Rafiki yangu anatembea na mke wa mtu

Rafiki yangu anatembea na mke wa mtu

Ili iweje hapo kwenye rangi? Ikitokea jamaa akaenda kumuua mshikaji wako utajisikiaje? Umeshatoa onyo inatosha mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe hayakuhusu.

Habari wana jamvi. Nimekuja hapa kuomba ushauri kwenu ili niweze kumsaidia rafiki yangu ambae amezama kwenye penzi la mke wa mtu. Nimejaribu sana kumshauri mpaka imefikia kipindi sasa hivi hatuongei kabisa kwa sababu ya jambo hilo.

Mume wa huyo dada alishawahi kumtafuta rafiki yangu kwa kumpigia simu akimtaka aachane na mke wake lakini rafiki yangu amekuwa mjeuri hasikii. Ndoa yao imekuwa haina amani kabisa ni ugomvi kila kukicha mpaka jamaa amekuwa mlevi kupindukia kwasababu mkewe hatulii.

Sasa nimepanga nimfungie mume wa yule dada nimwambie ukweli nimuelekeze jamaa mpaka kwao na mshkaji. Sasa najiuliza nikimwambia yule mume wa yule dada je mshkaji hatoniona msaliti?na pia kuacha bila kufanya kitu kuokoa ndoa ya wale watu moyo unanisuta maana anayesababisha matatizo namjua ni kiasi cha kumtaji ili aache kuharibu ndoa ya watu.

Naomba ushauri nifanye nini kuwasaidia wote wawili, yaani rafiki yangu aachane na mke wa mtu na pia kumsaidia jamaa kurudisha ndoa yake maana wana watoto wawili na anampenda sana mke wake.
 
Achaga umbea na ww khaaaa....fanya yako kila mtu atabeba fulushi lake
 
Mke wa mtu, jamani Mke wa mtu.

Ogopa Mke wa mtu.

Heshimu Mke wa mtu
 
Kila mchuma janga hula na wa kwao. Mwache mwenyewe. Umesha muonya hasikii. Ukimwambia mme wa mtu akimuua rafiki yako nafsi itakusuta mara nyingi zaid
 
Umeshamweleza na kumshauri ya tosha yatakayotokea baada ya hapo nawe kuwa mbali
 
Haya ma thread ya Hivi yameshakuwa mengi mno sasa Hivi, Ni kama watu wanatafuta attention ya watu kuchangia. Upumbavu tupu huu, kila siku kila Saa natembea na Mke wa MTU natembea na Mme wa MTU, ushenzi tu.

Tembeeni nao tu mkipata mnachotaka mtaacha
 
Mfate mwanamke mwambie aachane na rafiki yako...mke anauma asee,asikwambie ntu.
 
Back
Top Bottom