mzuluu
Member
- Sep 15, 2014
- 68
- 30
Habari wana jamvi. Nimekuja hapa kuomba ushauri kwenu ili niweze kumsaidia rafiki yangu ambae amezama kwenye penzi la mke wa mtu. Nimejaribu sana kumshauri mpaka imefikia kipindi sasa hivi hatuongei kabisa kwa sababu ya jambo hilo.
Mume wa huyo dada alishawahi kumtafuta rafiki yangu kwa kumpigia simu akimtaka aachane na mke wake lakini rafiki yangu amekuwa mjeuri hasikii. Ndoa yao imekuwa haina amani kabisa ni ugomvi kila kukicha mpaka jamaa amekuwa mlevi kupindukia kwasababu mkewe hatulii.
Sasa nimepanga nimfungie mume wa yule dada nimwambie ukweli nimuelekeze jamaa mpaka kwao na mshkaji. Sasa najiuliza nikimwambia yule mume wa yule dada je mshkaji hatoniona msaliti?na pia kuacha bila kufanya kitu kuokoa ndoa ya wale watu moyo unanisuta maana anayesababisha matatizo namjua ni kiasi cha kumtaji ili aache kuharibu ndoa ya watu.
Naomba ushauri nifanye nini kuwasaidia wote wawili, yaani rafiki yangu aachane na mke wa mtu na pia kumsaidia jamaa kurudisha ndoa yake maana wana watoto wawili na anampenda sana mke wake.