Raia Mwema: CHADEMA iache kujidanganya

Raia Mwema: CHADEMA iache kujidanganya

Mujumba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
853
Reaction score
306
"CHADEMA isichezee wala kuchukulia kiurahisi wakati wake huu wa kupendwa na wananchi. Isije kujidanganya kuwa itaendelea kupendwa vyovyote vile. Viongozi wake wasije kujivika kilemba cha ukoka wakiamini kuwa wanapendwa kwa sababu wao ni vijana, wanazungumza vizuri, wanavaa magwanda vizuri n.k.

Wajue kabisa wanapendwa kwa sababu watu wameamua kuikataa CCM “na mambo yake yote”. CHADEMA hawawezi kudai kuwa ni haki yao kupendwa au kuungwa mkono kwani historia ina mafunzo mazuri kweli – si hoja mtawala anapendwa vipi, siku moja anaweza kuchukiwa. " Gazeti Raia Mwema ikiandikwa na LULU WA NDALI MWANANZELA
 
mmmh, ok.sasa mkuu hoja/makala yenyewe ndo imeishia hapo au??!!......
 
Yap the guy is right...kuna wana ccm leo hii wakati wa uchaguzi wanaichagua chadema hilo hata lowasa alisema alivyokua arusha.. so cdm inaweza isiwe necessarily inapendwa sana but kikubwa ni kua ccm inachukiwa so wanachama wa ccm ambao hawapendi mwelekeo wa chama chao kinavyokwenda ndio hao wanaoipigia kura cdm.

Ikifika 2015 hao wanachama wa ccm wakawa wameridhishwa na mwelekeo wa ccm wakaamua kukupigia kura chama chao basi cdm itapoteza kura nyingi ambazo imekua ikizipata sasa hivi.

cdm ijitahidi wanachama wake wajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura kwa sababu inapokuja kwenye uandikishaji wa kupiga kura ccm wana watu wengi zaidi ya cdm.
 
Hilo linajulikana Mkuu.. Kwani hata CCM ilikuwa inapendwa.. Ila baadae kikaja kuwaacha wananchi njia panda.. Wananchi wanakuwa na mapenzi kwa chama ambacho kinawacikiliza na kuwatumikia kadiri wananchi wenyewe watakavyo.. Kitakacholeta ustawi na maendeleo kwao wananchi..

Viongozi wa CDM wanalijua hili mkuu.. Wao ndio wanaleta ukombozi na kuhamisha utawala toka wa wachache na kurudisha kwa wananchi..
 
Kupendwa ni kupendwa tuu siyo lazima itawale milele mbona marekani kuna democrat na republic vinatawala kwa vipindi tofauti na havipendwi kwa wakati mmoja
 
Kwa maana hiyo, mwisho wa kuchukiwa CCM ndio pia mwisho wa kupendwa Chadema au? Naomba ufafanuzi.
 
Huo ni mtazamo wa mwandishi tu , amefanya research yeyote au mikutano ya arusha tu,,,
 
Chadema ndio meli yetu ya ukombozi, tusiizamishe kamwe bali tuiimarishe zaidi ili tufike paradise.
 
Na nani aliyekudanganya wananchi wanaipenda chadema? wanaoipenda chadema ni wafuasi wachache wanaifata kwa ukabila na udini wao.
 
"CHADEMA isichezee wala kuchukulia kiurahisi wakati wake huu wa kupendwa na wananchi. Isije kujidanganya kuwa itaendelea kupendwa vyovyote vile. Viongozi wake wasije kujivika kilemba cha ukoka wakiamini kuwa wanapendwa kwa sababu wao ni vijana, wanazungumza vizuri, wanavaa magwanda vizuri n.k.

Wajue kabisa wanapendwa kwa sababu watu wameamua kuikataa CCM "na mambo yake yote". CHADEMA hawawezi kudai kuwa ni haki yao kupendwa au kuungwa mkono kwani historia ina mafunzo mazuri kweli – si hoja mtawala anapendwa vipi, siku moja anaweza kuchukiwa. " Gazeti Raia Mwema ikiandikwa na LULU WA NDALI MWANANZELA

Hili ni kweli kabisa na mimi nimekuwa mstari wambele kudai dira na misimamo ya kiuendeshaji endapo chadema itachukua nchi.
Hilo hawana.
Mara nyingi Chadema wanafanya kazi kubwa kulaumu tu bila kutoa mipango mbadala.
Sitashangaa kama madudu yaliyoko CCM yana mizizi ile ile ndani ya CDM.
 
Ndio maana yake mkuu!!

Tujipange sasa!

Mkuu kama ndivyo basi future ya Chadema iko mashakani tena sana na hasa viongozi wasipokuwa makini. Kumbe Chadema inapendwa simply because wananchi wamekosa mbadala! Hii ni hatari kwa chama na kusambaratika kwake ni kufumba na kufumbua endapo CCM itafanya reshuffle ya uhakika kwenye mfumo wake.

Ni hatari kwa chama kupendwa kwa sababu ya wananchi kukosa "pa kukimbilia" badala ya kupendwa kwa sababu ya SERA zake.
 
