Rafiki yangu kaombwa mkopo na mke wa mtu

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Waungwana nawasalimia.

Leo kuna rafiki yangu yeye ni Mfanyakazi wa Serikalini maskani yake ya kazi ni Dodoma.

Leo kanifuta kuomba nimpe loan ya laki 5 ana shida nayo ya haraka sana. Sikutaka kumpa mpaka nijue ni haraka gani imempata ndio akaja na habari ya kushangaza kabisa kuwa namkopea rafiki yake wa kike ambaye ni mke wa mtu. Nilimuangalia jamaa yangu wala sikuelewa kakamatwa na nini.

Nikamuuliza huyo dada ambaye ni mke wa mtu wanajuana akasema hapana. Ila wanachati kupitia META ila hawajawahi kuonana! Sijui huyu jamaa karogwa na nini maana namjua kichwani yupo mzima hasa.

Nikasema acha nimtengenezee mazingira magumu. Nikamwambia pesa ipo ila ina riba ya 20% ndani ya wiki mbili pia aniachie kadi ya gari lake. Nimempa sharti gumu na nimpe ushauri wa kina sana. Afanye uchunguzi wa kina. Nimemtahadharisha matokeo hasi ya kumkopesha pesa mke wa mtu.

Nimemwambia pia kama ni kweli wana urafiki tu na sio mahusiano ya kimapenzi amshirikishe mumewe. Sijui kuna watu wana wazimu, unakutana na mtu META ama hapa JF mnaanza kukopeshana? Mungu ampe ufunuo ndugu yangu aachane na hio habari maana kaaondoka kanuna sana.
 
Kaondoka kanuna kwani hakuafikiana na hayo masharti uliyompatia?

Na kama hakukubaliana alitoa maoni gani?

Ujue yaweza kuwa huyo mwanamke ni hawara yake, kashindwa tu kukupa ukweli kwa kuwa mahusiano hayo ni ya aibu.

Kukopesha hawara huwa ni kuhonga, hilo linafahamika tangu enzi na enzi.

Hati ya gari umempa sharti jepesi sana hilo, mwambie akukabidhi hati ya nyumba, tena mkataba huo ahusishwe na wakili ili asije kukugeuka.
 
Kuna mmoja ambaye alikuwa mpangaji mwenzangu huko mkoani kataka nimkopeshe 50 elfu ili aende msibani kijijini lakini ananambia tafadhali sana mmewe asijue kama kanikopa ela.

Sasa nikawaza kwenye purukushani za kudaina mmeo si atajua hapo si ndio atakaponigeuka na kupewa kesi ya kutaka kumla mke wa mtu.

Nikaachana nae na kumpotezea mazima.
 
META ndo Nini? We sema Facebook jamaa hawajabadilisha jina la app wamebadili jina la kampuni tu, lakin insta, Whatsapp, messenger & Facebook zinaendelea kutambulika kwa majina yake hayohayo

Alaf kma kaombwa hela na mwanamke wa Facebook ampigie vdeo call ahakikishe picha anayoiona ndo picha ya anaeongea nae kwa vdeocall vinginevyo anachat na mwanaume mwenzake anaetumia picha ya mwanamke haijui fesibuku vizuri huyo
 
META ndo Nini? We sema Facebook jamaa hawajabadilisha jina la app wamebadili jina la kampuni tu, lakin insta, Whatsapp, messenger & Facebook zinaendelea kutambulika kwa majina yake hayohayo....
Ukikua na ukijua kiingereza utajua baadae. Lakini kwa kiwango chako hiki cha kudhani bila na uhakika utapotea. Rudi shule.
 
PM Jina Na Number Ya Simu Ya Huyo Jamaa Yako Anayetoa Mikopo Chechefu
 
Usijaribu kumpa mkopo mwanamke ata awe na nani.

Kuna mdada aliniomba nimkopeshe 1m kwa ajili ya ada za watoto wake, tokea mwezi wa tatu lakini mpaka leo sijalipwa.
Kwahiyo kwavile we hujalipwa ndio na wengine wasisaidiwe?? Huoni kama huu ni ubinafsi??
 
Kuna mmoja ambaye alikuwa mpangaji mwenzangu huko mkoani kataka nimkopeshe 50 elfu ili aende msibani kijijini lakini ananambia tafadhali sana mmewe asijue kama kanikopa ela.

Sasa nikawaza kwenye purukushani za kudaina mmeo si atajua hapo si ndio atakaponigeuka na kupewa kesi ya kutaka kumla mke wa mtu.

Nikaachana nae na kumpotezea mazima.
Umefeli...elfu 50 sio hela ya kumnyima mtu aende msibani...tena huyo alisema atarudisha. Hata asingelipa sio ishu
 
Kuna mmoja ambaye alikuwa mpangaji mwenzangu huko mkoani kataka nimkopeshe 50 elfu ili aende msibani kijijini lakini ananambia tafadhali sana mmewe asijue kama kanikopa ela.

Sasa nikawaza kwenye purukushani za kudaina mmeo si atajua hapo si ndio atakaponigeuka na kupewa kesi ya kutaka kumla mke wa mtu.

Nikaachana nae na kumpotezea mazima.
50 nayo Unamaindi? Ningempa bila kuidai. Wewe inaelekea unakulaga mizoga isiyodai pesa kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom