mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Na Lula wa Ndali Mwananzela
NILIPOANDIKA pendekezo hili wakati wa kampeni bila ya shaka watu walifikiria natupa dongo la kisiasa tu kama sehemu ya Operesheni ya kukataa mabadiliko feki. Nina uhakika wapo waliodhani kuwa nilitoa pendekezo la Lowassa kuiongoza Chadema wakati ule kama ngumi ya tumbo kwa uongozi wa Chadema hasa kwa vile nilishaonesha upinzani wangu dhidi ya kumpokea Lowassa na kumpatia mikoba ya kugombea urais kwa kupitia chama hicho.
Sikuwa ninatania. Siku za karibu na mara baada ya uchaguzi wa 2015 kumetokea baadhi ya viongozi wa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema kuwa mafanikio kiduchu yaliyotokea wakati wa uchaguzi ni matokeo ya ujio wa Lowassa Chadema. Imani hii imeanza kuaminika kiasi kwamba Lowassa anaanza kubebeshwa sifa zote kuwa kwa siku chache alizoweza kukaa Chadema na kuzunguka nchi nzima aliweza kuijenga Chadema kushinda wale waliokuwepo ndani ya chama hicho na kuenyeka kwa muda mrefu. Simulizi hili jipya lina lengo la kuendeleza kile kile kilichotokea wakati ule wa uchaguzi – kuhalalisha ujio wa Edward Lowassa – Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa zamani wa Monduli – Chadema baada ya jina lake kukatwa katika chama kilichomlea – cha Mapinduzi.
Kwamba, Watanzania watambue na kukubali kuwa Lowassa alikuwa ni mtaji mkubwa kwa Chadema. Na ushahidi pekee wanaoutoa ni kutuonesha tu kuwa idadi ya wabunge wa kuchaguliwa imeongezeka kidogo na wabunge wa upinzani wameongezeka kuliko Bunge la 2010. Kwamba, hata kushindwa kwao kufikia theluthi moja ya wabunge wote kwa kukosa majimbo machache ni ishara ya mafanikio ya ujio wa Lowassa. Kwamba, wakiwa na Lowassa wameweza kuchukua kwa mara ya kwanza uongozi wa Halmashauri za Jiji la Dar na kuweza kutoa mameya kitu ambacho hakikuwahi kudhaniwa kwa muda. Kwamba, wameweza kuchukua halmashauri za miji ya Iringa, Moshi, Mbeya, Tanga, na Arusha na kuongoza mitaa mingi.
Hili linaweza kuwa kweli kabisa. Lakini pia halielezei jinsi gani walipoteza pia Jiji la Mwanza, na mji wa Musoma na kuelekea kufutika kabisa katika kanda ya ziwa. Lowassa ni kweli aliweza kuwa mtaji na kama hii ni imani ya viongozi hawa na kuwa ndio ushahidi wa kazi yake kubwa basi hakuna njia nyingine ya kumzawadia au kuonesha kuwa wanaamini kweli isipokuwa kumpa uongozi wa chama.
Kama Mbowe na timu yake yote walivyofanya kazi kwa miaka yote hii hawakuweza kuliteka Jiji la Dar, na hawakuweza kuongeza idadi ya wabunge kwa kiasi hicho ni wazi Lowassa ni mtaji mkubwa zaidi. Na ukweli kuwa wanahusisha wabunge wachache waliowapata kuwa ni matokeo ya Lowassa na kazi yake kubwa basi hakuna namna isipokuwa kuonesha imani hiyo kwa vitendo. Kama Mbowe na uongozi wote wa Chadema wanaamini kwa dhati kabisa kuwa bila ya ujio wa Lowassa wangepoteza viti vingi zaidi vya ubunge na wasingeweza kupata mavuno manono waliyoyapata basi Lowassa ni kiongozi sahihi kabisa wa kuivusha Chadema kutoka ilipo sasa kuelekea kwenye mafanikio zaidi.
Vinginevyo ni lazima tujiulize ni kiongozi gani mwingine ndani ya Chadema mwenye ujiko, uwezo, uzoefu na maono ya kuliinua taifa anayeweza kushindana na Lowassa? Kama Mbowe mwenyewe aliona Lowassa ni mtu anayefaa kubeba bendera ya mabadiliko yeye hafai kuiongozi tena Chadema. Kama Lissu, Mnyika, Msigwa na wengine wote ambao walisimama nyuma ya Lowassa na kutubu makosa yao wenyewe na kumvisha kilemba cha ushujaa ni kitu gani zaidi wanahitaji kufanya isipokuwa kupiga magoti mbele yake na kujiweka chini ya uongozi wake?
Hii ndio njia pekee ya kuenzi mchango mkubwa ambao unadaiwa ulitolewa na Lowassa na ndiyo njia sahihi – yaani kumpa uongozi wa Chama ili akisuke na kukipanga vizuri zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa na ule wa wabunge 2019 na 2020 kwa mfuatano huo. Mbowe asipofanya hivyo na viongozi wengine wasiposhinikiza hili litokee wananchi ni lazima watafikia hitimisho moja tu la kuchefua- vyote hivi ni njia za kuhalalisha kitu ambacho walijua siyo halali; namna ya kuficha kosa kubwa kabisa la kisiasa lililofanywa na viongozi hawa.
Chanzo: Raia Mwema