"CHADEMA isichezee wala kuchukulia kiurahisi wakati wake huu wa kupendwa na wananchi. Isije kujidanganya kuwa itaendelea kupendwa vyovyote vile. Viongozi wake wasije kujivika kilemba cha ukoka wakiamini kuwa wanapendwa kwa sababu wao ni vijana, wanazungumza vizuri, wanavaa magwanda vizuri n.k.

Wajue kabisa wanapendwa kwa sababu watu wameamua kuikataa CCM "na mambo yake yote". CHADEMA hawawezi kudai kuwa ni haki yao kupendwa au kuungwa mkono kwani historia ina mafunzo mazuri kweli – si hoja mtawala anapendwa vipi, siku moja anaweza kuchukiwa. " Gazeti Raia Mwema ikiandikwa na LULU WA NDALI MWANANZELA

mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia chahe sana,kwa sababu hakuna sehemu ambapo cdm imelazimisha watu waipende au wawapende viongozi wao,na huwezi ukasema kuwa watu wanaipenda cdm kwa sababu wanaichukia ccm kwani kama ni hivyo basi vipo vyama vingi sana na vinashiriki kwenye chaguzi mfano ppt-maendeleo,tlp,udp,cuf nk.kwa nini visipendwe hivyo na badala yake ipendwe cdm?
Tujifunze kuwa wa kweli kwamba watu wamepima na kuona kuwa ni cdm ndicho kinabeba matumaini yao kwa sasa hivi,tusiwe watu wa kuumauma maneno.
 
Na nani aliyekudanganya wananchi wanaipenda chadema? wanaoipenda chadema ni wafuasi wachache wanaifata kwa ukabila na udini wao.

kwa ukabila na udini wako, wewe unaonekana ukitoka ccm utaenda utaenda cuf!
 
Na nani aliyekudanganya wananchi wanaipenda chadema? wanaoipenda chadema ni wafuasi wachache wanaifata kwa ukabila na udini wao.
well said
tatzo kenge wanaofuata mkumbo hawataki
tundu lisu ana dada yake mule amepewa kimagumash magumash,hatukatai mbunge kua na nduguye mbunge la hasha,swali ni jins walivopatikana kwa zengwe,
alipofarik marehem regia tunashangaa mrith wake chadema badala ya kumtoa kule moro wao wanakimbilia uchagan,
af jaman tuwe serious hili suala la kumpa mtu nchi nalo sio dogo hili??
Mtu kama mbowe ninampaje mamlaka ya nchi jaman?nimpe et kisa tuh anaweza kuzishupulia kesi za uozo wa mafisadi wa ccm au weledi wake wa uongoz na taadhima yake?
Chadema wana mengi ya kufanya ili kuqualify kuingia state house,wajipange had 2020/2025
ila kwa huu unaokuja waingize wabunge wengne wengi,then huo unaofuatia ndio tuangalie wako imara kias gan
waondoe ukabila,waondoe ukanda,waondoe udini n.k,ni vitu kama hivo vimeigharim cuf had kuporeza trust kwetu na kuonekana kama kibaraka
 
Mkuu kama ndivyo basi future ya Chadema iko mashakani tena sana na hasa viongozi wasipokuwa makini. Kumbe Chadema inapendwa simply because wananchi wamekosa mbadala! Hii ni hatari kwa chama na kusambaratika kwake ni kufumba na kufumbua endapo CCM itafanya reshuffle ya uhakika kwenye mfumo wake.

Ni hatari kwa chama kupendwa kwa sababu ya wananchi kukosa "pa kukimbilia" badala ya kupendwa kwa sababu ya SERA zake.

hili mimi siliafiki,kwani kama simply watu wanaipenda cdm kwa kukosa mbadala basi kwa nini isipendwe tlp,cuf au nccr?.Tusiwape wananchi level ndogo namna hiyo ya uelewa.Naamini kuwa si kukosa mbadala bali ni sera na mwelekeo wa cdm ndo unawafanya wananchi wazidi kuipenda cdm.
 
Ndali Mwananzela, kamanda wetu naona umeamua kufunguka.
 
"CHADEMA isichezee wala kuchukulia kiurahisi wakati wake huu wa kupendwa na wananchi. Isije kujidanganya kuwa itaendelea kupendwa vyovyote vile. Viongozi wake wasije kujivika kilemba cha ukoka wakiamini kuwa wanapendwa kwa sababu wao ni vijana, wanazungumza vizuri, wanavaa magwanda vizuri n.k.

Wajue kabisa wanapendwa kwa sababu watu wameamua kuikataa CCM "na mambo yake yote". CHADEMA hawawezi kudai kuwa ni haki yao kupendwa au kuungwa mkono kwani historia ina mafunzo mazuri kweli – si hoja mtawala anapendwa vipi, siku moja anaweza kuchukiwa. " Gazeti Raia Mwema ikiandikwa na LULU WA NDALI MWANANZELA

Hiyo sio fomula, inategemea ukiingia madarakani unasimama upande gani. Kumbuka maneno ya Baba yenu "Mkikaa mbali na wananchi, wananchi watawakataa" Viko vyama kwenye nchi zenye demokrasia nzuri na ya vyama vingi, vimekaa muda mrefu bila kuondolewa madarakani, mf: BDP Botswana, ANC Nk.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom