Tatizo ni kuwa kila mtu anaangalia tumbo lake. Hii iaashiria kuwa hakutakuwa na Katiba Mpya hapa TZ kama hatutakuwa makini.
Katika chadema kuna makundi mawili
1. Ni akina Mbowe na Lema wake, wenyewe wanahangaika na UBUNGE. Hivyo Maridhianao yalikuwa Samia aachiwe Urais na wao waachiwe ubunge. Wakaona kila kitu safi ndiyo maana unasikia kila siku kumpamba Samia. Hata mabaya yanayoonekana kwa awamu ya 6 wao kimya. Kikibwa wamehaidiwa Ubunge (Nusu Mkate).
2. Tundu Lissu hataki ubunge bali URAIS tu. Hivyo yeye anaona hakuna haja ya kuhaidiwa ubunge bali kungekuwa na kuhaidiwa Urais, yeye kiu yake ingepona. Sasa wenzake wamemtupa maana alitegemea nusu nyingine ya mkate iwe Samia kumwambia Lissu kuwa nitakuachia kiti.
Huo ndiyo mgawanyiko wa Chadema ambao akina
Erythrocyte ,
Retired Mmawia brazaj hawaelewi mambo. Wanaburizwa tu kwa maslahi ya wachache.
Je, kwa mwendo huu, kutapatikana Katiba isiyokuwa na maslahi binafsi?