Rahisi: Kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mahindi (Corn Oil)

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania !

Kwa wewe mzalendo au mpenda biashara nakusihi unaweza anzisha kiwanda cha mafuta ya kula kwa kuchakata mahindi kuwa mafuta.

Katika bidhaa hii mahindi ya njano ndio malighaifi pekee inayochakatwa na kuwa mafuta ya kupikia kwa kukamuliwa na mitambo.

NB

a) Mahindi yapo.
b) Ardhi ipo ukitaka kulima.
c) Mtaji ni mdogo sana kuanzisha na kukiendesha kiwanda.
d) Soko la mafuta ya kula / kupikia lipo.
e) Kazi ni kwako boss mtarajiwa.

Karibu.
 
Boss hii haiwezi kuwa biashara viable.
Umepata wapi tafiti ya hesabu gunia moja la mahindi linatoa mafuta kiasi gani?
Gunia moja la KG 100 haliwezi kutoa lita 10 ya mafuta mzee. Sasa gunia la mahindi ya njano la kilo 100 unaijua bei yake?
Kama gunia moja linauzwa 100k na litoe lita 10. Lita 10 itauzwa shilingi ngapi?
Ndio maana unaona mpaka leo hatuna mafuta ya karanga unajua ni kwanini?
Gunia moja la karanga la kilo 60 linauzwa 170,000 na gunia hilo hilo ukikamua linatoa lita 15 za mafuta.
Lita moja ya mafuta ya karanga iuzwe shilingi ngapi ili tupate faida?
Mimi nipo kwenye industry ya mafuta ya kula ya alizeti nina plant najua ninachokiongea.
 
Lita moja ya mafuta inahitaji mahindi kiasi gani? Isije ikawa unauza Ng'ombe kwa kesi ya kuku
Kwa muhitaji anaweza ingia ndani kabisa kwa kufanya tafiti kuhusu ujazo, kemikali itumikayo kufanya bidhaa isiharibike, kiwekeo, usajiri wa taasisi na mambo kama hayo. Kwa mambo yote kila kitu ni rahisi na faida ni kubwa kuliko hasara.

Mimi nimefanya sehemu yangu kutoa wazo kwa mwenye kupenda kazi ni kwake.
 
Ila Mungu bana,
Eti mahindi nayo yana Mafuta, wakati tukila Mhindi mikono haibaki na mafuta. Wala ukichemsha mahindi sufuria halibaki na mafuta.
 
Kwa muhitaji anaweza ingia ndani kabisa kwa kufanya tafiti kuhusu ujazo, kemikali itumikayo kufanya bidhaa isiharibike, kiwekeo, usajiri wa taasisi na mambo kama hayo. Kwa mambo yote kila kitu ni rahisi na faida ni kubwa kuliko hasara.

Mimi nimefanya sehemu yangu kutoa wazo kwa mwenye kupenda kazi ni kwake.
Wewe umejenga wapi hicho kiwanda au unalimia wapi mkuu?
 
Mkuu kunashida gani tukiendelea kuyala humo kwwnye ugali kama tunavyoyala hivi sasa? Kwanini tusirndelee kuhangaika kukamua mafuta ya pamba na na alizeti ambavyo kiukweli hatuwezi kuvila.
Tatizo kuna uhaba wa upatikanaji wa mafuta na maisha kwa wananchi imekuwa mtihani.

Wananchi wananunua vibaba vya mafuta kuendesha maisha inauma sana na sio jambo la kupendeza abadani.
 
Boss hii haiwezi kuwa biashara viable.
Umepata wapi tafiti ya hesabu gunia moja la mahindi linatoa mafuta kiasi gani?
Gunia moja la KG 100 haliwezi kutoa lita 10 ya mafuta mzee. Sasa gunia la mahindi ya njano la kilo 100 unaijua bei yake?
Kama gunia moja linauzwa 100k na litoe lita 10. Lita 10 itauzwa shilingi ngapi?
Ndio maana unaona mpaka leo hatuna mafuta ya karanga unajua ni kwanini?
Gunia moja la karanga la kilo 60 linauzwa 170,000 na gunia hilo hilo ukikamua linatoa lita 15 za mafuta.
Lita moja ya mafuta ya karanga iuzwe shilingi ngapi ili tupate faida?
Mimi nipo kwenye industry ya mafuta ya kula ya alizeti nina plant najua ninachokiongea.
Brother hili ni wazo na lipo tangu zamani sana kabla hujaijua alzeti kama zao la mafuta kwa taarifa fupi.

Watu wengi wanafanya vitu baada ya kusikia sio baada ya kufanya tafiti.

Karibu.
 
Habari Tanzania !

Kwa wewe mzalendo au mpenda biashara nakusihi unaweza anzisha kiwanda cha mafuta ya kula kwa kuchakata mahindi kuwa mafuta.

Katika bidhaa hii mahindi ya njano ndio malighaifi pekee inayochakatwa na kuwa mafuta ya kupikia kwa kukamuliwa na mitambo.

NB

a) Mahindi yapo.
b) Ardhi ipo ukitaka kulima.
c) Mtaji ni mdogo sana kuanzisha na kukiendesha kiwanda.
d) Soko la mafuta ya kula / kupikia lipo.
e) Kazi ni kwako boss mtarajiwa.

Karibu.
Acha kudanganya watu kusema mtaji mdogo, wet milling inahitaji capital ya kutosha mzee, pia kiasi cha mafuta kinachopatikana ni kidogo sana maana mafuta yanatoka kwenye kiini pekee ila inasaidia kupunguza costs za uzalishaji wa unga kwa kuwa katika dry milling kiini hupotea
 
Back
Top Bottom