KATASAN'KAZA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 3,097
- 1,356
Kuna imani nyingi juu hawa watu.Kwani ni nini hatari?
$wissme
Jamani we acha bwana...Ungemwambia jamaa yako amuulize huyo demu wake atakufa baada ya muda gani.!!
Sawa, ila sasa ndiyo hivyo huu ugonjwa ni kurithi watoto pia wanaweza athirika, inakuwaje hapa??Mkuu huyo jamaa mwambie asithubutu kumnyanyapaa kisa ana Sickle Cell.. magonjwa ni mengi skuhizi mwambie hata yeye anaweza pata Heart attack at anytime na akaondoka au akapata Cancer,Ebola, Kisukari au hata ugonjwa mwingine wowote.
Mtaani watu wanawadiss watu wenye HIV alafu wao wanaondoka na pressure daily.
Hapo sasa watoto, ingawa lazima wote muwe carriers.MwanaFA nasikia pia ana sickle cell
Sidhani kama ni ugonjwa wa kuuogopa sana
Ila tatizo linakuja kuwa nasikia unaweza kurithishwa kwa mtoto
Duuuh! Jamani mbona jamaa nikimwambia haya atamwacha ni mkubwa yuko 22 sasa hivi.Kama huyo shemeji yako ameshavuka miaka 22 basi life expectancy yake ni sawa na ya mtu mwingine wa kawaidia. Kawaida wanasema mtu mwenye sickle cell akivuka miaka 18 basi huwa anakuwa na life span ya kawaida. Lakini mimi napinga hili kwa sababu nilimpoteza rafiki yangu kwa sickle cell akiwa na miaka 22.
Kitu ambacho rafiki yako anatakiwa afahamu ni kwamba sickle cell ni ugonjwa wa kurithi hivyo watakapojaliwa watoto kuna uwezekano mkubwa mmoja wa watoto akawa na sickle cell. Mungu akawabariki na wajukuu, uwezekano wa mjukuu mwenye sickle cell upo pia.
Shemeji yako nahitaji matunzo mazuri na care ya hali ya juu, hatakiwi kuwa stressed maana stress huwa zinawaletea matatizo ya pumzi.