Raha ya ndoa NI NINI?

Raha ya ndoa NI NINI?

Mnagombana kila siku kwasababu kila mmoja wenu anajiona mbora kuliko mwenzake,hakuna anayemsikiliza mwenza na wote hamjui kujishusha.
 
Niliyoyaona kwa wazazi wangu ni tofauti na unayotaka kutuaminisha...!!!:A S 39:
 
Mnagombana kila siku kwasababu kila mmoja wenu anajiona mbora kuliko mwenzake,hakuna anayemsikiliza mwenza na wote hamjui kujishusha.

Na ikitokea mmoja akawa anajishusha ndo atageuzwa kondoo wa kafara, Hilo ni tatizo.
 
Mwalimu gfsonwin anataka kutuletea ya kwake yaliyomshinda kama ni yetu wote na sijui huo utafiti kaufanyia wapi kuja na results kama hizo Mentor umeona eehhh

huyu kila siku majanga mara na divrce mara mke kaniibia mara sijui nnina HIV SASA anataka kutuambia nini??
 
Na ikitokea mmoja akawa anajishusha ndo atageuzwa kondoo wa kafara, Hilo ni tatizo.

Unless huelewi unajishusha katika mazingira gani. Sasa mtu amefanya kosa unajishusha ili iweje.Muktadha ninaozungumzia ni kwa vile confrontations za kawaida aise.
 
Maisha ya ndoa si mateso kama unavyodhani bali hubadilika kuwa mateso pale wanandoa wanaposhindwa kuelewa nini maana ya wao kuamua kuishi pamoja kama mume na mke,kuna mafunzo ambayo wanandoa huyapata kabla ya kuoa na kuolewa na wengi wa wanandoa siku hizi hawayazingatii mafunzo hayo na ndio maana tunaona ndoa hazidumu na zinazodumu basi ujue wanandoa wanaogopa tu kuachana na kufanya ndoa zao kuwa mateso badala ya raha.
Hakuna ndoa isiyo na changamoto za hapa na pale lakini kama mume na mke mnajua umaana wa ninyi kuwa pamja basi ndoa ni raha sana na maisha ni rahisi na yenye afya.
 
gfsonwin,hakuna mtu anaeweza kukupa furaha,furaha unayo mwenyewe.Hivyo ndoa haina furaha,lakini furaha ndo hisia ya juu kabisa inayomfanya mwanadamu kujisikia bora,mwenye afya na akiwa na furaha ataiona maana ya maisha.Namna ya kuipata furaha ni kujikubali kama ulivyo na kujitazama na kujipima kwa ubinadamu wako na sio kitu kingine cha nje yako.Ukishapata ridhiko la ndani utaanza kuhisi tofauti na utajiona si mwenye visirani tena.Hapo utaanza kuipata furaha.. . . . Raha ni kitu cha muda,kinakinaisha,hakuna tofauti kati ya raha na utamu.Unapopanda gari zuri au kulala kwenye kitanda kizuri unapata raha,lakini ukishazoea raha huisha. . . . Nikija kwenye swali lako,raha ya ndoa sio kitu kimoja ni vingi,baadhi umeviorodhesha hapo kwenye thread yako,ila navyo hukinai na kuna wakati mtu huiona ndoa haina maana.Yes,unaiona ndoa haina maana kwa sababu wengi kama sio wote tunawekeza kwenye vitu hivyo,tunadhani ndivyo vinamfanya mtu aifurahie ndoa.Badala ya kuwekeza kwenye raha,wekeza kwenye furaha na maswali yako yatapata majibu sahihi!

critical analysis

huwa napenda comments zako
noted
 
siku hizi ndoa zimekuwa zikifungwa nyingi sana tena kwa mbwembwe tafautitofauti.Swali langu ni ndoa ya ukweli ni ipi au ya yule mwanamke unayefunga naye kwenye nyumba nyumba ya ibaada lakini watu kibao walishaonja tunda ikiwezekana hata mfungishaji wa ndoa. Au yule mwanamke bikira unayemchukua bila kumpeleka nyumba ya ibada?
 
Ndoa ya kweli ni ile uliyoiridhia moyoni mwako na mwenza wako karidhia moyoni mwake, haijalishi imefungwa kwenye sinagogi, mtoni au chini ya mti.
 
Ndoa ya kweli ni ile uliyoiridhia moyoni mwako na mwenza wako karidhia moyoni mwake, haijalishi imefungwa kwenye sinagogi, mtoni au chini ya mti.



Ni kweli mkuu, km hamjaridhiana kutokana na mmoja wao kulazimishwa ama kwa kuwa unapesa ni bure, hiyo c ndoa bali ndoano
 
Wana jamvi, ni wiki mbili tu nimeshuhudia ndoa saba,mpya zimevunjika tena kwa matatizo ya kitoto,hasa wanawake nimechek sources ya ndoa zote kukatika ghafla na kwa mda mfupi,maana zote ni changa yaani mtoto mmoja au miaka isiyozidi miwili TUAMBIANE
 
Wana jamvi, ni wiki mbili tu nimeshuhudia ndoa saba,mpya zimevunjika tena kwa matatizo ya kitoto,hasa wanawake nimechek sources ya ndoa zote kukatika ghafla na kwa mda mfupi,maana zote ni changa yaani mtoto mmoja au miaka isiyozidi miwili TUAMBIANE

Matarajio ya pande zote hayakukidha walikurupuka labda!
 
Tatizo wanaoana fasheni..show off..wakipeana mimba tu ndoa..no love wanakuwa forced na environment
 
Unajua katika maisha ya mahusio kuna vitu viwili Ndoa na Harusi, sasa huwa wanapishana bila ya kuelewa mmoja kati yao anakuawa anaitaka harusi na mwengine anahitaji ndoa
 
Back
Top Bottom