmo, gavana ndulu, dk kimei
* maelfu waachwa 'kwenye mataa'
* orodha yabanduliwa ghafla

kashfa ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu muhimu nchini imezidi kushamiri ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao, akiwemo pia motto wa rais kikwete, ridhwan kikwete, raia mwema limebaini.

Uchunguzi wa raia mwema katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwemo mikoa ya ya kanda ya kaskazini, dar es salaam na mkoa wa pwani, unaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, baadhi ya maeneo vigogo hao wamekuwa wakinunuwa kwa fedha taslimu na baadhi ya maeneo wamekuwa wakijitokeza na kugawiwa na watendaji wa halmashauri na manispaa za maeneo husika, huku maelfu ya wananchi wa maeneo husika wakinyimwa pamoja na kuwa wa mwanzo kuomba na kulipia gharama za fomu ambazo hutumika kupimia viwanja.

Mfano wa hivi karibuni ni mkoani arusha ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira tata huku maelfu ya wananchi wa mkoa huo walioomba akijikuta wakiwa hawamo katika orodha ya watu waliopata viwanja iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo na kubanduliwa baada ya wananchi kuanza kulalamika.

Sakata hilo la aina yake limetokea katika halmashauri ya arusha vijijini mkoani arusha, ambako idara ya ardhi ya halmashauri hiyo ilikusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi, wakiwemo ‘makabwela', kwa ajili ya kupimiwa viwanja katika eneo la burka ambavyo hata hivyo vimegawiwa kwa vigogo.

Mbali na ridhwan, vigogo wengine waliogawiwa viwanja vya burka huko arusha vijijini ni pamoja na aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, philip marmo, na naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (tamisemi) aggrey mwanri…………………………..

habari zaidi katika raia mwema ya leo.

he huyu mwandishi hakupewa nini? Nasikkia huko arusha kuna wandishi wa habari maarufu wamepewa ili wasichonge!
 
Mwana JF aliye arusha ai post list ya waliopata tuone hatua ya kuchukua!tena walitaimu karibu na election ndio wakatoa fomu sh 20 000 zinaniuma jamani

kWELI KABISA IWEKENI, NASIKI NI HAO HAO TU, KUNA MTU YUKO ARUSHA ALINIPA BAADHI. NASIKIA WALIAMUA KUTOA MAJINA BAADA YA CCM KUSHINDWA KWENYE UCHAGUZI MKUU MAANA WALIJUAVIJANA WA CHADEMA WATAWAMALIZA, NA LOWASA ALISHIKA ENEO KUBWA SANA
1.LOWASA WIWANJA 6
2.LIZIWANI jk
3.RITHA MLAKI VIWANJA 6-KWA MAJINA YA FAMILIA
4.SOPHIA SIMBA
 
ethics za wanahabari zetu ziko wapi? Ukisoma unaona hii makala ni ya kichochezi.

Mwandishi anadrop names za jakaya. Ridhiwani, marmo bila kuweka vielelezo, sources, hata quotes za watendaji ili kutupa evidence sisi wasomaji. In this way, anybody with a big chunk of land, can be me or you we will stand to be accused.

Kitu kibaya zaidi, mwandishi was betting on ignorance of watanzania wa kutoweza kuona mapungufu ya hii makala. And sadly great thinkers wa jambo forum fell into mwandishi's trap. Hii makala is a prime example ya kutumia media kueneza chuki dhidi ya watu wengine. What else can you call this piece?

evidence za nini hapa, wewe elewa hivyo, kuna uhuni mkubwa sana katika mradi huo, hivi waweza kunipatia kigezo cha kupatiza riziwani kiwete kiwanja ukamuacha mmasai wa pale arusha? Oh samahani mtasema mbaguzi
 
Hivi hawa Wanachi si Wakalalamike kwa kupitia Mwakilishi wao waliyemchagua akawawakilishe
 
uvundo kama huu umetokea hata huko kongwa-dodoma, watu wameomba viwanja toka 2004 na kulipishwa shs. 100,000= kwa plot moja ya medium size, lakini hadi leo wanapigwa dana dana.

Sababu kuu wanayo dai watu wa ardhi pale kongwa niza kipuuzi tu na haziingii akilini... Kama wameshindwa kuwapa watu hivyo viwanja ni bora wawarudishie fedha zao.

Nchi hii nadhani kila kitu ni siasa tu, kwani cha ajabu viongozi wanapewa viwanja na wanajenga ila mwana-kongwa wa kawaida toka 2004 hadi leo ni blaa blaa tu.

Inauma, hata hivyo, kumbuka SIASA siyo uongo isipokuwa WANASIASA ndo waongo
 
Back
Top Bottom