Raha na karaha ya bia ya Sita

Raha na karaha ya bia ya Sita

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
561
Kwa wanywaji wazuri wa bia, chupa ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo. Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

Baada ya kumaliza chupa ya pili kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wagonjwa wa Ebola waliopona katika nchi ya Liberia. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.

Bia ya nne huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia, bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu, na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa' au ' Mume wangu sijui yukoje hanijali'

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo ---- na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.


Global Publishers
 
Huu utafiti ukiupeleka UD utapewa kuwa doctor maana umetulia na ni ukweli.
 
Wiki ijayo uje na research juu ya bangi kuanzia stick ya kwanza hadi ya nne,dry na mixer.
 
Kimsingi ikifika bia ya nne pombe huwa zinahamia chini,hasa kwa mademu.
 
Lyinga mkuu ulikuwa na uwezo wa ku komenti bila ku kote! Watu kama nyinyi huwa mnatuboa sisi ambao tunatumia cm za kichina! Badilika mkuu! Sorry lkn!
 
Duh, huu utafiti wako mkali, japo haujazingatia uchungu wa bia ya kwanza, bia mawazo, inakushawishi unywe mbili tu huku ya pili ikikufanya utambue utaalamu wa brewers kukifanya kinywaji hiki kuwa kitamu.

Bia ya tatu inakukumbusha kutizama muda na kukushauri bado kidogo au uhame kiwanja uende mahali penye bendi au shoo. Ongeza moja zaidi

Bia ya tano uko sahihi na utamu wa bia unaongezeka, mchanganyiko wa asali na korosho. Hapa lugha pekee unayoweza kuielewa ni kiinglishi potelea mbali
 
Wengine tunakunywa viroba, mchanganuo unakuwaje hapo?
 
kweli nimeamini kutoa mada ni kipaji, mada sikuipenda ila jamaa kanogesha mada hadi nimecheka ofisin
 
yani umeikopi humuhumu then unaipost humuhumu. Jana ilipostiwa humu'
 
Ah m nakula bia apa nmetumiwa wasap nkaileta tu... sijui hata kama imo
 
Hizo ni kwa wanaojifunza kulamba bia lkn kwa mm fundi hata kret inaisha bila hata kukosea chochote!!!!!
Wanywaji hoooyeeee!!!!
Ni Ijumaa nimekaa nalamba Sengeretiiii karibun mniunge mkono ImageUploadedByJamiiForums1414173400.366669.jpg
 
Back
Top Bottom