Raia Mwema: Tundu Lissu atoswa rasmi

Raia Mwema: Tundu Lissu atoswa rasmi

Hata mimi sikumuelewa Lisu alipoanza kutofautiana na msimamo wa viongozi wenzake.

..Lissu yuko sahihi.

..Kasi ya Maridhiano ni ndogo.

..Na ni ndogo kwasababu CCM hawana nia ya dhati ktk maridhiano.
 
Umetuacha Imara, Tanzania Salama, Mungu akulaze mahala pema peponi
Screenshot (54).png
 
Lissu na Mdude hawafai kuendelea kuwepo CHADEMA kwasababu wameshindwa kusoma alama za nyakati kwamba sasa ni muda wa kulamba asali. Namtupia lawama Mbowe kwa kutaka kumaliza buyu zima la asali mwenyewe.
Nenda home kwake mkajifungie chumbani nawe akulambishe asali kiroho safi.
Si unataka asali nenda ukapakuliwe saizi yako utakayo.
 
Acheni kuchochea migogoro, hata Msigwa mlisema hivo hivo alivopishana na wenzake hadharani. Kwenye chama hamuwezi wote kuwa na mawazo sawa na hii ndio demokrasia. Hakuna mgogoro Wala Nini kama mnasubiri Chadema kupasuka mnapoteza muda tu.
Fisi hao wanatembea nyuma ya binadamu wakisubiria mkono uanguke.... Watasubiri sana.
 
Kupoteza muda kwa mambo yasiyo halisia ni kujitoa ufahamu.

Lisu ametoswa na nani?

Lisu ametoswa katika nini?

Kama ametoswa, hiyo mikutano anayoifanya anaifanya kwa umbrela ya chama gani?

Kati ya tasnia iliyokosa watu wenye weledi, ya kwanza ni tasnia ya habari. Wamebakia kama wambea wa mitaani. Wanashindwa kufuatilia mambo ya maana kama report ya CAG, wanabakia kuokoteza umbea. Analysis hakuna, reasoning zero, weledi hakuna. Ndiyo maana watu wakitaka kupata habari za uhakika, wanatafuta BBC, Aljezira, CNN, wakati jambo limetokea Tanzania.
Kuelekea uchaguzi 2015 gazeti la Raia Mwema lilipoteza kabisa uweledi wake na kuanza kuwa kituko. Kabla ya hapo lilikuwa gazeti makini kabisa likisheheni makala za kuhabarisha, kuelimisha na uchambuzi wa kina kisiasa na kijamii. Baada ya kuingiliwa na kirusi cha uchaguzi idadi kubwa ya wale wanasafu waliacha kabisa kufanya uchambuzi na kugeuka wapambe wa mgombea wa mfumo. Bila shaka kuna kitu kilifanyika wakati huo na baada ya hapo gezeti hili halikuweza tena kurejea katika hali yake ya kabla ya 2015. Walibakia wanasafu kama wawili hivi ambao, bila shaka kutokana na ukongwe wao, mamlaka husika hazikuweza hata kupata ujasiri wa kujaribu kuwaingia. Binafsi nilikuwa msomaji wa Raia Mwema kila juma lakini tangu lilipokengeuka sijalisoma tena hadi leo. Pamoja na kwamba hadhi yake imeshuka sana, bado kuna uwezekano kuwa kilichofanyika 2015 kinaendelea kufanyika hata leo. Kusema kweli kwa jinsi "uchawa" unavyothaminiwa na kuendekezwa katika siasa zetu sasa sehemu kubwa ya matumizi mabaya ya fedha yanayoibuliwa na GAG inachangiwa na ununuzi wa "chawa" kwa gharama yoyote! Na kwa bahati mbaya, tofauti na kipindi kile kwa sasa umbilikimo katika siasa zetu na vyombo vya habari nao umeshika kasi. Utadhani watu hawajaenda shule kabisa! Kutokana na umbilikimo huo tumefikia mahali hata gazeti kama Raia Mwema lililopata kuheshimika sana katika nchi hii sasa linadiriki kuandika habari za kizushi, umbea na uchochezi! Hili halijatokea kwa bahati mbaya au kukosa uweledi, la hasha. Ni sehemu ya ule ule uovu ulioliingiza taifa hili katika giza kwa miaka zaidi ya mitano. Ushetani huo bado upo na utaendelea kuwepo kwa muda mrefu.
 
Mzee wa tutashitakiwa MIGA
Hivi unadharau MIGA? Ungekuwa na akili ungekwenda ku GUGO ukajuwa uhusiano wa MIGA, CISD na World Bank. Ungekuwa na akili ungetafuta sababu kwa nini moja ya ndege zetu kwa nini zinashikiliwa huko Netherlands na tuna kesi ngapi zinaendelea CISD kwa kupuuza ushauri wa Lissu kuhusu MIGA
 
Hivi unadharau MIGA? Ungekuwa na akili ungekwenda ku GUGO ukajuwa uhusiano wa MIGA, CISD na World Bank. Ungekuwa na akili ungetafuta sababu kwa nini moja ya ndege zetu kwa nini zinashikiliwa huko Netherlands na tuna kesi ngapi zinaendelea CISD kwa kupuuza ushauri wa Lissu kuhusu MIGA
Huyo Etwege anajua hicho kibwagizo cha MIGA tu,katika IDs zake zote lazima amhusishe Lissu na MIGA mwenyewe anajiona amepost madini
 
Lissu ni typical Magufuli katika kusema hovyo sema tofauti Lissu yuko upinzani na hajawahi kuwa Rais. Wote wawili ni hatari kuwapa madaraka ya juu kabisa ya kuongoza nchi. Tumejifunza kwa Magufuli tusirudie makosa hata kama upinzani watachukua nchi lakini LISSU hafai kuwa Rais.

Post zangu za nyuma nimemtetea sana Lissu kwa umahiri wake kwenye sheria za madini na mazingira, nimemtetea wakati Magufuli ananyima haki zake baada ya kumpiga risasi 16
Unamtazamo kama wangu... pamoja nakuisapoti chadema ila tundu lisu si presidential material
 
Xhochote kitokeacho kwa sasa ni jambo la kheri Kwan MAGUFILI ajishajiletea umauti mwenyewe!!!!

Celebrate, celebrate, celebrate....tunalala, kuongea, kuwasema, kukosoa, kushauri kwa aman kwan jini magufuli alishatoweka

Team magu kamfufueni MUNGU WENU chattle
Unajikaza upepo umeshabadilika tunawasubiri konani
 
Back
Top Bottom