Akikukatalia ku-sex usilazimishe, unaepushwa na majanga

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
878
2,428
Kwa vijana hasa vidume wenzangu....

Niliingia Tanga mwaka jana mwanzoni, ugeni ni upofu nikakurupuka nikamtongoza binti flan wa mtaa wa pili ni muajiriwa wa serikali.

Huyu binti ni mweupe, mrefu kiasi na ni mwembamba anamsambwanda kiaina. Alinivutia sana to be honest.
Basi nikaanza kumpangia mikakati ya kumpata maana alikuwa ananiringia sana na mizungusho kama yote.

Nilikaza mwisho wa siku mchumba akakaa kwenye line.
Mida yake ya kupatikana ilikuwa ni jioni kwanzia saa12 na siku za weekend.
Nilianza kumshawishi tukutane geto au lodge ili tupate kuenjoy mautamu ya dunia.
Kwa jinsi huyu Binti alivo na nilivomsumbukia basi nilikuwa na vibe naye sana na nilikuwa nimepanga kumpiga show Kali sana na nilisahau kabisa swala la kupima.

Siku hiyo bhana nilikuwa nimetoka kazini nikawa kwangu tu nimechill naperuzi jamii forum nikaona nimchek Binti nimkumbushe juu ya ombi langu la kukutana. Binti akajaa akanambia kesho yake saa kumi jioni nilifurahi kinoma nikajiona mtu mwenye bahati sana.

Kesho yake alikuja kwangu nilikuwa nimepika zangu wali na nyama ya kuku kienyej na mandondo mixer mboga ya majani.
Nilipika makusud ili mchumba aje tule hafu tule tena.

Baada ya kumaliza kula nikaanza uchokozi, katika kumchokoza tukawa tunapiga stors hasa kuhusu details zetu familia zetu na mambo kama hayo.
Nilimshawishi tukaingia bedroom, Moja kwa moja kitandani.

Binti alikuwa ananikubalia kukagua kila Kona lakin french kiss alikataa.
Nikakazana kumregeza kupitia touches na mbinu zingine.
Binti asalim amri, Ile nataka kuinsert dudu la yuyu binti alinisukuma kwa nguvu mpk kidogo nipige kichwa chini maana nilifika mpka kwenye ukingo wa kitanda ilibaki sentimita chache nianze safar ya kufika chini.

Ile kitu ilinishangaza sana, baada ya pale nikaona Binti kabadirika kavaa nguo fasta akasepa bila hata kuaga.

Nikabak najiuliza nimekosea wapi? Au ninamikosi gani? Au nini shida? Nikakosa majibu.

Baada ya pale nilikuwa nilimtafuta hajibu mesej na cm hapokei.
Hakutaka kuwa karibu tena namimi.

Zilipita weeks kadhaa, siku moja nikawa naenda kumchek jamaa flan anashugulika na watu wenye VVU kuwafatilia watumie dawa vizur, Huwa anazunguka huku na kule kupima watu na wanaobainika na VVU anawapa elimu na kuwaanzishia dawa. Jamaa yupo na shirika flan ndo kaajiriwa huko.

Sasa siku hiyo nipo na huyo jamaa restaurant tunapata lunch cm tulikuwa tumeweka mezan. Simu yake ukaanza kuita na nilifanikiwa kuona nan alikuwa anapiga.
Nilishangaa kuona ni yule binti ndo alikuwa anampigia jamaa. Namba na jina vyote vilikuwa vya yule binti.

Nilisita kumuliza jamaa kuhusu yule binti kwasababu ni ngumu na si vzr wataalam wa afya kudisclose details za wateja au wagonjwa wanaoshugulika nao au kuwahudumia hasa hawa wa VVU.

Nilifanya utafiti wangu kwa kina na nilikuja kugundua huyu binti ni m-VIU na alikuwa anatumia dawa tayar.
Nilimshukuru kimoyomoyo na nikapanga nimtafute na nilazimishe kuonana naye ili nimuweke karibu namm maana niliona ni mtu mzuri na hakutaka kunipa VVU.

Lakini nikakosa namna ya kumuingia na niliona kama vile ningemcost jamaa yangu kwani angeona kama vile yeye ndo kanambia kuhusu hali yake kwasababu anajua kwamba mimi na jamaa tunafahamiana na na kuna ukaribu kati yetu.

Kijana sometimes dem akikunyima hasa mkiwa hamjapima na ukawa hauna ndom it's better ukawa mpole usifosi utayakanyaga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom